Sababu Ambazo Zinapelekea Mtu Kutokufanya Jambo

Sisi binadamu huwa tunafanya au hatufanyi kitu kwa sababu kuu mbili. Ukiona mtu hataki kufanya au hawezi kufanya sababu kuu inakuwa ni uwezo au motisha. Mwingine hataki kufanya jambo kwa sababu hawezi kufanya. Yaani uwezo wake ndiyo unamfanya afanye vizuri au la. Wengine wana uwezo wa kufanya lakini hawataki tu kufanya kwa sababu hawana motisha. …

Somo Muhimu Unalopaswa Kuwafundisha Watoto Wako

Mzazi ndiye mwalimu wa kwanza katika familia na malezi kwa ujumla. Lakini baadhi ya wazazi huwa wanaamini kwamba walimu mashuleni ndiyo wana jukumu hilo la kuwafundisha watoto. Kitu ambacho napenda kukujulisha wewe kama mzazi, mlezi au mzazi mtarajiwa ni kwamba wafundishe watoto wako somo muhimu la kutotoa siri za familia yako. Kwanini nasema hivyo? Wako …

Jinsi Ya Kusafisha Maisha Yako

Angalia kila hali unayopitia kwenye maisha yako hata kama ni ndogo kiasi gani. Je, unafanya kila unachoweza kufanya? Je, umeweza kutumia kila fursa inayokuzunguka? Je, unayatumia vizuri maarifa unayopata kwa vitendo? Unaweka juhudi za kutosha kwenye kazi yako? Je, umepatana na wale ambao mmepishana yaani mmesameheana? Je, una mjali mke au mume wako? Je, unaijali …

Samaki Huwa Anaanza Kuozea Kichwani

Ukiona familia yako haiendi wewe kama baba au mama jua shida ndiyo iko kwako kwa sababu, samaki huwa anaanza kuozea kichwani. Samaki huwa anaanza kuozea kichwani hii maana yake nini? Tatizo huwa linaanza kwenye wale watu wenye mamlaka makubwa kwenye eneo husika. Biashara inaanza kufa kwa sababu mmliki tayari alishakufa, wewe kama ndiyo kichwa cha …

Ni Afadhali Nikose Fedha Lakini Siyo Hiki Hapa

Jumamosi ya wiki ya jana nilikuwa sokoni na rafiki yangu. Siku hiyo ilikuwa imenyesha mvu kubwa kweli hata wale wafanyabiashara waliokuwa wanatoa huduma mbalimbali walishindwa kupata wateja kwa sababu ya mvua. Kuna hitaji moja ambalo rafiki yangu alikuwa anaenda kulipata hapo sokoni. Kabla hatujafika eneo ambalo anapaswa kupata huduma, tutakutana na muuzaji ambaye angempatia huduma …

ZAWADI YA KUMNUNULIA YULE UMPENDAYE KWENYE SIKU YA VALENTINE.

Je, unataka kumpatia zawadi mtu wako wa karibu leo kwenye kilele cha siku ya wapendao duniani? Kama jibu lako ni ndiyo, basi zawadi sahihi ya kunogesha mahusiano yako ni kumnunulia yule umpendaye kitabu. Pata zawadi ya kitabu hiki kwa shilingi elfu 15 leo kwa bei ya ofa. Acha wajue kwamba unampenda, waoneshe watu wako wa …

Kwenye Biashara Zingatia Vitu Hivi Viwili, Kama Biashara Haina Vitu Hivi, Ni Bora Uifunge

Mwandishi mmoja wa riwaya Ayn Rand anasema kwamba, siku ukishindwa kumfukuza msaidizi wako wa kazi kwenye biashara yako, hiyo biashara bora ufunge. Kwa kuwa maisha ni biashara, kama maisha unayoishi au kile unachofanya hakikulipi ni bora kuacha hicho unachofanya. Dunia ina utele huwezi kukosa kitu kinachokulipa kama unatoa thamani kubwa. Wako watu wanateseka kwenye mahusiano …

Imebaki Siku Moja Tu Ili Tuhitimishe Kilele Cha Mwezi Wa Mapenzi Mubashara.

Imebaki Siku Moja Tu Ili Tuhitimishe Kilele Cha Mwezi Wa Mapenzi Mubashara. Soma kwanza kisa cha hadithi hapo chini, kisha chukua hatua ya kujali mahusiano yako kwa kusoma kitabu cha Ijue Njaa Ya Wanandoa. "Mwaka wa kwanza wa ndoa mume anaongea mke anasikiliza. Mwaka wa pili mke anaongea mume anasikiliza. Mwaka tatu mume na mke …

Kwenye Maisha Kuna Vitu Hivi Vitatu, Lazima Uchague Viwili Ili Maisha Yaende

Kwenye maisha kuna vitu vitatu navyo ni;Moja, kazi.Mbili, familia naTatu, Bata( starehe). Ili maisha yako yaende vizuri lazima ukubali kuchagua vitu viwili tu utakavyoweza kutembea navyo kwenye maisha yako. Usipofanya hivyo ni rahisi kuyumba. Huwezi kufanya yote kwa wakati mmoja lazima uchague viwili ili maisha yako yaweze kwenda. Kwa mfano, ukichagua familia na kazi lazima …

Design a site like this with WordPress.com
Get started