Kama unataka kupata fedha zaidi inakupasa utoe thamani zaidi.
Fedha haziwezi kuja tu kwako kama huna mitego ya kuinasa. Mitego mizuri ya kunasa fedha ni kuwa na vitega uchumi vingi. Yaani unakuwa unatoa thamani kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato ulivyotega.
Tabia mojawapo ya fedha inapenda mtu mbunifu. Usipokuwa mbunifu wa miradi mbalimbali fedha zitakukimbia na kwenda kwa mtu ambaye ni mbunifu. Ukitaka uwe na fedha zaidi kuwa mbunifu wa namna ya kutoa thamani kupitia kazi, biashara nk.
Fedha humtoroka mtu mvivu. Kumbe basi, unapotaka kupata fedha zaidi, kuwa mtu wa bidii na epuka tabia ya uvivu.
Katika kila kazi kuna faida hii ni kadiri ya kitabu cha Methali. Ukifanya kazi yoyote halali lazima utapata faida ndani yake.
Fedha zinapenda mtu mwenye bidii. “Mawazo ya mwenye bidii huelekea utajiri tu; bali kwa kila mwenye pupa huelekea uhitaji”
Katika kila jambo kunahitajika bidii. Bidii ni nguvu iwezeshayo mtu kufikia malengo yaliyo mbele yake.
Ukitaka kupata fedha zaidi, kuwa mtu wa kutoa zaidi. Fedha haipendi mtu bahili. Ubahili wa kutokutoa ili uzalishe zaidi. Ili upate uwe mtu wa kutoa kile ulichonacho ili upokee kile ambacho hauna.
Hatua ya kuchukua leo; nenda kaongeze bidii katika kuongeza vyanzo vya mapato yako.
Weka mitego mingi kiasi kwamba fedha ikipita anga zako inanasa tu.
Fedha huleta jawabu la mambo yote. Na fedha ni kitu kizuri na wala siyo kitu kibaya. Mtumiaji wa fedha ndiyo anayefanya fedha kuwa nzuri au mbaya lakini fedha yenyewe haina shida.
Mungu anataka tuwe na fedha kwa ajili ya mambo mawili. Moja kwa ajili ya kuendeleza ufalme wake na pili kwa ajili ya mahitaji yetu ya kila siku.
Fanya bidii ya kuwa na fedha ili uendeleze ufalme wa Mungu na upate kufanya mahitaji yako ya kila siku.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo