Ili tupate matokeo mazuri kwenye chochote kile tunachofanya lazima kwanza tuwe na maandalizi. Angalia kile unachofanya kinahitaji mahitaji gani ya msingi kabla hujaanza kile unachofanya. Kwa mfano, kama wewe ni daktari kabla hujamfanyia mgonjwa upasuaji unatakiwa kuwa na orodha ya vitu vya msingi vya kufanyia upasuaji kabla hujaanza zoezi la upasuaji. Haipendezi umeanza kazi, mara …
Huwezi Kutafuta Amani Kwa Kuepuka Maisha
Tunaishi kwa sababu tuna amani. Unasoma hapa kwa sababu una amani kama ungekuwa kwenye vita usingeweza kupata hata muda wa kujifunza. Kwa sasa watu wanakosa uhuru wa kufanya biashara, kazi na hata uhuru wa kuabudu kwa sababu hakuna amani. Hofu ya ugonjwa wa Corona imechukua nafasi ya amani. Tusipokuwa na amani ndani yetu hatuwezi kuifanya …
Jinsi Ya Kuepuka Kifo, Maafa Na Hatari Nyingine
Yako mambo mengi katika maisha yetu ambayo tunaweza kuyaepuka kwa kuwa tu waangalifu.Mwandishi mmoja aliwahi kusema, kuishi muda ni kuwa mwangalifu maana usipokuwa mwangalifu utaiacha dunia mapema. Wako watu wengi wanatapeliwa kwa sababu ya kukosa kuwa waangalifu. Kukosa uangalifu katika maisha yako ni rahisi sana kukaribisha kifo, maafa na hatari nyingine. Angalia hasara nyingi wanazopata …
Continue reading "Jinsi Ya Kuepuka Kifo, Maafa Na Hatari Nyingine"
Huyu Ndiye Mama Wa Bahati Yako
Kila mtu ana bahati yake hapa duniani. Na ukweli ni kwamba licha ya juhudi tunazoweka lakini katika mafanikio yetu bahati nayo inahusika. Miguel de Cervantes aliwahi kunukuliwa akisema, bidii ni mama wa bahati nzuri. Hakuna mtu ambaye ameweka kazi katika kile anachokifanya halafu akabaki kama alivyo. Bidii huwa haimwangushi mtu yoyote yule. Juhudi unazoweka huwa …
Je Unavumilia Hali Hii Hapa?
Tunaalikwa kuwa wavumilivu katika maisha yetu. Lakini siyo kila kitu ni cha kuvumilia kwanini kila kitu siyo cha kuvumilia? Katika maisha ya binadamu kuna mambo ya aina mbili;Moja; haya ni yale mambo ambayo yako ndani ya uwezo wetu.Mbili; haya ni yale mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu Sasa kama jambo lipo ndani ya uwezo …
Je Una Maadui? Kama Huna Maana Yake Umekosa Hiki
Duniani hakuna malaika bali kuna binadamu ambao asili ya binadamu ni kukosea. Hakuna mtu ambaye mwenye akili timamu atatoka hapo alipo na kwenda kumpiga teke mbwa aliyekufa. Ukiona huna maadui maana yake huna unachofanya ni sawa na mbwa aliyekufa hakuna mtu atakayeangaika naye. Je ulishawahi kuona watoto wanakwenda kuhangaika na mti ambao hauna matunda? Mti …
Continue reading "Je Una Maadui? Kama Huna Maana Yake Umekosa Hiki"
Je Umesikia Hiki?
Ni kawaida katika jamii yetu tunayoishi kukutana na mengi kwa sababu panapokuwa na wengi pia pana mengi. Iko tabia moja ambayo hata wewe umeshawahi kuisikia, mtu anakuja kwako anakuambia umesikia kitu fulani? Dalili ya mtu mwenye umbea na ambaye hana uhakika na kile anachosema ni ataanza na nimesikia moja mbili tatu. Unakuta mtu hana uhakika …
Mshukuru Mungu Hata Kwa Kuwa Na Zawadi Hii
Tunavyo vitu vingi sana vya kushukuru, karibu kila kitu tulichonacho hatuna budi kushukuru na nikisema nivitaje itakua ni litania(orodha)ndefu sana. Kila binadamu amepewa uwezo wa akili, wa kutambua zuri na baya. Utashi huu tuliopewa ndiyo unatufanya sisi kuwa viumbe bora kuliko wengine. Leo kupitia makala hii, tunakwenda kujifunza zawadi ambayo tunapaswa kushukuru kwa kuwa nayo …
Continue reading "Mshukuru Mungu Hata Kwa Kuwa Na Zawadi Hii"
Nyote Njema Huonekana Hata Jioni
Siyo kila siku nyota njema itaonekana asubuhi tu. Mambo yanabadilika sana kiufupi siyo rahisi kutabiri kila kitu na kikatokea sawa. Hakuna mtabiri wa uhakika katika haya maisha kwani yale tunayotabiri ni kama kubashiri tu lakini kuamua matokeo gani ya utabiri ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako. Wakati mwingine unaanza siku yako vizuri, huku …
Bila Nidhamu Hizi Huwezi Kuthubutu
Kinachotufanya tusipige hatua kubwa ni nidhamu tu.Wanaofanikiwa ni wale ambao wana nidhamu kwenye kile wanachofanya. Unatakiwa kuwa na nidhamu ya kazi, fanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu na zalisha ubora.Toa thamani kubwa na jua kuwa kazi ndiyo rafiki wa kweli ambaye hatoweza kukuangusha pale unapokuwa na shida.Watu ni rahisi kukuangusha lakini kazi haiwezi …