Antisthenes ni mwanafalsafa wa kigiriki. Mwanafalsafa huyu aliwahi kusema hivi juu ya adui yako. ” Wasikilize maadui wako, kwa sababu ni wa kwanza kugundua makosa yako.”
Ni kweli maadui wako huwa wanagundua makosa yako sana kuliko watu wengine. Hivyo fuata ushauri uliopata leo kutoka kwa mwanafalsafa Antisthenes.
Hivi hujawahi kujiuliza ni kwa nini Yesu alisema wapende adui zako?
Usimchukie adui yako kwani adui wakati mwingine anakupa hamasa ya wewe kuendelea kuwa bora zaidi.
Ukimchukia adui au mpinzani wako unajidanganya mwenyewe kwa sababu hutaona mazuri ya wapinzani au maadui bali utaona mabaya tu.
Kumbuka, chuki humchoma anayeitunza. Achilia chuki ili uweze kuishi kwa amani.
Jifunze kwa Aliyeumba mbingu na nchi huwa akiachia mvua huwanyeshea wabaya na wema na sasa wewe kwanini unawachukia maadui zako?
Hatua ya kuchukua leo; Wapende adui zako.
Usiangalie upande wa ubaya tu bali angalia upande wa mazuri tu.
Ila kumbuka kiasili hakuna baya wala zuri. Wewe mwenyewe ndiyo unatengeneza mazuri au mabaya kwa mitazamo yako mwenyewe.
Mtazamo wako ndiyo chaguo lako.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo