Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huu Ndio Wakati Sahihi Na Muhimu Wa Wewe Kuishi Hapa Duniani

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu uko salama na unaendelea vizuri kutafuta ushindi kwenye kile unachofanya. Rafiki, hongera sana kwa zawadi ya kipekee sana ya siku hii ya leo kama unasoma hapa natumaini na wewe utakuwa umenufaika na zawadi ya siku hii ya leo. Hivyo basi, tunamshukuru Mungu kwa mapenzi yake kwa kutustahilisha kuiona siku hii ya leo hivyo tunadeni la kuitumia vizuri siku hii ya leo kufanya maisha yetu kuwa bora pamoja na wengine wanaotuzunguka.

Image result for present moment

Mpendwa msomaji wangu, nikupongeze pia kwa kuendelea kusafiri pamoja na mimi kila siku kupitia mtandao huu na tutaendelea kujifunza kila siku kadiri ya mapenzi ya Mungu. kwahiyo, naomba nitumie nafasi hii kukualika wewe mpendwa msomaji wangu katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja somo zuri nililo kuandalia siku hii ya leo hivyo nakusihi tusafiri pamoja mpaka mwisho wa somo letu. Karibu rafiki tujifunze ambapo katika somo letu la leo tutakwenda kujifunza muda mzuri wa wewe kuishi hapa duniani.

Rafiki, muda mzuri wa wewe kuishi hapa duniani ni sasa, wala siyo kesho wala jana. Kesho bado haipo katika maisha na kamwe haitokuja katika maisha ya binadamu. Na jana tayari imeshapita katika maisha yako usitegemee jana kuja tena katika maisha yako. Baadae tena huna uhakika nayo ila muda mzuri uliobaki na wa kipekee wewe kuishi ni sasa rafiki na siyo baadae. Kama unataka kupata furaha ya kweli katika maisha yako basi ishi maisha yako ya sasa na wala usiishi maisha yako jana achana na kufikiria kuhusu jana kwani ukifikiria kuhusu jana na yaliyopita ni njia nzuri ya kujiingiza katika msongo wa mawazo na hali ya kutokua na furaha. Vilevile, njia nzuri ya kupoteza muda wako ni kuishi maisha ya jana yaani yaliyopita. Fanya ya sasa kwanza na ya baadaye yatakuja kama unafanya kazi yako weka akili yako yote na nguvu zako zote kwenye kile unachofanya sasa.

SOMA;  Hii Ndio Zawadi Ya Kipekee Sana Uliyopewa Kutoka Kwa Mungu

Ndugu, watu wengi wanakata tamaa katika maisha yao kwa sababu ya kutokuishi maisha yao ya sasa. Muda ambao una uhakika nao katika maisha yako ni sasa rafiki hivyo hakikisha unaitumia sasa vizuri ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote lile. Sasa ni njia nzuri ya kushinda kuahirisha mambo katika maisha yako na kushinda sababu nyingi katika maisha yako. Mwandishi na mwanafalsafa Lucius Annaeus Seneca aliyezaliwa karni ya nne (4 BC) kabla ya Yesu kuzaliwa na kufa mwaka 65 baada ya Yesu kuzaliwa (65 AD) aliwahi kusema furaha ya kweli ni… kufurahia sasa, bila wasiwasi na utegemezi juu ya hali ya baadaye. ‘’ true happiness is… to enjoy the present, without anxious dependence upon the future’’ Kwahiyo, kama unataka furaha ya kweli bila wasiwasi na utegemezi wowote basi ishi wakati wa sasa.

Hatua ya chukua leo; wakati muhimu ambao una uhakika nao katika maisha yako ni sasa hivyo tumia wakati wa sasa kufanya mabadiliko katika maisha yako. Kama ulipanga kufanya jambo Fulani kesho au baadaye basi kumbuka huo sio wakati wako rafiki wakati wako ni sasa na utumie vizuri. Ukifanya jambo moja weka akili yako yote na nguvu kwenye jambo unalofanya wala usihangaike na vitu vingine fanya kwa ustadi wa hali ya juu ili kupata matokeo bora.

SOMA;  Hii Ndio Mbinu Bora Ya Kumsaidia Mtu Ambaye Hajui Kwenda Na Muda Kwenye Maisha Yake

Kwahiyo, sisi kama binadamu tunaalikwa kutumia vizuri na kuishi wakati wetu sasa. Wakati wa kesho na baadaye ni wakati ambao hatuna uhakika nao. Kama umestahilishwa kuwa wakati huu basi utumie wakati wako wa sasa kwani ndio njia bora ya kukufanya wewe kuishi maisha bora yenye furaha na mafanikio.
Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: