Hakuna mtu anayeweza kukupeleka mahakamani kwa sababu umetumia maarifa yake aliyoyaandika katika kitabu na ukafanikiwa. Kwa mfano wewe rafiki yangu, unasoma mtandao huu kila siku sasa haya maarifa unayopata yakakusaidia kufanikiwa kwenye eneo fulani la maisha yako unafikiri Mimi nitakuja kukushitaki?
Lengo kubwa la Mimi kuandika ni kutaka wewe ufanikiwe kwa kile ninachokijua ninakushirikisha na wewe.
Kwa sababu msingi mkuu wa mafanikio yoyote yale ni kuwasaidia wengine kupata kile wanachotaka na mimi nitapata kile ninachotaka.
Huwezi kufanikiwa kama huwawezeshi wengine kufanikiwa kwanini? Kwa sababu tunategemeana na kile unachotaka tayari kipo kwa watu wengine.
Njia pekee ya kuiba maarifa ya wengine ni kusoma vitabu, dunia ya sasa ina vitabu vingi sana, kwenye eneo la kiroho vitabu vipo vingi hivyo kama unataka kukua kiroho iba maarifa kutoka kwa wale walioandika vitabu kwa kusoma vitabu vyao.
Huwa ninakusihi sana usome vitabu kwa sababu ninajua faida ya vitabu kwani nakiri wazi vimebadilisha maisha yangu. Usikose kusoma kila siku kama vile unavyokula chakula au kuoga kila siku.
Yatumie maarifa ya wengine kwa kuweka kwenye vitendo ili ufanikiwe.
Unajua ni kwanini mwenzako anafanikiwa eneo fulani halafu wewe hufanikiwi? Jibu ni kwamba kuna kitu anachokijua kuliko wewe , ukiona mtu anakuzidi kwenye eneo lolote lile jua kuna kitu anakijua kushinda wewe. Sasa kama ndiyo hivyo ufanyeje? Jawabu, jifunze kutoka kwao, kama wana vitabu basi soma vitabu vyao, kama hawajaandika nenda kawaulize ni kitu gani kinachowafanya wawe hivyo walivyo. Na Kitu chenyewe lazima kitakuwa ni maarifa ambayo yeye anayo wewe huyajui.
Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kubadilisha kitu chochote kile tafuta maarifa kwenye eneo unalotaka. Usiwe tena mtu wa sababu wakati kuna msaada wa maarifa unaoweza kubadili kabisa mtazamo maisha yako.
Jitume kujua kile ambacho hujui kwani ndiyo kinakurudisha nyuma.
Kwahiyo, ukilalamika kwamba hujui kitu fulani ndiyo maana hufanikiwi eneo fulani huo ni uzembe na ujinga mkubwa. Soma vitabu, tumia maarifa unayopata kufanikiwa kwenye kile unachofanya.
Maarifa ndiyo siri inayowafanya wengine wafanikiwe na wengine wasifanikiwe.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo