Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuwa Na Maisha Tulivu

Katika jamii yetu ya sasa iko njia nzuri sana ya wewe kuwa na maisha ya utulivu, huna haja ya kujisumbua na watu wakati kiasili tayari maisha yanakusumbua halafu tena mtu aje akusumbue, utahangaika na vingapi?

Watu wamekuwa ni watu wa kukimbizana na mambo ambacho yako nje ya uwezo wao wakifikiri watayaweza. Wako ambao wanakazana kutaka kumaliza matatizo ya watu, nani aliyekuambia unaweza kumaliza matatizo ya mtu? Matatizo ya mtu yana malizwa na mtu mwenyewe na siyo wewe.

Wajibu wako mkuu ni kufanya kazi yako au fanya kile unachopaswa kufanya kwa kutimiza wajibu wako vizuri utasaidia kuifanya dunia kuwa sehemu salama kuishi kwa kila mmoja wetu lakini kwa kuacha unaongeza shida duniani.

Ukitaka kuwa na maisha tulivu, fanya yafuatayo;

Usiseme kila unachojua. Unajua shida inaanza pale unapoanza kusema kila unachojua na hapa lazima utakosana na watu. Muda mwingine hata kama unajua usitake kuwaonesha watu kuwa unajua, ni bora ukae kimya kufunika kombe mwanaharabu apite. Kuna vitu vingine ukisema utaibua ugomvi ambao hata haukuwepo, muda mwingine ishi tu kile unachokiamini wewe ni sahihi hata kama wengine hawataki kukubaliana na wewe.

Itafikia mahali ukweli utajitetea wenyewe na siyo wewe kutaka kusema kila kitu, kwa mfano kama wewe unayajua mangapi ya siri? Unafikiri hayo unayojua kama ukisema itakuwaje? Kuna mengine ukisema utazua balaa kwa wengine ni bora kutokusema kuliko kusema na kuibua mapya.

Usihukumu kila unachoona, umeona vingapi? Na umehukumu vingapi mpaka sasa? Muda mwingine hata unavyohuku siyo sahihi na pengine unahukumu kwa nje tu lakini kwa ndani hujui vizuri.

Kama unataka uwe na maisha tulivu usipende kuhukumu kila unachoona, vingine viache tu maana utahukumu vitu vingine hata siyo kazi yako kuhukumu. Kazi ya kuhukumu hebu tumwachie Mungu  au mahakama waliopewa dhamana hiyo.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kuwa na maisha tulivu; usihukumu kila unachoona na pili usiseme kila unachojua maana vitu hivi viwili vinaweza kuibua vitu ambavyo huku tegemea vitokee katika hali ya kawaida tu.

Hivyo basi, ukishawajua watu na  misingi ya maisha katika maeneo fulani jifunze kuishi kadiri ya asili inavyotaka na fanya yale ambayo yanakuhusu na yasiyo kuhusu waachie wafanye wengine.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com, kessy@ustoa.or.tz  

Asante Sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: