Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuwa Na Hamasa Ya Kudumu

Siku zote hamasa za watu kwenye kile wanachofanya huwa hazidumu, siku ya kwanza kuanza kufanya kile unachofanya ulikuwa na hamasa ya ajabu yaani kama ni mzuka ulikuwa nao sana.

Sasa unaweza kujiuliza iweje leo Mwl. Deogratius Kessy anataka kuniambia kuna hamasa ya kudumu?
Hamasa hazidumu ila ukitaka iweze kudumu iko njia moja ambayo unapaswa kuifanyia kazi.

Njia hiyo ni kuwa na malengo unayofanyia kazi au kuwa namba unayofanyia kazi. Kwa mfano, Kama wewe ni mfanyabiashara kuwa namba ya kufanyia kazi kila siku, yaani kwa mfano, unakuwa namba ya mauzo unayoifanyia kazi kila siku mpaka uifikie, kile kitendo tu cha kuwa namba ya mauzo unayopaswa kuwa nayo kila siku yanakuhamasisha kupiga hatua zaidi.

Kama vile tunavyokula kila siku na kuogopa kila siku ndivyo hamasa zinavyokuwa unatakiwa ufanye kila siku lakini pia uwe na namba unayopaswa kuifanyia kazi kila siku.

Kama wewe unaandika basi uwe na kiwango cha maneno unayopaswa kuandika kila siku.

Kama wewe ni tabibu, basi jiwekee kiwango fulani cha kuona wagonjwa na kuwahudumia vizuri sana wagonjwa wote wanaopita katika mikono yako.

Kama wewe ni mwalimu panga kufundisha somo bora na kile ulichopanga kufundisha kadiri ya andalio lako la somo.

Bila kuwa na kitu cha kufanyia kazi, kitu kinachokusukuma kwenye kile unachofanya ni rahisi kuahirisha, kuchoka na kukata tamaa. Ila ukiwa na namba unayoifanyia kazi utajituma mpaka pale utakapoipata namba hiyo.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa na kitu au malengo unayofanyia kazi kila siku yatakufanya uwe na hamasa ya kukusukuma kufanya kila siku, lije jua au mvua wewe unachoangalia ni kufikia lengo ulilojiwekea.

Kwahiyo, usijiwekee malengo madogo, weka malengo makubwa sana kwani ndiyo yanakuhamasisha kuchukua hatua kuliko malengo madogo.

Nakuachia changamoto kwenye eneo la fedha, kipato unachopata sasa kizidishe mara kumi na namba utakayoipata ndiyo unayotakiwa kuifanyia kazi kila siku.
Usilale, amka na pambana kufanyia kazi namba ya kipato chako kwa mwezi, wiki au siku.
Inawezekana kama ukijitoa kweli kwenye kile unachofanya.

Ukihitaji usimamizi wa karibu yaani coaching ili uweze kuwa na hamasa ya kila siku ya kufikia malengo makubwa unayofanyia kazi, karibu sana rafiki yangu tufanye kazi pamoja.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz  

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: