Maisha ambayo hayana thamani, ni maisha ambayo hayana maana kuishi. Alisema mwanafalsafa Socrates. Chochote kile ambacho unafanya, jaribu kukipima kwanza matokeo ya yale unayopata. Unaweza kujiona unalima na unapata faida kumbe huna unachopata, kaa chini pima je kile unachofanya kinakuletea faida? Iko wazi, kama huna faida unayopata kwenye kile unachofanya basi unapata hasara kwenye kile …
Usiupoteze Muda Huu Bure
Mara nyingi huwa tunapoteza muda pale tunapokuwa kwenye foleni, au tunaposubiria kitu fulani au tunapokuwa kwenye gari. Huu ni ule muda ambao umekufa hatuwezi kufanya kazi. Sasa kama wewe uko gari au foleni usikubali muda ukupitie hivi hivi, Bali tumia muda huo kujifunza kwa kusoma kitabu au kusikiliza vitabu vilivyosomwa. Popote pale unapotembea , tembea …
Jinsi Ya Kufanikiwa Kwenye Karne Ya 21
Msingi wa mafanikio uko wazi kadiri ya aliyekuwa mwandishi na mwanafalsafa Zig Ziglar ambaye anasema wasaidie wengine kupata kile wanachotaka na wewe utafanikiwa kupata kile unachotaka. Katika karne hii ya 21 hakuna muujiza mwingine, naye bilionea wa kichina Jack Ma anaongezea na kusema Kama unataka kufanikiwa kwenye karne ya 21 unatakiwa kuwawezeshe wengine, hakikisha kuwa …
Usalama Wa Mahusiano Yako Ya Ndoa Uko Hapa
Hakuna maisha mafupi hapa duniani kama maisha ya ndoa kwani wote mnakutana mkiwa tayari ni watu wazima. Kama mtatumia maisha ya ndoa yenu kulaumiana na kila mwanandoa kuangalia mabaya ya mwenzake mtakuwa mnavumilia kuishi maisha ya ndoa na siyo kufurahia. Wanandoa ndiyo waamuzi wa mwisho katika mahusiano yao, wao ndiyo wanaamua ni aina gani ya …
Continue reading "Usalama Wa Mahusiano Yako Ya Ndoa Uko Hapa"
Furahia Kile Ambacho Tayari Unacho
Kama umepata nafasi ya kucheka, basi cheka.Furahia kufanya kile ambacho unayo nafasi ya kufanya kwa muda huo. Ukipata nafasi yoyote ile wewe ifurahie kutumia vizuri. Kwa kitendo cha kuifurahia utaweza kuacha alama na kufanya makubwa. Kila kitu kinakuja kwa sababu yake na kikiondoka hakiwezi kurudi tena. Ukifanikiwa kuiona siku mpya basi hakikisha unaiishi vizuri kiasi …
Jilazimishe Tena
Sisi binadamu tumetawaliwa sana na miili yetu. Tunaisikiliza miili yetu na inatuongoza kuamua mambo. Miili yetu kiasili haipendi bughudha, hivyo inapokutana na kitu ambacho kitautesa mwili unapeleka taarifa katika akili ya kukata jambo fulani. Tunatakiwa kuamua mambo yetu kwa njia ya kufikiri na siyo kuupa mwili nafasi, anayeusikiliza mwili wake atakuwa mtumwa wa wengine. Unajua …
Umekubali Mwenyewe Iwe Hivyo
Mara nyingi kile kitu ambacho ni muhimu sana katika maisha yetu huwa tunakipa uzito sana. Lakini kama siyo muhimu tunatengeneza mazingira ya kukichukulia poa. Umekubali mwenyewe kuwa hivyo ulivyo leo. Kwa mfano, kama unasafiri bila hata ya kuweka alamu lazima utaamka tu muda muafaka ili usiachwe na gari na muda mwingine unajikuta hata usingizi huna …
Usiende Kubishana Siku Hii Ya Leo
Usiende kupoteza nguvu zako bure katika kubishania mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Kubishana ni kupoteza nguvu na muda wako. Tumia muda wako kufanya kazi ambayo inakupatia kipato na mambo mengine achana nayo. Unapokuta watu wakibishana juu ya mpira, siasa, udaku wewe nenda kafanye kazi inayofanya maisha yaende. Badala ya kubishania mambo ambayo hayakuingizii …
Jinsi Ya Kujitofautisha Na Wafanyabiashara Wengine
Kufanya kile ambacho kila mtu anafanya hapo unakuwa umejijengea mazingira ya kuchukuliwa poa. Kama wote mnafanya biashara moja, na mteja akija kwako na akienda kwa mwingine anapata huduma hiyo hiyo hapo unakuwa bado huna thamani. Ili kujitofautisha na wafanyabiashara wengine unatakiwa kwenda hatua ya ziada. Unatakiwa kufanya kile ambacho watu wengine hawafanyi. Jijengee kutoa huduma …
Continue reading "Jinsi Ya Kujitofautisha Na Wafanyabiashara Wengine"
Hivi Ndivyo Vitu Saba Unavyopaswa Kuvilinda Kwenye Karne Hii 21
Viko vitu vingi sana ambavyo tunapaswa kuvilinda katika maisha yetu. kazi yetu kubwa katika maisha yetu ni kutengeneza, kukuza na kisha kukitunza. Haifai kutengeneza na kisha kuacha, hapana unapswa kutunza na kukuza kile ambacho umekianzisha au kukitengeneza ndani yako. Leo nakwenda kukushirikisha vitu saba unavyopaswa kuvilinda kwenye maisha yako na vitu hivyo ni kama ifuatavyo; …
Continue reading "Hivi Ndivyo Vitu Saba Unavyopaswa Kuvilinda Kwenye Karne Hii 21"