Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Ambacho Huwa Hakikosi Matumizi

Binadamu sisi ni watu wa kujisahau pale maisha yetu yanapobadilika. Ukiwa huna fedha utakuwa na mipango mizuri sana lakini fedha ikishapatikana mipango mizuri yote inapotea na inakuja kurudi pale ambapo huna kitu mfukoni.

Rafiki, kitu ambacho huwa hakikosi matumizi kama ukiwa nacho ni fedha. Fedha ikiwepo tayari matumizi hujitokeza yenyewe.

Unatakiwa kuwa makini na fedha zako. Dhibiti matumizi yako yale ambayo hujapangilia. Fanya matumizi kwa vitu ambavyo ni muhimu tu na usipofanya hivyo maisha yako hayawezi kwenda.

Kwa matumizi ambayo yanaweza kusubiri usifanye manunuzi yasubirishe kwanza.

Unapokuwa na fedha usikubali kuendeshwa na hisia za kununua vitu. Fedha isikutawale wala kukuendesha. Wewe ndiyo unatakiwa kuitawala na kuidhibiti fedha.

Kuwa na kiasi kwenye kila kitu. Kwa sababu ukiwa na fedha tayari matumizi yanajitokeza yenyewe. Usipokuwa makini utajikuta unamaliza fedha zako kwa matumizi mabaya.

Hatua ya kuchukua leo; Kuwa na nidhamu ya fedha. Usikubali kuendeshwa na fedha bali wewe ndiyo uzitawale fedha zako.

Hivyo basi, uwe na bajeti inayokuongoza katika matumizi na siyo ukiwa na fedha usukumwe kununua kila unachokutana nacho.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: