Jinsi Ya Kuwa Na Mchango Kwenye Jamii

Maisha yenye maana ni yale ambayo yana mchango kwa wengine. Je, maisha yako yana mchango kwa wengine?Ili maisha yawe na mchango kwa wengine unapaswa kufanyanini? Kwa kufanya kitu chenye manufaa kwa watu wengi iwezekanavyo tunaweza kuwa na michango kwenye jamii. Kila unachofanya kinapaswa kuwa na manufaa siyo tu kwa watu wengi hata kwa watu wachache …

Unajionaje Ukiwa Sehemu Hii

Kila mmoja wetu ana picha kubwa ndani yake ambayo anaiona. Picha hii ina nguvu sana kutusaidia sisi wote kuweza kutimiza malengo yetu. Kuna wakati unajiona kabisa unaweza kufanya kitu fulani na kuna wakati unajiona kabisa huwezi kufanya kitu fulani. Picha ina nguvu, ndiyo inayoendesha maajabu mengi na makubwa ambayo watu wanafanya. Je, wewe binafsi unajionaje …

Wasaidie Watu Kupitia Kitu Hiki

Rafiki yangu nikupendaye,Kama unataka ufanikiwe zaidi kwenye chochote kile, wasaidie wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapa kile unachotaka. Sasa basi, unachotakiwa kufanya ni wewe kuweza kusaidia watu kupitia MAUZO. Kwa sababu ni kupitia MAUZO ndiyo wewe utaweza kupata chochote kile unachotaka. Kwa sababu kila mmoja wetu ni muuzaji, mpaka hapo ulipo, upo kwa sababu …

Usikubali Watu Wakushinde Kwenye Vitu Hivi Viwili

Kwenye maisha watu wanatushinda katika mengi. Watu wanatushinda kiuzuri, wanatushinda kimwonekano, wanatushinda kipato, mali na vingi wanavyomiliki nk. Unaweza kukubali watu wakushinde kwenye vitu vyote lakini usikubali wakushinde kwenye vitu hivi. Moja, kazi. Usikubali mtu akushinde katika kufanya kazi. Jitahidi kufanya kazi kuliko watu wengine. Kwa sababu kazi ndiyo rafiki wa kweli ambaye anaweza kukupa …

Achana Na Watu Wote, Shirikiana Na Huyu

Mwanafalsafa Seneca, kwenye moja ya barua zake, aliwahi kushauri yafuatayo;Seneca anashauri tuchague kushirikiana na watu ambao wanatusukuma kuwa bora zaidi ya tulivyo sasa.Watu ambao wana ushawishi mzuri kwetu wa kutuboresha zaidi ya vile tulivyo siyo kuchukua watu ambao hata hawakusukumi zaidi ya kukurudisha nyuma. Katika kufanya hivyo tunapaswa kuchunguza imani, mitazamo, fikra na tabia za …

Bidhaa Yenye Soko Sana

Kama unataka kufanikiwa na kufanya vizuri kwenye kile unachofanya basi kuwa na bidhaa yenye ubora. Ubora ndiyo bidhaa yenye soko sana, ukiwa na ubora lazima watu watataka sana kile unachouza. Kwa chochote kile unachofanya, hakikisha unafanya kwa ubora.Kama bidhaa yako ina ubora, mauzo kwako siyo kitu cha kukusumbua. Tengeneza bidhaa yenye ubora kiasi kwamba unateka …

Kuwa Mkweli Kwako Mwenyewe

Kama kitu unaweza kufanya, fanya na kitu huwezi sema ukweli, huwezi. Kwa mfano, mtu anakuja kwako ana shida ya kitu fulani, na wewe huwezi kumsaidia usimpe matumaini ya kuendelea kutegemea kwako na badala yake mwambie ukweli, inawezekana au haiwezekani. Kuwa huru na maisha yako, kumsaidia mtu au kutokumsaidia mtu hiyo ni hiyari yako. Usikubali mtu …

Sala Ya Asubuhi

Najua kila mtu anapoamka huwa anasali sala kadiri ya imani yake. Kuomba ni jambo zuri kwa sababu unakua unajiunganisha na nguvu za asili. Sina uhakika kama itakufaa lakini asubuhi unapoamka kuwa na kauli zako chanya utakazokua unajiambia, siyo tu kujiambia, ziandike na ziseme kisha jirekodi na jisikilize na huo ndiyo unakuwa wimbo wako.Sikiliza wimbo wako …

Ili Mambo Yaweze Kwenda Vizuri Unahitaji Vitu Hivi Viwili

Kwenye maisha lolote linaweza kutokea. Hivyo basi, ili mambo yaweze kwenda vizuri, unapaswa kuwa na ; Kuwa na njia ya mbadala, usitegemee kitu kimoja. Kuwa na kitu ambacho kitaweza kuchukua nafasi (back up). Usitegemee namba moja kwa sababu mambo yanabadilika sana. Kwa mfano, kwenye maisha usitegemee chanzo kimoja cha mapato. Kwenye biashara usitegemee mteja mmoja, …

Kwa Nini Watu Wanapaswa Kuwa Na Fedha Taslimu

Kama fedha ingekuwa dini, basi fedha ndiyo dini inayowaunganisha watu wote duniani na kuwa kitu kimoja bila kujali rangi au tofauti zetu za kidini. Fedha ni mfalme, ndiyo ni mfalme kwa sababu ukiwa na fedha ina maliza changamoto zote zinazokukabili. Watu wengi hatuna changamoto, ila changamoto yetu kubwa ni kwamba hatuna fedha ya kutatua changamoto …

Design a site like this with WordPress.com
Get started