Rafiki,
Kazi ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato.
Na tukirudi katika msingi wa fedha tunaambiwa kuwa fedha ni zao la thamani hivyo kama huna unachotoa, basi ni wazi kwamba hutoweza kupata kitu.
Kumbe basi, fedha ni kutoa na kupokea.
Usitegemee utafanikiwa kifedha kwa njia ya dhuluma.
Fedha ya dhuluma huwa haikai itaondoka kwako kama ilivyokuja.
Usipende fedha ambayo hujaifanyia kazi. Utawakuta wanalalamikia fedha za watu ambazo hata hawajazifanyia kazi.
Usitamani fedha au kitu kukipata kama hujakifanyia kazi.
Fanyia kazi kile unachotaka na kuwa tayari kupata matokeo yake.
Usitamani fedha ambayo hujaitolea jasho.
Kula matunda ya jasho lako mwenyewe.
Ndiyo maana wale ambao wanatamani fedha ambazo hawajazifanyia kazi wanaishia kuzipoteza tu.
Kuwa huru kupambana na haki yako lakini kitu ambacho siyo jasho lako usikitamani kukipata bila kukifanyia kazi.
Unaweza kuwa tajiri bila kuiba, ziko njia sahihi zitakazoweza kukupatia kile unachotaka katika maisha yako.
Fedha ina mtindo wa kumkimbia yule ambaye hana anachotoa nje na kwenda kwa yule anayetoa.
Hatua ya kuchukua leo; Tamani vitu ambavyo unavifanyia kazi , vitu halali ambapo unavitolea jasho lako.
Hivyo basi, fanya kazi halali ambayo itakupatia fedha halali.
Jua kabisa kuwa fedha ni rafiki yetu mzuri. Tunapaswa kutembea naye na kuwa naye. Ila anapenda mtu ambaye ni mwandilifu na siyo vinginevyo.
Kila la heri rafiki yangu.
Makala hii imeandikwa na
Deogratius Kessy
Unaweza kujifunza zaidi kupitia kundi la Wasapu linalojulikana kwa jina la mimi ni mshindi nimezaliwa kushinda.
0717101505//0767101504
Karibu sana mwanamafanikio,
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
http://www.mtaalamu.net/kessydeo
Asante sana