Jinsi Ya Kufanya Kisichowezekana Kadiri Ya Mt. Fransisco

Kinachoshindikana kwako, kwa mwingine kinawezekana. Watu tumezidiana uwezo, kitu ambacho kwako unakiona ni kigumu kwa mwenzako ni kirahisi. Hakuna kitu kigumu bali ugumu uko kwa mhusika mwenyewe. Kama hesabu watu wanasema ni ngumu lakini mbona kuna watu wanaifaulu vizuri? Hapa ndiyo tunajifunza dhana hii kwamba hakuna kitu kigumu bali ugumu uko kwa mhusika mwenyewe. Unaweza …

Jinsi Ya Kujitofautisha Na Wafanya biashara Wengine

Kwanini mteja aje kununua kwako na siyo kwa mtu mwingine? Hilo ndiyo swali unalopaswa kujiuliza kwa kila mfanya biashara. Wateja wengi hawanunui kwa sababu ya kukuonea huruma bali wateja wananunua kwa sababu ya shida zao, kuna thamani ambayo wanaitaka kutoka kwako. Ili kujitofautisha na wafanya biashara wengine hakikisha kwanza unakuwa na kitu cha ziada. Unatakiwa …

Pale Unapojikuta Njia Panda

Kuna wakati unajikuta njia panda, una mambo mengi ya kufanya halafu hujui ufanye lipi na uanze lipi. Unapojikuta katika hali kama hiyo, siku zote unashauriwa kufanya kile kilicho sahihi kwako kufanya. Kumbe basi, Unapojikuta njia panda na hujui lipi la kufanya wala usipoteze muda wako, bali wewe nenda kafanye kile kilichokuwa sahihi kwako kufanya. Siku …

Huyu Ndiye Mtu Wa Kwanza Wa Kukutia Moyo

Huwa tunakutana na changamoto nyingi sana kwenye maisha yetu. Na inafikia wakati tunajikuta tunataka kukata tamaa kwa sababu za kibinadamu. Wengine wanavunjika mioyo katika utendaji wao wa kazi kutokana na makwazo wanayopitia makazini. Yapo mengi tunayokutana nayo, katika maisha, zipo changamoto tunazokutana nazo katika kazi, biashara, mahusiano yetu, malezi ya watoto na nk. Licha ya …

Sehemu Pekee Unayoruhusiwa Kuchepuka

Si halali kuchepuka katika mahusiano bali ni halali kuchepuka eneo la kipato. Unaruhusiwa kuchepuka katika eneo la fedha, kama unaona kiwango cha fedha ulichokuwa nacho hakikutoshi hujafungwa bali tafuta fedha zaidi. Hakuna mtu atakayekufunga kwa wewe kutoa thamani kubwa na kisha kupata fedha zaidi. Matumizi yakiwa makubwa usilalamike ongeza kipato. Kuna wakati unaweza kubana sana …

Chagua Moja Kati Ya Hivi

Dunia huwa haina huruma, inamwadhibu mtu kadiri ya uzembe wake na inamlipa mtu kadiri ya thamani yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia fedha ambazo hawana kununua vitu ili kuwafurahisha watu wasiojali. Leo ninakuomba kitu kimoja, uchague kuwafurahisha watu uendelee kuwa masikini au ujinyime na kuwa tajiri. Huwezi kutoka katika umasikini bila kuishi tabia za kitajiri. Chagua …

Huyu Ndiye Rafiki Wa Kweli

Kila mtu ana rafiki yake wa karibu lakini licha ya kuwa na rafiki wa karibu bado huyo rafiki anaweza kukuangusha pia. Yuko rafiki wa kweli, ambaye hajui kuangusha watu pale unapokuwa na shida na rafiki huyo siyo mwingine bali ni kazi. Kazi ni rafiki wa kweli kwa sababu anakupa kile unachotaka. Ukifanya kazi, utapata fedha …

Kamwe Usiogope Kuwa Mtu Huyu

Ni wangapi tokea wazaliwe hawajawahi kuishi maisha yao?Je maisha unayoishi sasa ndiyo maisha yako halisi? Kile unachofanyia kazi sasa ndiyo ndoto unayoishi? Wengi wamepotea kwa kutokuishi ndoto na hata maisha yao halisi.Maisha ya watu wengi ni maigizo matupu. Tuko radhi dunia ituone sisi ni watu wanaoenda na fasheni, tukope fedha ambayo hatuna kununua vitu ambavyo …

Epuka Kutumia Lugha Hii Ya Ufundishaji Katika Malezi Ya Watoto

Wanasema watoto ni malezi, je malezi unayowapa watoto wako yanawawezesha kusimama kwa miguu yao wenyewe hapo baadaye? Unawapa misingi au unawalea ili mradi tu?Zawadi nzuri ya kumpatia mtoto ni kumpa malezi bora ambayo hatoweza kuyapata sehemu nyingine yoyote ile. Hata kama mzazi umekosa vitu vyote bado unayo nafasi ya kutoa upendo kwa watoto wako. Na …

Ni Bora Kufa Kwa Kitu Kuliko Kuishi Bure

Ni bora upambane kwa kitu kuliko kutokupambana.Ni bora uwe na kitu cha kusimamia kuliko kuishi bila kuwa na kitu cha kusimamia. Kuwa na misingi michache ambayo itakuongoza kwenye kila eneo la maisha yako. Usiwe kama bendera fuata upepo. Huwezi kuwa na ushawishi kama huna kanuni na msingi. Watu huwa wanavutiwa na watu ambao wanaushawishi tayari …

Design a site like this with WordPress.com
Get started