Kuwa Mwendesha Farasi Usiwe Farasi

Watu wengi wanachagua kuendeshwa na farasi badala ya wao kumwendesha farasi. Unaweza kujiuliza je farasi na mwendesha farasi ni akina nani? Farasi ni hisia na mwendesha farasi ndiyo akili. Kumbe basi,  unatakiwa kuendeshwa na akili na siyo hisia. Hatua ya kuchukua leo; tumia akili na usikubali hisia ikuongoze. Kuwa mwendesha farasi na usiwe farasi. Usiendeshwe …

Kama Hasara Haikuhusu, Hupaswi Kunufaika Na Faida

Tumeshazoea kuona katika mahusiano na makubaliano mengi baina ya watu yapo kwenye hali kwamba inapopatikana faida basi pande zote zinanufaika na kufurahia. Lakini, inapopatikana hasara, upande mmoja unakuwa hauhusiki kabisa na hasara hiyo. Kama unanufaika na faida na hasara pia inakuhusu. Linapotokea jambo ambalo linaleta hasara unapaswa kuwajibika kama ulivyokuwa unawajibika kwenye faida. Unapaswa kujua …

Ukitaka Uhuru Mkubwa Unapaswa Kulipa Gharama Kubwa

Je, unataka uhuru? Rafiki yangu nikupendaye, kila aina ya uhuru unaotafuta kwenye maisha yako, ipo gharama ambayo utapaswa kulipa ili kupata uhuru huo. Kifupi tu, hakuna uhuru wa bure, na kadiri unavyotaka uhuru mkubwa , ndiyo unahitajika kulipa gharama kubwa. Uhuru ni kitu kigumu sana kukifikia na watu wengi hawaielewi dhana hii ya uhuru. Kwa …

Hii Ndiyo Hamu Unayopaswa Kuwa Nayo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa

Je, una hamu kiasi gani ya kufikia ndoto yako? Hamu kubwa  unayokuwa  nayo  kwenye  kitu  unachotaka  ndio  inapima  kama  utaweza kukipata. Kama  una  hamu  kubwa  sana  ya  kupata  kitu,  hakuna  kitu  kitakachoweza  kukuzuia kukipata.  Hata  utapokutana  na  changamoto  lazima  utapata  njia. Hamu kubwa  ya  kupata  kitu  inakupa  nguvu  ya  kulipa  gharama  ya  mafanikio. Unaweza  kujitengenezea  …

Unahitaji Fedha Zaidi

Matatizo mengi katika jamii yetu ukiyatazama mengi yanasababishwa na tatizo la fedha. Na matatizo mengi tuliyokuwa nayo siyo kwamba ni matatizo bali ni kukosa fedha ya kutatua matatizo tuliyonayo. Kama tatizo lako ulilokuwa nalo ukipata fedha linaisha basi hapo wewe huna tatizo bali tatizo lako ni fedha. Umasikini ni mbaya, pambana kufanya kazi ili kuondoa …

Vunja Utamaduni Wa Hovyo

Kwa utamaduni wa kiafrika ambao tunao, ni vigumu sana mtu kufanikiwa kwa sababu watu wengi wanafanya kazi kimazoea. Huwezi kufanikiwa kwenye kitu chochote kile kama hujaondoa utamaduni wa kiafrika ambao tunao. Utamaduni wa kiafrika hauchochei maendeleo bali unadumaza maendeleo. Pata picha kwenye jamii yako wewe unavyokuwa wa tofauti na jamii inavyokusema. Kwa mfano, jamii zetu …

Naomba Uniombee Ili Niache Hiki Hapa

Kiasili binadamu ni wavivu. Watu wengi wamekuwa hawataki kufanya kitu wanachopaswa kufanya kwa sababu ya uvivu uzembe na ujinga halafu wanaomba uwaombee ili wakae kwenye mchango. Mtu anakua anashindwa kutimiza wajibu wake anamsingizia shetani hivyo anaomba umuombee aache hiyo tabia. Yaani mambo binafsi ambayo yanahitaji nidhamu ya kuamua na kufanya mtu anataka aombewe. Tumpunguzie Mungu …

Kukubali Kwa Nje Tu

Watu huwa wanafanya kitu kama wamekubali wao wenyewe kutoka ndani ya mioyo yao. Unaweza ukawahamasisha kadiri uwezavyo na ukakubaliana nao kabisa kwamba watafanya lakini wanakuja kufanya kinyume. Ukiona mmekubaliana na mtu kufanya kitu halafu hafanyi jua alikukubalia kwa nje tu ili kukufurahisha kwa nje. Lakini ile ndiyo kutoka ndani yake haiko. Anaona ni bora akuridhishe …

Jinsi Ya Kujua Thamani Ya Utajiri Wako

Katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa ya ubilionea ni muhimu sana ujijue mpaka sasa una utajiri wa kiasi gani. Kuishi bila kujua una utajiri wa kiasi gani unakuwa kama vile mtu uko gizani. Umeshasikia tajiri fulani, utajiri wake ni kiasi gani, na wewe pia unapaswa kujua. Jinsi ya kujua utajiri wako halisi, CHUKUA THAMANI YA …

Design a site like this with WordPress.com
Get started