Kama Unataka Kujinyanyua Juu…

Binadamu hatufanikiwi kwa miujiza, Bali sheria ya asili inafanya kazi yake. Kama alivyowahi kusema Jim Rohn, ukitaka kufanikiwa wasaidie au wawezeshe wengine kwanza kupata kile wanachotaka na wewe utafanikiwa. Ni hivyo tu ,wala hakuna njia ya mkato rafiki yangu. Ukitaka Kujinyanyua Juu wewe mwenyewe, basi anza kuwanyanyua juu watu wengine. Unapowanyanyua wengine nawe unanyanyuka. Unapomsaidia …

Hii Ndiyo Faida Ya Jawabu La Upole Kwa Mtu Ambaye Ana Hasira

Mpendwa rafiki yangu, Sisi binadamu tunayo mamlaka ya kudhibiti hisia zetu lakini hatuwezi kuzuia tusiwe na hisia. Unaweza kudhibiti hasira lakini huwezi kuzuia usiwe na hasira. Kwa mfano, kitu chochote cha hasira kikitokea unaweza kujidhibiti kutochukua hatua pale unapokuwa na hasira ambayo inaweza kuleta madhara. Leo tunakwenda kujifunza jawabu la upole linavyoleta mafanikio katika maisha …

Hiki Ndiyo Kitu Pekee Ambacho Teknolojia Hakizalishi

Tunashukuru kwa uwepo wa Teknolojia duniani. Ni msaada mkubwa sana miongoni mwetu, hili halihitaji sababu nyingi kuthibitisha hilo. Teknolojia inawasaidia watu wengi kuwa matajiri katika zama hizi. Watu wanatengeneza koneksheni mbalimbali kupitia teknolojia ambayo tunaitumia leo hii katika maisha yetu. Dalai Lama aliwahi kunukuliwa akisema, ninafikiri kweli teknolojia imeongeza uwezo wa binadamu. Lakini, teknolojia haiwezi …

Mafanikio Yoyote Yale Kamwe Hayaji Kwa Njia Hii

Kwa asili tu hakuna kitu kinachotokea kwa njia rahisi, asili huwa haifanyi kazi kwa njia za miujiza ya haraka hata siku moja. Kwa mfano, ulishawahi kuona mwembe umepandwa leo na leo uzae? Vipi sisi binadamu tunafanya kazi leo na tunataka mafanikio ya haraka? Asili ndiyo inaleta mafanikio ya kweli na ya uhakika. Hakuna mafanikio yanayokuja …

Usiweke Mayai Yote Kwenye Kapu Moja

Ni usemi maarufu sana katika uwekezaji.Ukiwa na maana kwamba usiwekeze katika eneo moja. Unatakiwa kutawanya uwekezaji wako katika maeneo tofauti tofauti. Inapotokea hatari ya uwekezaji, labda umewekeza kwenye eneo moja utapata hasara sana lakini kama utakua umewekeza maeneo tofauti haiwezi kukuletea shida, haiwezekani maeneo au sekta zote ulizowekeza zikaanguka zote kwa mara moja. Kama uwekezaji …

Jifunze Kujichelewesha Kuchukua Hatua Ukiwa Na Hali Hii

Pale unapojihisi uko kwenye hisia yoyote ile, jicheleweshe kuchukua hatua hapo kwa hapo.Kwa mfano, mtu akikutukana, au akikuambia maneno mabaya kwako, usichukue hatua ya kutaka kumjibu badala yake jicheleweshe ili hasira ziishe kwanza. Jifunze Kujichelewesha, unapojichelewesha unakuwa unazipunguza hasira. Siyo tu kupunguza hasira lakini pia unajifunza kutawala hisia zako. Hatuwezi kuzuia hisia katika maisha yetu, …

Usimchukie Mtu, Bali Chukia Hiki

Katika maisha tunaalikwa tupendane, na pale inapotokea mtu amefanya ndivyo sivyo basi tueleweshane kwa upendo. Kila binadamu ana udhaifu wake, hivyo ukisema umchukie kila mtu kadiri ya udhaifu wake utabaki peke yako duniani na kila mtu utamwona ni mbaya. Chukia dhambi na wala usimchukie mtu. Mtu ataweza kuja kubadilika sasa kama umemchukia maana yake itakuja …

Jinsi Ya Kuwa Mtumwa Wa Sasa

Kati ya viumbe waliopendelewa sana na Mungu basi ni binadamu. Tumepewa akili ambayo inatutofautisha na wengine wote. Ila sasa, changamoto yetu wengi hatutumii uwezo huu mkubwa ulioko ndani yetu. Hebu pata picha hapa, tumeshindwa kuwa kama samaki lakini tukatengeneza vifaa vinavyoelea majini kwa kutumia akili. Tumeshindwa kuruka kama ndege lakini tumetumia akili kutengeneza ndege inayoruka …

Kama Mahusiano Yako Yamekosa Hiki…

Asili ya kila binadamu ametokea katika mahusiano, kila mmoja wetu mpaka tunazaliwa ni wazi tunatokea katika mahusiano ya kama vile kutoka kwa wazazi, ndugu, nk. Mahusiano mengi siku hizi yamekuwa na changamoto kwa sababu ya kutokuishi misingi ya mahusiano. Mahusiano yetu mengi yanajengwa na uaminifu, na sasa kama uaminifu haupo ndani ya mtu maana yake …

Kile Unachohofia Mara Nyingi Kinakuwa Hivi

Mara nyingi kile tunachohofia hata huwa hakitokei. Ni sisi tu binadamu tunapenda kutengeneza mazingira ya hofu ambazo hata kiuhalisia hazipo. Hofu huwa tunaanza kuitengeneza akilini. Tukishaijaza hofu akili na mwili unapokea matokeo yake tunashindwa kuthubutu na kufanya kile tulichochagua kufanya. Dawa ya hofu ni wewe kuingia mzima mzima. Bila kujali nini kitatokea, na hata unachohofia …

Design a site like this with WordPress.com
Get started