Kauli ya uchumi mgumu haitokuja kuisha kamwe. Ndiyo wimbo ambao watu wanapenda kuimba. Watu kusema uchumi ni mgumu wala haijaanza leo, hata kama uchumi ni mzuri watu watasema uchumi mgumu. Ile ya wateja kusema hali mbaya ni kawaida kuisikia kila mara, hata mteja awe na hela, kauli pendwa kwake ni uchumi mgumu. Mtu akitaka kukutoroka …
Njia Ya Haraka Ya Kumpoteza Mteja Kwenye Biashara Yoyote Ile
Ni kuahidi halafu usitekeleze ahadi yako. Watu huwa wanakumbuka sana ahadi, hivyo unapoahidi kitu ni bora ukitimize au usiahidi kabisa.Ahidi vile ambavyo viko ndani ya uwezo wako, vile ambavyo unaweza kuvidhibiti. Chochote kile ambacho unamwahidi mteja kwenye mchakato wa mauzo, hakikisha unakitimiza. Usiahidi kitu ambacho hakipo kwenye udhibiti wako. Kuwaahidi wateja mambo mazuri ni moja …
Continue reading "Njia Ya Haraka Ya Kumpoteza Mteja Kwenye Biashara Yoyote Ile"
Ukikosa Vitu Hivi Viwili Utanyanyasika Sana
Ukivikosa vitu hivi, siyo tu utanyanyasika lakini pia hutathaminikiwa. Ni asili kabisa na kamwe huwezi kwenda kinyume na asili. Vitu ambavyo kama huna basi utaishia kuburuzwa ni;Moja, huna fedha. Fedha ni jawabu la mambo yote. Sehemu yoyote ile ukikosa fedha utadharauliwa. Tukiachana na hewa tunayovuta, kinachofuata kwa umuhimu ni fedha. Fedha ndiyo inaendesha maisha yetu, …
Continue reading "Ukikosa Vitu Hivi Viwili Utanyanyasika Sana"
Sababu Nyingi Unazojipa Ni Kwa Sababu Hii Hapa
Rafiki yangu nikupendaye, Sababu nyingi tunazojipa ni kwa sababu ya sauti za ndani. Kwa mfano, umepanga kufanya kitu fulani labda kumpigia mteja simu, sauti ya ndani inakuambia usipige simu, huenda huyo mtu atakua ana kazi kwa sasa na tunapokuwa tunaitii sauti ya ndani ya kutokufanya basi hapo tunakua tumeisha. Sauti ya ndani ndiyo inakukosesha kupata …
Continue reading "Sababu Nyingi Unazojipa Ni Kwa Sababu Hii Hapa"
Utumwa Pekee Unaopaswa Kuwa Nao
Kuliko kuwa mtumwa wa kulalamika, kukata tamaa na kila aina ya mtazamo hasi.Wewe kuwa mtumwa wa MATUMAINI Kuwa mtumwa wa MATUMAINI, amini katika ndoto zako, amini mambo yanawezekana na endelea kukaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachoamini. Kuwa mtumwa wa MATUMAINI lakini hakikisha uko katika mchakato sahihi. Usiwe na matumaini kama hauko katika njia sahihi. …
Fanya Kama Vile Hutaki Pesa
Kuna kitu kimoja cha kushangaza kwenye tabia za binadamu, watu huwa wanahangaika na kile ambacho hakiwajali. Kwa mfano, Benki huwa zinawapa mikopo wale ambao hawazihitaji sana hizo fedha za mikopo. Makampuni makubwa ya sanaa huwa yanawapa mkataba wasanii ambao hawahitaji hata mkataba wao.Watu huwa wanawapenda sana watu ambao hawana hata muda nao. Ni kanuni ya …
Nafasi Za Kazi
Watu wanalalamika kuwa hakuna nafasi za kazi. Lakini siyo kweli, nafasi za kazi zipo ila changamoto ni watu.Waajiri wengi wanakuwa na maono makubwa lakini wanakosa watu sahihi wakusaidiana nao. Utakuja kuliona hili changamoto siyo kazi, bali changamoto ni watu. Nafasi za kazi zipo ila changamoto ni watu.Watu ni rahisi kuanzisha kitu lakini ni wagumu kumaliza …
Kama Kweli Unampenda Wa Kwanza, Usingefanya Hivi
Mtu mmoja aliwahi kusema, kama umewapenda watu wawili na unatakiwa kubaki na mmoja, unatakiwa kumchagua wa pili. Kwa sababu kama ungekuwa unampenda kweli wa kwanza usingeenda kwa wapili.Hapa tunajifunza nini? Kile ambacho unakipa muda sana kwenye maisha yako ndiyo unakipenda. Hivyo basi, unatakiwa kukipa muda kitu ambacho unakipenda ili kiweze kukupa matokeo mazuri.Biashara na kazi …
Continue reading "Kama Kweli Unampenda Wa Kwanza, Usingefanya Hivi"
Huwezi Kujikimbia
UENDAPO NDIPO ULIPO, HUWEZI KUJIKIMBIA.Watu wengi wanapokuwa na msongo au sonona, huwa wanaona kubadili mazingira kwa kusafiri itabadili hali yao.Lakini hilo siyo linalotokea, pamoja na kusafiri, watu bado hujikuta wakiendelea kuwa kwenye hali zile zile. Sasa Mwanafalsafa Seneca anatufundisha kwamba kitakachobadili hali zetu siyo kubadili mazingira yetu, bali kubadili mtazamo na fikra zetu.Kama hutabadili mtazamo …
Kuwa Mwema Na Tenda Mema
Falsafa rahisi ya kuishi maisha bora ni kuwa mwema na tenda mema. Na njia rahisi ya kuishi falsafa hiyo ni hii hapa, kama kitu siyo sahihi usifanye. Na kama kitu siyo kweli, usiseme. Ukiishi kwa misingi hiyo miwili itakusaidia bora. Hatua ya kuchukua leo; kuwa mwema na tenda mema. Mara zote ishi falsafa hii pale …