Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kushindwa Kwenye Maisha Yako Kuna Anzia Hapa

Kushindwa kwenye maisha yako kuna anzia pale unapoipoteza siku yako moja. Kwa sababu, mafanikio ni mkusanyiko wa siku nyingi unazoishi kimafanikio kila siku.

Jim Rhon anasema siku ni ghali sana na unapotumia siku moja maana yake umepunguza siku kwenye maisha yako.

Maisha ndiyo haya haya, ukitumia muda wako vizuri inakuwa ni faida kwako na ukitumia muda wako vibaya inakuwa imekula kwako.

Usikubali kupoteza siku yako kizembe, kila siku fanya jambo la maana ambalo litaacha alama, usiamini kesho kwa sababu hakuna mwenye uhakika wa kesho.

Tumia siku zako kwa umakini mkubwa sana. Usikubali kupoteza muda, kuwa bahili wa muda wako na utumie kuzalisha zaidi.

Ukiwa unafanya kitu, jiulize hiki nachofanya kinafanya maisha yangu kuwa bora? Ukiona hakina umaana acha hapo hapo na kafanye chenye umaana.

Hatua ya kuchukua leo; chukulia kila siku inayopita kama siku unayokaribia kifo chako na usikubali kabisa kupoteza hata siku moja.

Kwahiyo, kila siku hesabu yapi ni muhimu unayofanya na yanakupeleka kwenye mafanikio makubwa?
Muda wako ni ghali sana, usiuchezee na kuupoteza kwa mambo yasiyokuwa na mashiko.
Kumbuka, siku zako zinahesabika, tumia muda wako vizuri sana.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: