Design a site like this with WordPress.com
Get started

Wafahamu Watu Wanaofanya Mambo Makubwa Duniani

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na umeianza siku yako kwa hamasa ya hali ya juu kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako ya leo. Leo ni siku bora sana kwetu hivyo basi, tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya leo kwa  kuweza kutustahilisha  tena kuvuta pumzi siku hii ya leo.

Mpendwa rafiki, tumia muda wako vizuri jali sana muda wako usikubali mtu akupotezee muda kwa mambo hasi. Napenda kutumia nafasi hii kukukaribisha tena katika kipindi chetu cha leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Image result for WHEN GOD TAKE AN ORDINARY PEOPLE TO BE AN EXTRAORDINARY PEOPLE

Mpendwa rafiki, Mungu alipokuwa anahitaji mfalme wa Israeli hakuchagua Yule mtu ambaye tayari ana ujuzi au ana wadhifa Fulani bali bali alimchagua mtu wa kawaida ambaye hata familia yake walimuona ni mtoto ambaye hastahili. Mungu alimchagua Daudi mtu wa kawaida na kumfanya mtu mkubwa (ordinary people to be  an extraordinary people) kuwa kiongozi wa Israeli.

Mpendwa rafiki, mara nyingi katika jamii yetu tumezoea kuona wale wanaofanya mambo makubwa katika jamii ni wale watu wenye nyadhifa Fulani, watu wanaotokea katika familia bora nakadhalika. Kwahiyo, ikitokea jamii wakiona mtu asiyekuwa na cheo Fulani anafanya makubwa watu wanaanza kujiuliza maswali ya kwanini na iweje mtu huyu afanye mambo kama haya.

SOMA; Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Lead To The Field

Mpendwa rafiki, napenda kukutia moyo katika maisha yako,usikate tamaa Mungu atakuinua na kukufanya mtu wa watu na bora kama ilivyoonekana kwa Daudi. Huenda kuna watu wanakudharau na kukuona hustahili kufanya hicho unachofanya sasa lakini usikubali kukatishwa tamaa wewe moto wako uwe ni kuongoza bila kujali cheo au wadhifa ulionao na utafanya makubwa.

Watu wengi duniani waliofanya makubwa ni wale ambao walionekana ni watu wa kawaida sana, wengi  wanahukumu watu kwa kuwaangalia kwa nje kulingana na sehemu aliyotoka, familia aliyotokea,wadhifa au cheo Fulani.  Wale wanaonekana hawafanyi vizuri darasani ndiyo wanakuja kuwa watu wakubwa na kuwaacha watu midomo wazi. Usijali watu wataongea nini bali sikiliza sauti yako ya ndani.

siku moja,nilikuwa mahali Fulani ndugu mmoja alikuwa anasoma moja ya maandiko yangu nami niko karibu naye bila kujua mimi ndiye mwandishi wa kile anachosoma.  Alivyokuwa amemaliza kusoma akauliza hivi huyu Deo Kessy ndiyo nani? Nikamjibu kwa tabasamu Deo Kessy Ndiye mimi. Aliishiwa maneno ya kusema. Kwahiyo, rafiki watu wengine wameshajiwekea akilini mwao kuwa watu wanaofanya kitu Fulani ni watu wenye vyeo Fulani.

Hatua ya kuchukua leo, jikubali vile ulivyo na endelea kufanya mambo makubwa bila kujali cheo,elimu, wadhifa Fulani, sikiliza sauti yako ya ndani na tambua Mungu amekuita wapi, na itika kubali kutumika atakuinua kama alivyomwinua Daudi na kuwaacha watu midomo wazi. Inawezekana kwa yeyote anayeamua. Kumbuka wewe ni bora rafiki na ulizaliwa mshindi.

SOMA; Moto Wa Hamasa Utakaokuwezesha Kupata Nafasi Ya Kazi Sehemu Yoyote Duniani

Mpendwa msomaji, fanya kile unachofanya kwa moyo kitakuja kukuinua siku moja, usijali hata kama sasa watu hawakuheshimu  watakuja kukuheshimu tu, kikumbwa kama uko hai ndoto yako haiwezi kufa. Endelea kuwashangaza watu, endelea kuishangaza dunia kwa kufanya mambo tofauti katika jamii.

Nakutakia utekelezaji mwema katika haya ulijifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: