Huwa tunakua bize kuwatafuta wengine, tunataka kujua mambo ya wengine yakoje lakini tunasahau sana kutafuta kujua mambo yetu binafsi. Baba wa falsafa mwanafalsafa Socrates aliwahi kunukuliwa akisema, ukitaka kujitafuta wewe mwenyewe, jifikirie kuhusu wewe mwenyewe. Hatuwezi kujua matatizo yetu ya ndani kama tusipojitafuta sisi wenyewe. Tutajua mengi kuhusu sisi wenyewe pale tutakapojitafuta kwa kujifikiria sisi …
Kama ulianguka Jana Fanya Kitu Hiki Leo
Ni kawaida yetu sisi binadamu kuanguka katika mengi, lakini kuanguka siyo sababu ya sisi kuendelea kuwa chini. Kama vile ilivyo dunia, inatupa usiku na mchana nasi tunatakiwa kuishi hivyo. Pale unapokuwa umeanguka unapaswa kunyanyuka juu. Usiendelee kukomaa na hapo chini bali nyanyuka juu. Kama jana ulianguka , unachotakiwa kufanya ni leo kuamka. Kila mtu anaanguka, …
Kitu Pekee Unachoweza Kupata Kwa Haraka
Kama tunavyojua kazi ya haraka inakuwaje na matokeo yake yakoje. Jaribu tu kuchunguza vitu vyote ambavyo vinafanywa haraka haraka na utapata jibu. Shahidi wa kwanza kwenye hili ni wewe mwenyewe, ukiangalia vitu ulivyofanya kwa haraka na vile ulivyofanya kwa umakini kwenda taratibu unaona tofauti ya matokeo. Kitu pekee unachoweza kupata kwa urahisi ni usumbufu. Aliwahi …
Usikubali Kile Usichojua Kufanya Kiingilie Hiki
Kama unajua vizuri utafanya vizuri hii ni kanuni ya asili na kama hujui utafanya vibaya. Kanuni sahihi lazima italeta jibu sahihi. Hata katika somo la hesabu ,ukitumia kanuni sahihi lazima itakuletea majibu sahihi. Ukiwa na maarifa sahihi kwenye kile unachofanya, ukayatumia maarifa hayo lazima yatakuletea matokeo mazuri. Aliyekuwa kocha wa mpira wa kikapu John Wooden …
Continue reading "Usikubali Kile Usichojua Kufanya Kiingilie Hiki"
Vunja Laana Ulizobeba Kwenye Kipato
Linapokuja suala la fedha na utajiri watu wengi wamevurugwa na laana. Wanaamini kuwa hawezi kwenda hatua ya ziada, kama wazazi wao walifikia kiwango fulani basi nao hawezi kufikia. Watu wanaona ni vibaya kama wao watakua na kipato kikubwa kuliko wazazi wao. Unatakiwa kuvunja laana hii na kujiambia kuwa nitakuwa na kipato kikubwa kuliko wazazi wangu, …
Bidhaa Pekee Ambayo Hupaswi Kuiuza Kwenye Biashara Yako
Biashara ni watu, watu ndiyo wanaleta mzunguko mkubwa wa biashara. Watu wakiwa wengi watapelekea mauzo kuwa makubwa endapo watanunua. Katika kipindi hiki wako watu wengi sana wanapoteza wateja wateja wao. Wengine wameshafunga biashara wengine wanaendelea kupambana na hali ilyoko. Ni bora kuendelea kupambana hata kama huoni wateja kuliko kufunga biashara maana unapofunga ndiyo unawapoteza kabisa …
Continue reading "Bidhaa Pekee Ambayo Hupaswi Kuiuza Kwenye Biashara Yako"
Jinsi Ya Kununua Vitu Kwa Bei Rahisi
Fedha ni mfalme kwani karibu kila kitu katika maisha yetu kina dai fedha.Hatuwezi kuishi vile tunavyotaka kama hatuna keshi . Hatuwezi kwenda sokoni kununua kitu kwa maneno, ukienda sokoni unapaswa uwe na keshi mkononi ndiyo uweze kununua kile unachotaka. Katika hali ya kawaida huwa unakuta kitu kinauzwa kwa bei rahisi sana na cha kushangaza unajikuta …
Ningejua Ningefanya Hivi Au Vile
Siku zote majuto hayawezi kubadilisha matokeo ya aina yoyote ile kwenye maisha yetu. Ningejua ningefanya hivi au vile ni maneno ambayo hayana msaada tena katika maisha yako. Kama jambo limeshatokea huna udhibiti nalo tena bali unatakiwa kujifunza kadiri ya majuto hayo uliyoyapata. Majuto ni mwalimu mzuri sana kwani anatufundisha ili siku nyingine tuwe makini kwa …
Siku Zote Kuwa Mkweli Hususani Kwa Mtu Huyu
Ni rahisi kujidanganya wewe mwenyewe na hata kuwadanganya watu wengine. Lakini kuna watu hawajui uongo bali wao wanaamini kuwa kila unachowaambia ni ukweli tu. Ndiyo maana kundi hilo ukiwaambia kitu cha uongo wataendelea kuamini mpaka wanakua na mtu akija kuwaambia hawatamwamini. Watu hao ni watoto wadogo. Siku zote kuwa mkweli hususani kwa watoto wadogo. Siku …
Continue reading "Siku Zote Kuwa Mkweli Hususani Kwa Mtu Huyu"
Huwezi Kufanya Kazi Na Watu Bila Kuwa Na Kitu Hiki
Unaweza kufanya kazi na vitu kama vile kukata kuni, kutengeneza chuma, kulima na vingine vingi tu vinavyohusiana na hivyo bila upendo. Lakini huwezi kufanya kazi na binadamu bila kuwa na upendo.Ukitaka kufanya kazi na watu lazima uwe na upendo na kama unavyojua sisi binadamu ni viumbe vya hisia. Huwa tunajihisi vizuri pale tunapoona watu wanatujali …
Continue reading "Huwezi Kufanya Kazi Na Watu Bila Kuwa Na Kitu Hiki"