Huu Ndiyo Wakati Mzuri Wa Kuonesha Uwezo Wako Kwa Wale Wanaokukataa

Ni kawaida katika jamii yetu hata katika maisha ya kawaida hatuwezi kukubalika na kila mtu. Wako ambao wanakuchukia kwa wewe kumzidi, ile chuki ya kwanini wewe upige hatua ndiyo inamsukuma adui yako akufanyie ubaya. Kiasili, dunia haipendi kuona mtu akipata kitu kirahisi hata siku moja. Lazima ujaribiwe, upitie magumu mpaka pale watakapoona kweli una nia …

Acha Kujifunga Kisaikolojia

Tumeshazoea kusikia kauli nyingi ambazo watu wamekuwa wanazitumia kama vile ndiyo kifungo kwao. Kwa mfano, wako watu ambao wanasema hawawezi kuishi bila kunywa pombe. Wako watu ambao wanasema hawawezi kuishi na mwanamke mmoja au mwanaume mmoja, yaani yeye lazima tu atachepuka au kutoka nje ya ndoa. Wako ambao wanasema hawawezi kulala bila kufanya kitu fulani. …

Ukienda Kununua Nguo Sokoni

Kila mmoja wetu hapa ameshawahi kununua nguo ya aina yoyote ile. Ulivyokuwa mdogo wazazi wako walikuwa wanakuchagulia karibu kila kitu. Lakini kwa sasa, hawana tena hiyo nafasi bali wewe ndiyo umekuwa mkurugenzi wa maisha yako ambapo unajichagulia kile unachotaka kufanya. Acha tumchukulie mfano mtu anayekwenda kununua nguo, akifika eneo alipoenda kununua nguo atachukua muda kuchagua …

Katika Biashara Hutakiwi Kuwa Na Kitu Hiki

Kila mtu ni mfanyabiashara kwa asili lakini wengine hawajui namna ya kuongea na mteja. Mtu anamchukulia mteja kama vile mtu wa kawaida tu kwake. Wateja hawatakiwi kuchukuliwa kwa namna ya kawaida, bali wanatakiwa kuheshimiwa kwani wao ndiyo wanafanya biashara yako iwe na uhai, kama hakuna wateja basi hakuna biashara hapo. Wateja ni kama vile gari …

Jinsi Ya Kupata Masaa Ya Ziada Katika Masaa 24 Uliyonayo

Moja ya zawadi ambayo Mungu amempa kila mtu basi ni muda. Tajiri na masikini wote wamepewa muda sawa na kufanya kile anachotaka kufanya. Wote tuna masaa 24 katika siku, hakuna aliye mbele au nyuma na tunapokuja kwenye suala la muda wote tunakuwa sawa. Tofauti yetu inakuja kwenye matumizi ya muda tulionao. Wako ambao wanatumia muda …

Usikubali Anayekuonea Aendelee Kukuonea

Rafiki, Usikubali kuwa mtu wa kuonewa na watu. Na kuchukulia ni kitu cha kawaida tu. "Simamia utu wako na yeyote anayekuonea mfanye ajifunze kwamba uonevu siyo kitu sahihi" Waoneshe wale wote mwenye tabia ya kukuonea kwamba huwezi kuonewa kirahisi. Wafundishe adabu na watajifunza kupitia wewe na wataheshimu utu wako. Binadamu huwa wanatabia ya kukuchukulia vile …

Kabla Hujainyoosha Dunia Fanya Hiki

Huwa tunajikuta tunataka kuwa viraja wa dunia. Mama Theresa aliwahi kunukuliwa akisema, kama unataka kubadili dunia, nenda nyumbani kaipende familia yako. Kama unataka kuibadili dunia anza kujibadili wewe mwenyewe kwanza. Nyoosha kwanza maisha yako kabla hujajipa jukumu la kuinyoosha dunia. Tunayo mambo mengi sana ya yakufanya na kama tungekuwa tunayafanyia kazi basi tungekuwa mbali na …

Mbinu Moja Nzuri Ya Kuokoa Gharama

Ni kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato kinapokuwa kimeongezeka. Huwa tunajidanganya kuwa kama mshahara au kipato kikiongezeka basi shida zetu zitakuwa zimepungua. Kipato kinapokuwa kimeongezeka zaidi na matumizi nayo huwa yanaongezeka. Mwanzoni ulipokuwa na kipato kidogo ulikuwa huoni hata matumizi makubwa lakini shida inakuja pale tu kipato kinapoongezeka yanaongezeka matumizi ambayo hata hukuwahi kuyafikiria. Nikupe …

Kuwa Sawa Na Wengine Lakini Siyo Eneo Hili

Unaweza kuwa sawa kama wengine, ukala kile ambacho wengine wanakula, wanakunywa. Unaweza kuvaa kama vile wengine wanavyovaa, kucheza kama wengine wanavyocheza lakini; Kamwe usiwe wa kufikiri sawa na wengine na kuamuliwa kile ambacho unataka katika maisha yako. Unaweza kuwa sawa na wengine katika maeneo mbalimbali lakini siyo kwenye kufikiri, ili uwe wa tofauti lazima ufikiri …

Mafanikio Yote Yanaanza Kitu Hiki

Sisi binadamu tuna asili ya uvivu ndani yetu, miili yetu huwa haipendi sana shida ndiyo maana hata wakati wa kuamka asubuhi kutoka kitandani unakuwa unapata upinzani mkubwa kutoka katika mwili wako. Mwili huwa unataka kile unachotaka, hivyo ukiwa ni mtu wa kuusikiliza mwili utavuna mabua, mwili hauhitaji uwe mtu wa demokrasia bali udikteta. Mafanikio yote …

Design a site like this with WordPress.com
Get started