Design a site like this with WordPress.com
Get started

Agiza Tukuletee

Maisha yamebadilika, zama zimebadilika na watu wamekuwa na mambo mengi huku muda ukiwa mchache sana ukilinganisha na mambo wanayotakiwa kufanya.

Ili ufanikiwe kwenye mauzo unatakiwa kupiga pale kwenye maumivu. Huwezi kuuza kama unapiga kwenye uimara wa mtu bali utaweza kuuza kama ukipiga kwenye udhaifu wa mtu.

Ili upate ushindi wowote ule, usikimbilie kwenye uimara wa mtu bali kimbilia kwenye udhaifu wa mtu.

Ona ni kitu gani hajui, kisha kuwa sehemu ya kumsaidia kwa namna hiyo utakuwa rahisi kukubaliana naye lakini pia kujenga ushawishi.

Kwa kuwa watu wengi kwa sasa wana mambo mengi, tumia huo udhaifu wao kuwasogezea huduma karibu yao.

Watu wanapenda kitu ambacho kinawaokolea muda, na ukija na suluhisho la kuwaokolea muda watafurahi sana.

Kwenye kazi au biashara unayofanya anza kuwatafuta wateja, waombe oda kuhusiana na kile unachouza na kisha waombe waagize na kisha wapelekee.

Nimefurahishwa na rafiki yangu Reifrid Maganga leo asubuhi katika kipindi cha Billionaires in Training baada ya kuona eneo analokaa lina fursa akaamua kuitumia hiyo kama sababu ya kuanzisha biashara ya kuagiza mzigo tukuletee kwani eneo wanapokaa ni mbali na mjini na watu wanashindwa kupata huduma.

Hata wewe kama unafanya biashara, usisubiri mpaka mteja aje, jaribu kuwatembelea wateja wako, waombe wakupe oda na uwapelekee huko walipo.

Tibu maumivu ya watu na njoo na suluhisho litakalowasaidia.

Hatua ya kuchukua leo;
Angalia ni maumivu gani au udhaifu gani unaowasumbua watu na biashara yako inaweza kuja na suluhisho gani kwa ajili ya kusaidia hao watu.

Kwenye kitabu chake Godius, anasema maisha ni fursa, zitumie zikubebe.
Nami naongezea changamoto za watu kwenye maisha ni fursa nzuri ya kuanzisha biashara na kutoa huduma bora, tumia maumivu ya watu kama fursa kwa kuja na suluhisho lake ili zikubebe.

Ongea na wateja wako leo, waombe miadi na kisha tambulisha huduma mpya ya agiza tukuletee. Wateja hawana muda, hivyo wasaidie kuwapelekea huduma bora hapo walipo.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: