Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Kinaathiri Maisha Yako

Dunia inatufundisha vitu vingi, kwa kuona, kusikia na kwa kufanya.

Asili huwa inatufundisha vitu vingi sana katika maisha lakini changamoto kubwa ya watu wengi hawajui namna ya kukielewa kile ambacho asili huwa inawafundisha.

Ruben Gonzalez aliwahi kunukuliwa akisema, kinachoathiri maisha yako siyo kinachotokea, bali jinsi unavyopokea na kufanyia kazi kinachotokea.

Nakubaliana na Ruben Gonzalez kwa sababu asili inatufundisha mengi yanayotokea kwenye maisha yetu. Lakini jinsi tunavyopokea na kufanyia kazi kinachotokea ndiyo changamoto yetu iko hapo.

Kwa mfano, pale unapokutana na changamoto yoyote ile usilalamike bali kaa chini jifunze kutokana na kile kilichotokea na kwa njia hiyo utaweza kunufaika zaidi.

Hatua ya kuchukua leo; fanyia kazi hii nukuu, rudia tena sentensi hii kuisoma; kinachoathiri maisha yako siyo kinachotokea, bali jinsi unavyopokea na kufanyia kazi kinachotokea.

Habari njema ni kwamba, unayo mengi yaliyokutokea katika maisha yako, nenda kayapokee katika namna ya mtazamo chanya na kufanyia kazi yale yote yanayotokea kwenye maisha yako.

Kwenye kila kinachotokea kwenye maisha yako, kuna funzo, hivyo jifunze kujifunza na kuchukua hatua.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: