Fanya Chochote Kile Kama Hivi

Fanya chochote kile kwenye maisha yako kama vile kila tendo lako unalofanya linarekodiwa na kamera na kuna watu wanaangalia vile unavyofanya. Ukichukulia kila tendo unalofanya linarekodiwa , huwezi ukafanya kitu ambacho siyo sahihi. Fikiria kama unarekodiwa na watoto na wajukuu zako wataoneshwa jinsi ulivyokuwa unafanya mambo yako, kila siku na kila mahali. Kama unajua kuna …

Kabla Hujawekeza Fedha Yako Popote, Fanya Hiki Kwanza

Kabla ya kuwekeza fedha yako popote pale, unatakiwa kuwekeza ndani yako kwanza. Wekeza ndani yako kwanza kwa kujifunza sana, kuwa bora kwanza wewe mwenyewe kabla hujataka kuwekeza sehemu yoyote ile. Mtu akishajifunza, akishakuwa bora anaweza kufanya maamuzi sahihi ya wapi pa kuanzia. Kwa mfano, katika fursa, zipo fursa ambazo ni za kweli na zipo ambazo …

Usiamini Vitu Juu Juu

Badala yake vijue kwa undani wake. Kabla hujaingia makubaliano ya kikazi au kibiashara au makubaliano yoyote yale na mtu, ni vema mkawa na makubaliano yaliyoandikwa, vinginevyo mtakuja kuumbuana. Makubaliano yaliyoandikwa yanakuwa yana ulinzi kwa pande zote mbili. Kwa mfano, ukiajiri, hakikisha mnaingia mkataba wa kimaandishi hata siku lolote lile likija kutokea unakuwa salama. Ni muhimu …

Hiki Ndicho Kitakachotokea Pale Usipokazana

Juhudi binafsi ni kitu ambacho kinahusika sana kwenye mafanikio makubwa. Kinachotutofautisha na wengine ni juhudi binafsi. Kwa mfano, kazini mnaweza kufanya wote kazi moja lakini msifanikiwe wote. Wanaofanikiwa kwenye maeneo mengi na kuwaacha wengine wakishangaa ni juhudi binafsi. Juhudi binafsi inasaidia sana katika safari ya mafanikio. Leo shabaha yangu kubwa ni kukuambia kuwa, usipokazana hutatokea …

Hakuna Mpango wa Biashara (Business plan) Wenye Kitu Hiki

Kifupi tu rafiki yangu, unaweza kuwa na mpango wa biashara yaani business plan lakini siyo kwamba ukishakuwa na kitu hiko ndiyo tayari umeshaipatia biashara. HAKUNA business plan yenye hasara. Kila unapokuwa na mpango wa biashara unaona faida tu. Lakini, ukiingia kwenye uhalisia ndiyo utaona kazi yenyewe. Mwanzoni mwa mwaka mpya, watu wengi hupenda kuwa na …

Huyu Ndiye Anayesababisha Matatizo Yako Ya Kifedha Na Jinsi Ya Kupata Suluhisho

Mwandishi na mwendeshaji wa vipindi vya radio na tv Dave Ramsey kwenye kitabu chake cha The Total Money Makeover anasema kwamba matatizo yako ya kifedha yanasababishwa na wewe mwenyewe. Watu huwa wanadhani kwamba matatizo yako ya kifedha huwa yanasababishwa na serikali serikali, uchumi, bosi wako nk. Ukitaka kumjua adui wako wa kifedha, simama mbele ya …

Usikubali Anayekuonea Aendelee Na Uonevu Wake

Usikubali kuwa mtu wa kuonewa na watu kukuchukulia poa au ni kitu tu cha kawaida. Unatakiwa kusimamia utu wako na yeyote anayekuonea mfanye ajifunze kwamba uonevu siyo kitu sahihi. Weka misingi yako na isimamie yeyote anayekuja kwako kwa nia ovu nenda kasimamie misingi yako. Usiposimamia utu wako watu wanakudharau na kukuchukulia poa. Jiamini na kile …

Futa Msamiati Huu Kwenye Akili Yako

Watu wengi wanajiwekea vikwazo bila wao kujua. Vikwazo vya kiakili, kiroho na hata kimwili. Kikwazo cha akili ni kikwazo kibaya sana kwa mtu yeyote yule kuweza kufikia mafanikio makubwa. Akili ikiamini inaweza kufanya makubwa sana lakini kama akili haiamini hata ufanye nini huwezi kufanikiwa kwa chochote kile. Leo naomba uende kufuta msamiati wa haiwezekani katika …

Sala Ambayo Huwa Inajibiwa

Heri ya mwaka mpya rafiki yangu. Najua tayari umeanza mwaka wako 2022 ukiwa na hamasa kubwa ya kwenda kufanya makubwa lakini muda siyo mrefu hamasa hiyo inakwenda kupotea kama vile mshumaa unavyopotea kwenye upepo. Januari 3, tunakwenda kuanza semina yetu ya kuanza mwaka 2022 kiushindi na lengo la semina ni kupata maarifa ambayo yataendelea kuwasha …

Zimebaki Siku 2 Kuanza Semina Ya Kuanza Mwaka 2022, Penda ushindi Na Kuwa Bora Zaidi

Mabilionea wana msukumo mkubwa wa kutaka ushindi ndani yao na kuwa bora zaidi kwenye kile wanachofanya kuliko mtu mwingine yeyote. Wanaiishi kila siku yao kutafuta ushindi mkubwa. Wanajisukuma kuendelea kuwa bora zaidi ya vile walivyo sasa. Rafiki yangu, penda ushindi na kuwa bora zaidi mwaka 2022 kwa kuanza na semina ambayo semina itakufanya upende ushindi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started