Jambo Muhimu La Kujifunza Kutoka Kwa Simba

Kama tunavyojua Simba ndiyo mfalme wa mwituni. Na ufalme wake huu hautokani na yeye kuwa mrefu sana, mzuri sana bali ni mtazamo alionao. Simba ana mtazamo tofauti na wanyama wengine. Ila kikubwa ambacho nimependa kushirikisha kutoka kwa Simba ni Simba anawinda ili apate kitoweo. Hapa unajifunza nini, na wewe fanya mpaka upate matokeo unayoyataka. Hatua …

Inafanya Kazi Vizuri Sana

Maarifa yoyote yale unayopata yanafanya kazi kama ukiyafanyia kazi. Kumbe basi, inafanya kama kazi kama ukiyafanyia kazi.Wengi wanajifunza, wanasoma vitabu wanaishia kuhamasika lakini hawachukui hatua. Kama huchukui hatua huwezi kupata matokeo. Ndoto au chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kifanyie kazi. Usiseme haiwezekani wakati hujaifanyia kazi.Usiseme umeshindwa wakati umejaribu mara moja. Jaribu zaidi, hakuna kitu …

Usiwaangushe Wengine

Chochote kile unachofanya jua hufanyi kwa sababu yako tu bali unafanya kwa sababu ya wengine pia. Sababu ya kufanya isiwe kwa sababu unapata pesa tu kwa sababu unafanya hivyo ni wajibu wako kufanya na wengine wanakutegemea wewe ili maisha yao yaendelee.Chochote kile unachofanya ni huduma kwa wengine. Ukianzisha huduma usisitishe kwa sababu kuna watu wanakutegemea …

Ujumbe Kwa Wauzaji Wote

Katika mauzo, watu wengi wanakuwa wanawachukia watu wa mauzo kwa sababu ya tabia yao ya kuongea sana. Hivyo basi, wewe kama mtu wa mauzo, punguza kuongea sana, na nenda moja kwa moja kwenye hoja, usipoteze muda kwenye maelezo yasiyokuwa na tija. Pili, unapoongea na mteja ongelea zaidi mambo ambayo mteja anapenda. Hapa unatakiwa kujali maslahi …

Kipokee Kama Kilivyo

Huwa tunahangaika na vitu vingine ambavyo viko kabisa ya uwezo wetu. Wala hatuwezi kuviathiri moja kwa moja lakini tunalalamika kweli. Ni kawaida ya binadamu kulalamika kwa jambo lolote lile ambalo halijaenda sawa na vile alivyotaka yeye. Kwenye falsafa ya ustoa, kuna vitu viwili, Moja,Baadhi ya vitu vipo ndani ya udhibiti wetu. Kwa mfano, kudhibiti hasira, …

Kabla Hujafikiria Kupata Fedha, Fikiria Hiki Hapa Kwanza

Kama fedha ingekuwa ni dini basi fedha ndiyo dini inayowaunganisha watu wote duniani bila kujali tofauti zao. Fedha ni jawabu la mambo yote hilo halina ubishi. Kwa sababu kila mtu anataka fedha sasa kabla hujafikiria utapataje fedha, fikiria kwanza kutoa thamani. Fedha zimefichwa katika kutoa thamani, wape watu thamani kwa sababu fedha ni zao la …

Vumilia Matokeo Lakini Siyo Mchakato

Maisha ni mchakato na siyo matokeo ya siku moja. Watu wengi wamekuwa ni watu wa kutaka matokeo ya haraka kwenye maisha yao na kitu ambacho hakipo.Ukilazimisha matokeo ya haraka, utakachopata ni maumivu baadaye. Endelea kukaa kwenye mchakato wa kutafuta kile unachotaka na matokeo ni suala la muda tu. Vumilia matokeo lakini siyo mchakato. Mchakato wa …

Kuwa Mbele Ya Kitu Hiki

Kwenye maisha unapaswa kuwa mbele ya mabadiliko, kabla mabadiliko hayajatokea basi unapaswa kuyawahi. Kwenye kazi, biashara na maeneo mengine ya maisha yetu, usikae mpaka mabadiliko yaje na yakukute hujajiandaa bali mabadiliko yaje, yakukute tayari umeshajiandaa. Kuwa mtu wa kusoma nyakati, ona mbele, ona mabadiliko gani kwenye eneo ulilopo yanaweza kutokea na yafanyie kazi. Ukiwa mbele …

Watu Wananua Kwa Sababu Hii

Watu wananunua kwa sababu zao binafsi. Pata picha wiki umenunua vitu vingapi? Na je, umenunua kwa sababu gani? Ukimuuliza mtu swali hili kila mtu atakuja na majibu yake na hapo unapata jibu kwamba kila mtu ananunua kwa sababu zake binafsi. Ili mtu aweze kununua kwako, kwanza inabidi ujue maumivu ya mteja. Huwezi kuuza kama hujui …

Epuka Ushamba Huu Wa Kitanzania

Wengi wakipata fedha au mafanikio kidogo tu wanakuwa kama wana ushamba wa hela. Na watanzania wengi wana ushamba wa hela, hela kidogo zinamfanya mtu alewe sifa na kujiona hakuna kama yeye kwenye hii dunia.Kitu ambacho watu wengi hawakijui kuhusu utajiri ni hiki hapa, utajiri siyo kile kinachoonekana kwa nje bali ni kile kisichoonekana kwa nje. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started