Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huna Mkataba Wa Kuishi Naye Milele

Vitu vyote ambavyo tunafanya hatuna uhakika navyo asilimia mia moja. Kitu ambacho kwa kila mmoja ana uhakika nacho asilimia mia moja ni kifo tu. Haya mambo mengine yote hatuna uhakika nayo kwa sababu ni vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu.

Wazazi kuwapenda watoto wao ni kitu kizuri sana. Lakini, baadhi ya wazazi wanajisahau sana katika malezi ya watoto wao. Watoto wanageuka kuwa wafalme katika familia na wazazi wanakua hawana kauli.

Uwe na mipaka kwa watoto wako. Wape haki zao zote lakini usisahau kuwapa watoto wajibu wao. Watoto nao wanatakiwa kuwajibika kwenye zile shughuli za nyumbani na siyo mtoto kutokufanya kitu chochote kile eti kwa sababu unampenda sana. Je, huko ni kumpenda sana au kumharibu mtoto?

Mzazi mfundishe mtoto kuvua samaki na siyo kumpa samaki. Kumbuka, huna mkataba naye wa kudumu wa kusema kwamba utaishi naye milele. Hutakua naye kila siku hivyo mfundishe mtoto wako kazi.

Mruhusu mtoto akutane na changamoto ili aweze kujifunza.

Mfundishe mtoto kazi. Yale majukumu ambayo mtoto anapaswa kufanya nyumbani afanye na asifanyiwe kila kitu kwa sababu utamwaribu.

Mfundishe mtoto kujitegemea. Asimame na miguu yake mwenyewe. Mpe misingi imara kwenye kila eneo la maisha yake.
Mpe misingi kisha mwache ajaribu ili asili imfundishe.

Mwache mtoto akosee ili ajifunze. Mwache mtoto ajaribu ili ajifunze.

Usimchagulie mtoto kuishi ndoto unayotaka wewe. Bali mwache achague ndoto anayoipenda yeye mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; mfundishe mtoto kuvua samaki na siyo kumpa samaki.

Mfundishe mtoto misingi ya maisha kuanzia eneo la kiroho, kimwili na kiakili. Mtoto akikosa misingi kitu chochote kitaweza kumwangusha.

Kumpenda mtoto ni pamoja na kumfundisha uwajibikaji kwenye kile anachotakiwa kufanya.
Iwe ni mtoto wa kike au wa kiume wafundishe maadili mazuri ambayo yatakuja kuwasaidia kukabiliana na maisha huko mbeleni.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: