Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndio Siri Ya Nyuma Ya Pazia Katika Mafanikio

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu uko salama na umeanza siku yako kwa ushindi na furaha. Hongera kwa zawadi ya siku hii ya leo ni imani yangu kwamba utaitumia vizuri siku hii kuleta mabadiliko chanya sehemu uliyopo. Rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja yale mazuri niliyokuandalia leo. Nakusihi sana rafiki karibu tusafiri pamoja mpaka mwisho wa makala hii.

Related image

Leo tutakwenda kujifunza kuhusu siri ya nyuma ya pazi katika jambo lolote lile. Je ungependa kujua ni siri gani ya nyuma ya pazia? Karibu tuweze kujifunza kwa pamoja. Katika jambo lolote kama unataka kufanya na kupata matokeo mazuri lazima kuna siri ya nyuma ya pazia. Na siri hiyo si kitu kingine bali ni maandalizi. Jambo lolote unalotaka kufanya lazima ufanye maandalizi ya kutosha. Kabla ya kwenda kuongea mbele ya watu lazima ujiandae kimwili na kiakili kama unakwenda kuongea mbele ya watu na una andaa kuongea kitu gani. Kama unataka uwe mwanarihadha bora lazima ufanye mazoezi kila siku ya maandalizi kabla ya mashindano. Kama unahitaji chakula lazima ufanye maandalizi ya kupata chakula hakitokuja tu hivi hivi lazima kutakua na mchakato wa kukiandaa mpaka kiive na inafikia muda wa kupakua.

SOMA;  Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu Cha Secrets Of The Richest Man Who Ever Lived

Rafiki, maisha yetu yanahitaji maandalizi kwenye kila idara ya maisha yetu. Ili upate mavuno mazuri ni lazima uandae maandalizi mazuri na usipojianda na kuwa na maandalizi mazuri basi utakua umejiandaa kushindwa. Unaweza kuona mifano mbalimbali ya watu wanaofanya kazi zao kwa kujiandaa na wale ambao hawajiandai kuna tofauti kubwa sana. mtu aliyefanya maandalizi anakuwa ana ufanisi mzuri katika uzalishaji ukilinganisha na mtu ambaye hana maandalizi ya kutosha. Kama wewe unataka kufanikiwa katika jambo unalofanya lazima utenge muda wa kujiandaa kabla ya kufanya jambo hilo. Pata maandalizi ya kutosha kwani maandalizi mazuri yanazuia utendaji duni katika matokeo ya kile tunachofanya.

Hatua ya kuchukua leo. Fanya maandalizi mazuri kabla ya kwenda kufanya jambo lolote lile. Kama ulikuwa unafanya vitu vyako bila maandalizi acha kuanzia sasa. Jiandae vizuri kwani maandalizi mazuri ndiyo ishara ya ushindi. Maandalizi mazuri yanatabiri ushindi na matokeo ya ushindi.

SOMA ZAIDI;  Ifahamu Bidhaa Inayopendwa Kununuliwa Na Watu wengi

Kwa kuhitimisha, mpendwa msomaji, somo letu la leo linatualika sisi sote kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kwenda kutenda jambo Fulani. Jipe muda wa kujianda na kujinoa vema kabla ya kwenda kutenda. Maandilizi mazuri ni ishara ya ushindi mzuri.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: