Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Kiwango Sahihi Cha Fedha Unachopaswa Kupata Kila Mwezi

Rafiki,

Fedha ni muhimu katika maisha yetu hilo halina ubishi kabisa. Karibu kila kitu kinahitaji fedha ili mambo mengine yaende katika maisha yetu bila fedha mambo yanakuwa ni magumu lakini tukiwa na fedha mambo mengi yanawezekana.

Kileambacho tunakipata kila mwisho wa mwezi, kila siku, wiki ambacho ni kipato tunachopata kutoka katika kazi au biashara. Ni fedha ambayo akili yetu tayari imeshajua kuwa tunapata kiasi gani hivyo hata akili inaandaa mazingira ya kuwa na matumizi kadiri ya hiyo hela na ikitokea kikipatikana akili itahakikisha unahaingaika mpaka unapata kile kiwango ulichopaswa kukipata.

Unatakiwa kuizoesha akili yako kufikiria viwango vikubwa vya fedha. Na njia nzuri ya kuizoesha akili viwango vikubwa vya fedha ni pale unapochukua kiwango chako cha fedha unachokipata sasa hivi kwa kuzidisha mara kumi .

Kwa mfano, kama ulikuwa unapata kipato chako cha fedha kila mwezi shilingi elfu 50 basi chukua hiyo elfu 50 zidisha mara kumi na utapata laki tano. Hapo utaipa akili yako ni wapi utaweza kupata fedha hiyo.

Kila mtu akizidisha kipato anachopata kwa sasa mara kumi hiko ndiyo kiwango halisi cha fedha unachotakiwa kukipata kila mwezi. Hii ni njia inayokupa kazi ya kukusanya fedha ili uweze kufikia kile kiasi halisi.

Usipoizoesha akili yako kufikiria viwango vikubwa vya fedha utaishia kupata fedha za kawaida. Acha akili yako iwaze kiwango cha fedha cha juu sana kiasi kwamba hata ukija kuzipata akili itazoa. Unakuta wale wanaostaafu wakipata kiwango kikubwa cha fedha akili zao huwa zinalewa kwanza, zitatumia ile fedha vibaya mpaka iishe ndiyo akili itarudi kwa sababu akili haijazoea kuwa na kiwango kikubwa cha fedha.

SOMA; Kama Unataka Kiasi Kikubwa Cha Fedha, Badili Kwanza Kitu Hiki

Hatua ya kuchukua leo; fedha ni rafiki yetu mzuri, hivyo tufanye kazi ili tuweze kufikia uhuru wa kifedha. Nenda kazidishe kiwango cha fedha unachopata sasa mara kumi na hicho utakachokipata ndiyo kiwango sahihi unachopaswa kukipata kila mwezi.

Kwahiyo, tumia akili yako vizuri kuiwazisha mambo makubwa. Huwa tunaanza kujenga picha ya kile tunachotaka kwenye akili zetu. Hivyo ni wakati wako sasa wa kujenga kiwango cha fedha unachohitaji.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: