Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Mbili Za Kuepuka Kujivuruga Kwenye Maisha Yako

Maisha tayari ni magumu lakini watu tunayafanya maisha kuwa magumu zaidi kwa kulazimisha mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu.

Siku moja nilikuwa nasoma kwenye mtandao wa kisima cha maarifa nikakutana na vitu viwili ambavyo huwa vinawavuruga watu.

Kwa lugha rahisi msongo ni hali ya kuvurugwa. Sasa kuna vitu ambavyo huwa vinawafanya watu kuvurugwa zaidi.

Moja ni kutokukubaliana na hali iliyotokea. Jambo lolote linapotokea kubaliana nalo kwanza maana usipokubali unazidisha yali ya msongo zaidi.
Kubali kile kilichotokea ili ujipange kukikabili.

Mbili ni kulazimisha jambo. Wako watu ambao huwa wanapenda kulazimisha mambo yawe kama vile wanavyotaka wao.

Kulazimisha mambo yawe kama unavyotaka wewe ni kwenda kinyume na sheria ya asili. Wewe siyo kiranja wa dunia wakulazimisha dunia iende kama unavyotaka wewe.

Rafiki, pale unapojikuta kwenye msongo au umevurugwa angalia vitu hivi viwili moja huenda hujakubaliana na jambo lilitokea na mbili huenda unalazimisha mambo yatokee kama unavyotaka wewe.

Hatua ya kuchukua leo; kubaliana na matokeo kama yalivyo na usilazimishe mambo kama vile unavyotaka wewe.

Usiyavuruge maisha yako kwa kulazimisha mambo na kutokubaliana na matokeo. Huwezi kupingana na ukweli, ishi kadiri ya ukweli na utakua na amani.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: