Jinsi Ya Kuwa Na Maisha Tulivu

Katika jamii yetu ya sasa iko njia nzuri sana ya wewe kuwa na maisha ya utulivu, huna haja ya kujisumbua na watu wakati kiasili tayari maisha yanakusumbua halafu tena mtu aje akusumbue, utahangaika na vingapi? Watu wamekuwa ni watu wa kukimbizana na mambo ambacho yako nje ya uwezo wao wakifikiri watayaweza. Wako ambao wanakazana kutaka …

Jinsi Ya Kuiba Maarifa Ya Wengine

Hakuna mtu anayeweza kukupeleka mahakamani kwa sababu umetumia maarifa yake aliyoyaandika katika kitabu na ukafanikiwa. Kwa mfano wewe rafiki yangu, unasoma mtandao huu kila siku sasa haya maarifa unayopata yakakusaidia kufanikiwa kwenye eneo fulani la maisha yako unafikiri Mimi nitakuja kukushitaki? Lengo kubwa la Mimi kuandika ni kutaka wewe ufanikiwe kwa kile ninachokijua ninakushirikisha na …

Jinsi Ya Kuwa Na Hamasa Ya Kudumu

Siku zote hamasa za watu kwenye kile wanachofanya huwa hazidumu, siku ya kwanza kuanza kufanya kile unachofanya ulikuwa na hamasa ya ajabu yaani kama ni mzuka ulikuwa nao sana. Sasa unaweza kujiuliza iweje leo Mwl. Deogratius Kessy anataka kuniambia kuna hamasa ya kudumu?Hamasa hazidumu ila ukitaka iweze kudumu iko njia moja ambayo unapaswa kuifanyia kazi. …

Hivi Ndivyo Unavyopaswa Kuwa Mwezi Huu Wa Juni

Vipi kama mwezi huu ukiamua kuishi kinyume na miezi mingine? Miezi yote iliyopita umeishi kimazoea halafu ukiangalia tokea Januari mpaka sasa Juni hakuna kikubwa ulichofanya na kujivunia haya ndiyo matunda yangu ya mwezi Januari mpaka Juni. Kila siku uko bize, unafanya kila kitu, unawahi kuamka na kuchelewa kulala. Badilisha mtazamo wa maisha yako badala ya …

Jinsi Ya Kujifunza Unyenyekevu

Asili huwa ina kawaida ya kuwanyang'anya wale wote ambao wana majivuno kwenye kile wanachofanya. Majivuno yanatuharibia vitu vingi sana kwenye maisha yetu ya kila siku.Tunapoteza vile tulivyokuwa navyo kwa sababu ya kukosa unyenyekevu. Tunajiona kuwa sisi ndiyo kila kitu kwa kila kitu na wengine hawana maana kwetu. Ili tuweze kuwa na maisha ya unyenyekevu ambayo …

Usitumie Tu Fedha Kwa Sababu Una Fedha

Wengi wanajikuta wanatumia fedha kwa sababu wana fedha. Hawa ni wale ambao hawawezi kujizuia au kusema hapana pale wanapokutana na kitu halafu wana hela ya kununua. Kama hakuna ulazima sana wa kitu unachotaka kufanya siyo lazima kutumia fedha linda fedha yako. Usiwe wakala wa fedha zako mwenyewe yaani wewe unakua ni mpokeaji tu baada ya …

Fanya Kinachowezekana Halafu Kisichowezekana Mwachie Huyu

Fanya mambo ya kawaida yaani yale ambayo yako ndani ya uwezo wako halafu mambo makubwa ambayo yako nje ya uwezo wako mwachie Mungu atafanya. Huwa tunajisumbua kupambana na kila kitu, ndiyo maana tunajikuta tuna kazi sana. Kwa mfano, tukimchukulia Musa kwenye kitabu cha Biblia yeye alikuwa na fimbo tu ya kawaida iliyokuwa mkononi mwake alifanya …

Kama Unaishi Kwenye Karne Ya 21 Usiache Kujifunza Kitu Hiki Hapa

Kuna kitu ambacho watu wengi wanapuuzia bila kujua ni kitu muhimu kwa kila mtu. Kama uko hai na unaishi kwenye karne 21 basi unapaswa kujifunza kitu hiki kimoja ambacho tunakwenda kujifunza leo. Unatakiwa ujifunze kuuza. Jifunze namna ya kuuza kwenye kile unachofanya kwa mfano, kama wewe ni mwalimu jifunze kuuza ualimu wako, kama wewe daktari …

Haziwezi Kukusaidia Kamwe

Ni rahisi kuwadanganya watu kwa maneno lakini matokeo na matendo yanakuumbua. Tumekuwa ni watu tunaofanya kazi kwa mdomo na kujielezea sana kile tunachofanya badala ya kuweka kazi na kazi zetu zitutangaze. Nikuambie ukweli rafiki yangu, sababu hazitoweza kukusaidia hata siku moja. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa kwenye eneo lolote lile la maisha kwa njia ya sababu. …

Hili Ndiyo Eneo Gumu Kwako Kufanikiwa

Watu wanaofanya vizuri kwenye vile wanavyofanya ni wale wanaopenda vile wanavyovifanya. Ni rahisi kufanikiwa kwenye mchezo uliochagua kucheza kama unaupenda mchezo huo. Angalia wanaofanya vizuri kwenye michezo mingi ni wale wanaoupenda huo mchezo na muda wao mwingi wanautumia kujifunza huo mchezo wanaoupenda. Eneo gumu kwako kufanikiwa ni lile eneo unalolichukia. Huwezi kufanikiwa kwenye kile unachokichukia. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started