Ila Wanapuuza Tu

Watu wanajua kile wanachopaswa kufanya ila wanapuuza tu ukweli na kujifanya kama vile hawajui. Ni nani asiyejua kuishi maisha yasiyokuwa na maadili ni kitu ambacho siyo sahihi kwa jamii? Watu wanajua wanapaswa kufanya kazi lakini ni wachache wanaofanya kazi na kupata mafanikio. Watu wanajua wanapaswa kuweka akiba kile wanachopata na kukiwekeza lakini ni wangapi wanafanya …

Njia Rahisi Sana Ya Kutokupoteza Muda Wako

Ni kujua thamani ya muda wako. Pata picha kama unajua thamani ya muda wako kwa saa moja ni million moja utalipoteza kwenye mambo ya kijinga? Unatakiwa kukokotoa thamani ya muda wako na kuona muda wako ni fedha na pale unapotumia kwenye mambo ambayo siyo sahihi jisikie vibaya kutumia fedha zako kwa mambo yasiyokuwa muhimu kwako. …

Usijali Wengine Wanakuchukuliaje

Huwa tunajali sana wengine wanatuchukuliaje, ndiyo maana mambo mengi sana tunayofanya ni kuwaridhisha watu na kujionesha kwa wengine. Ikiwa utaweza kuishi maisha yako na kutokujali wengine wanakuchululiaje basi utaweza kuishi maisha bora na uhuru wa kufanya kile unachotaka. Wewe ndiyo mkurugenzi wa maisha yako, unaelewa unatoka wapi, ulipo na kule unakotaka kufika. Hivyo basi, usiogope …

Ukifanya Kazi Matokeo Yaonekane

Kama unafanya kazi, basi matokeo yataonekana kama kweli unafanya kazi wala hayawezi kudanganya. Na kama hufanyi kazi matokeo yataonekana. Kama unafanya kazi halafu matokeo hayaonekani basi jua kuna mahali unakosea. Unatakiwa ukae chini ujitafakari ni wapi unakosea ili basi matokeo yaonekane. Unapofanya kazi, lazima maisha yako yabadilike. Kazi ni rafiki mzuri kwako. Kama huoni matokeo …

Tegemea Kupata Kitu Hiki Kutoka Kwa Mtoto Wako

Watoto wanakupa kile ambacho wewe mzazi unawapa watoto. Kama unawapa upendo basi watoto watakurudishia upendo. Baadhi ya wazazi wanalalamika kuwa watoto hawawajali pale wanapokuwa wakubwa. Kama mzazi hukumjali mtoto wako akiwa mdogo unategemea na yeye akujali ukiwa umezeeka? Kumbuka unavuna kile ulichopanda, usitegemee kuvuna kitu ambacho hujakipanda kutoka kwa mtoto. Kwa mfano, kama mzazi hujawafundisha …

Sababu Mbili Za Mafanikio

Kuna sababu mbili za kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Ukiweza kuzifuata lazima utafanikiwa ni suala la muda tu. Sababu ya kwanza, jua gharama ya mafanikio unayotaka.Kama unataka kufanikiwa kitu jua ni gharama kiasi gani unayopaswa kulipa. Sababu ya pili, kuwa tayari kulipia gharama. Baada ya kujua gharama sasa kuwa tayari kulipia gharama hizo. Kila …

Unatakiwa Kufanya Hivi Kama Kitu Hakipo Sawa

Wakati  mzuri wa  kubadili  mambo  yaliyoharibika  ni kabla  hayajaharibika,  na  unaweza kufanya  hivyo  kwa  kuchukua  hatua  kwenye  mambo  madogo  ambayo  hayana  madhara na  yanaweza  kupuuzwa,  lakini  baadaye  yanatengeneza  madhara  makubwa. Kwa mfano, huwa tunadharau yale mambo madogo madogo kwenye maisha yetu, lakini baadaye yanakuja kutugharimu. Kama  kitu  hakipo  sahihi,  kirekebishe  kabla  mambo  hayajaharibika. Muda mzuri …

Mafanikio Siyo Kushinda Mara Zote

Somo kubwa ambalo unapaswa kulielewa wakati wote kwenye maisha ni kwamba, mafanikio Siyo kushinda mara zote. Bali matokeo ya USHINDI mkubwa kwenye mambo machache. Unapokuwa unakabiliana na changamoto kwenye kazi, biashara, uwekezaji nk na kushindwa vibaya, siyo kwamba hutafanikiwa bali utafanikiwa. Unachotakiwa kufanya ni wewe kushinda kwenye maeneo machache ambayo uko vizuri na kufidia kwingine. …

Unachopaswa Kujua Ni Hiki

Mtu mmoja aliwahi kunukuliwa akisema, nataka kujua ni wapi nikienda nitakufa, niepuke kwenda sehemu hiyo. Hii ina maana gani kwetu? Hii ina maana kwamba, unatakiwa kujua ni vitu gani ukivifanya vitakupa hasara na uviepuke kuvifanya vitu hivyo. Unatakiwa kujua ni uwekezaji gani ukifanya utakupa faida na uwekezaji gani ukifanya utakupa hasara na uepuke hasara hiyo. …

Maana Ya Kutosheka

Kutosheka haimaanishi kidogo kama wengi wanavyofikiri. Kutosheka ni kufikia hatua ambayo unajua hata ukienda zaidi hakuna mabadiliko makubwa utakayoleta na kwa kuwa kila hatua unayochukua ina hatari hivyo hakuna hatari itakayoweza kukulipa. Kwa mfano, mtu ukishiba maana yake umetosheka na hata ukisema ule zaidi inakuwa ni hatari na sumu. Wengi wakisikia kutosheka wanaona ni kama …

Design a site like this with WordPress.com
Get started