Njia yenyewe ni kifo.
Ukifikiria majukumu uliyonayo, watu wanaokutegemea katika familia yako huku ukifikiria siku yoyote utakufa huwezi kufanya ujinga utajisukuma kufanya makubwa.
Aliyekuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kila mara katika hotuba zake alikuwa anaongelea kifo. Anasema kama akifikiria siku moja atakufa je akifa leo hii miradi aliyoiacha nani ataindeleza? Akifikiria hivyo anaamua kufanya kazi.
Hata wewe unaweza kujifunza kupitia kifo na kujituma zaidi.
Ukifikiria mipango unayopaswa kuitekeleza na siku moja utakufa usipange kuahirisha hata kidogo.
Usipoteze ndoto yako. Anza kuifanyia kazi ndoto yako kabla hujafa. Tumia fursa ya uhai kufanya mambo makubwa yatakayoacha alama kwenye maisha yako hata pale utakapoondoka kazi zako zitaongea kwa niaba yako.
Hatua ya kuchukua leo; Tafakari juu ya kifo na kisha jiambie iko siku moja utakufa hivyo basi, unapaswa kufanya kazi unazopaswa kufanya.
Kwa hiyo, kichukulie kifo kama hamasa kwako ya kuthubutu zaidi.
Kumbuka chuma kisipotumika kitapata kutu. Nawe ni wakati wako wa kutumika ili usipate kutu.
Tumia muda wako vizuri kabla hujaondoka hapa duniani.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo