Iko wazi kuwa watu huwa wanapenda kujihusisha na watu wanaowajua. Ni ngumu sana watu kujihusisha na watu wasiowajua.
Wewe hushangai ule usemi unaosema haijalishi unajua nini bali unamjua nani. Huu msemo huwa unasema kweli.
Kama unataka kufanikiwa hakikisha unakuwa na watu. Kwani utajiri wako ni wastani wa watu unaojihusisha nao.
Mafanikio unayotafuta yako tayari kwa watu wengine.
Kumbe basi, unatakiwa kutengeneza mahusiano bora na wengine ili upate kile unachotaka kutoka kwao.
Unapokuwa na shida huangalii unajua nini bali unamjua nani ambaye anaweza kukusaidia changamoto uliyonayo. Kwa mfano, hata ukifungua biashara huwezi kujiuzia mwenyewe lazima utawategemea wengine ili wanunue.
Hatua ya kuchukua leo; jihusishe na watu chanya ambao unajua watakusaidia pale unapokutana na changamoto. Hakikisha unajuana na watu kwani watu huwa wanajihusisha na wale tu wanaowajua.
Kwa hiyo, leo nenda katafakari huu msemo kuwa haijalishi unajua nini bali unamjua nani. Huwezi kufanikiwa bila watu. Ni kazi yako sasa kujenga mahusiano bora na wengine ili uweze kupata kile unachotaka kutoka kwao.
Kwa chochote utakachofanya lazima utawategemea wengine ili kukikamilisha. Hata ukisema wewe ni jeshi la mtu mmoja huo ni uongo kwani wewe siyo kisiwa.
Kujitegemea siyo kujitosheleza hivyo licha ya kujitegemea kumbuka kuhusiana na watu kwani mafanikio unayotafuta yako kwa wengine.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo
Asante sana Deo,
Watu chanya ni muhimu sana katika maisha ya mafanikio.
Umekunikumbisha kuhusu msemo usemao ” Jeshi la mtu mmoja ”.
Huwa siuelewi msemo.
Asante sana kwa makala nzuri.
Rafiki yako,
Aliko Musa
LikeLike
Karibu sana Mr Aliko Musa.
Jeshi la mtu mmoja maana yake ni mtu kujitegemea kwa kila kitu. Yaani wewe pekee yako unaweza bila wengine.
LikeLiked by 1 person