Binadamu tunayo nguvu ya kufanya vitu vya kushangaza sana lakini hii nguvu tuliyonayo ndani yetu huwa hata hatuitumii vile ipasavyo.
Ili uweze kutumia nguvu za ajabu zilipo ndani yako unapaswa kuwa na kitu hiki kimoja ambacho ukiwa nacho utafanya yasiyowezekana hata kama watu wanaona hayawezekani.
Tunaweza kuwa na nguvu ya ajabu ndani yetu kama tukiwa na imani. Tukiwa na imani tutaweza kufanya mambo ya kushangaza na yasiyowezekana.
Tunashindwa kufanya makubwa kwa sababu ya kukosa imani ndani mwetu. Tunayo nguvu ya ajabu na za kushangaza ila hizi nguvu haziwezi kudhihirika ndani mwetu kama tumekosa imani.
Imani ni uhai wa mtu unaomsaidia kuishi vizuri kiakili, kiroho na kimwili. Tukiwa na imani hofu na mashaka vinakimbia vyenyewe lakini tukikosa imani kwenye maisha yetu tunakuwa tunakaribisha kila aina ya matatizo.
Mtu akishapoteza imani ya maisha yake ni mtu hatari ambaye anakua ameshajichokea na maisha hivyo anakua yuko tayari kwa lolote kwani anakua ameshakata tamaa.
Ukitaka kuwa mtu wa miujiza kuwa mtu wa imani na utafanya miujiza mingi sana kwenye maisha yako.
Wewe ni nabii wa maisha yako na huwezi kuwa nabii mzuri wa maisha yako kama hauna imani za kufanya miujiza.
Utaishangaza dunia endapo utakua ni mtu wa imani na ukiwa mtu wa imani utapata nguvu za kufanya makubwa.
Hatua ya kuchukua leo;
Tumia nguvu ulizonazo ndani mwako kwa kuwa na imani ya kuamini kufanya makubwa.
Ukiwa na imani utafanya miujiza mingi.
Kwahiyo, yasiyowezekana yanawezekana kama ukiwa na imani. Kiasili unazo nguvu za kuishangaza dunia endapo utatumia imani yako vizuri katika hali ya uchanya.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo