Design a site like this with WordPress.com
Get started

Amka Na Fanya Mabadiliko Haya Muhimu Kwenye Maisha Yako

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko salama rafiki yangu na unaendelea vizuri katika maisha yako. Leo ni siku nyingine ya kipekee sana kwetu katika maisha yetu hivyo tunaalikwa sote kumshukuru Mungu kwa zawadi hii ya uhai na tuitumie vizuri siku hii ya leo kuleta mabadiliko ambayo tunataka kuyaona katika dunia yetu. Mpendwa msomaji, napenda kukualika katika makala yettu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja mambo mazuri niliyokuandalia siku hii ya leo. Nakusihi sana rafiki ungana nami tuweze kusafiri pamoja mpaka mwisho wa somo letu la leo.

Image result for wake up and change

Leo kupitia somo letu la leo tutakwenda kujifunza jambo muhimu la kwenda kulifanya katika maisha yako. Je ni jambo gani hilo rafiki? Karibu tuweze kujifunza kwa pamoja. Leo napenda nikushirikishe zoezi muhimu la kufanya katika maisha yako ili uweze kupata matokeo chanya kwenye maisha yako. Kama unataka mabadiliko katika maisha yako rafiki lazima ufanye jambo hili muhimu katika maisha yako nalo ni kuamka na kubadilika (wake up and change). Unatakiwa kuamka na kubadilika ili kuweza kupata matokeo Fulani. Kama unaishi maisha ya kuigiza amka na badilika na anza kuishi maisha yako, kama umekuwa mtumwa na mlevi wa kuangalia TV amka na badilika kwani unajiua mwenyewe.

SOMA; Hii Ndio Siri Ya Nyuma Ya Pazia Katika Mafanikio

Kama unatumia muda mwingi kuongea bila kuzalisha chochote mpaka siku inaisha amka na badilika anza kuzalisha leo. Upo katika hali ya madeni sugu na kuishi maisha ya kukopa kila siku amka na badilika rafiki kwani madeni sugu ndio njia nzuri ya kubaki katika umasikini. Kama unanunua vitu kwa kuongozwa na hisia badala ya akili amka na badilika sasa na usinunue vitu kwa kuongozwa na hisia. Kama wewe ni mtu wa kuishi juu ya kipato chako amka na badilika kuishi juu ya kipato chako ni njia nzuri ya kubaki kwenye umasikini. Unaishi maisha bila ya kujilipa kwanza wewe pale unapopata hela anza kujilipa leo asilimia kumi ya kipato chako.

Unaishi maisha ya mahusiano ya ndoa na uchumba halafu si mwaminifu amka na badilika acha hiyo tabia sasa. Kutokua na uaminifu katika mahusiano ni hatari sana katika maisha ya mahusiano. Familia yako haina upendo wala amani ni wakati sasa wa kuamka na kuibadilisha familia yako iwe sehemu sahihi. Wewe mwenyewe ndio una uamuzi wa kubadilisha chochote kile katika maisha yako kama ukiamua kuamka na kubadilika.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Kuepuka Ili Yasikuharibie Siku Yako Ya Leo

Hatua ya kuchukua leo, rafiki, kuna mambo mengi unatakiwa kuamka na kwenda kubadilisha katika maisha yako hivyo inuka leo na nenda kabadilishe kile ambacho hakipo sawa. Wewe ndio unajijua vizuri ni sehemu gani katika maisha yako haiku sawa. Hivyo leo ni fursa kwako ya kwenda kufanya mabadiliko kwenye maisha yako katika idara zote za maisha yako.

Kwa kuhitimisha, somo letu la leo limetualika sisi sote kuamka na kubadilika katika yale mambo ambayo hayako sawa katika maisha yetu. Kama ulikuwa ni mvivu hata wa kusoma kitu chochote katika maisha yako amka na badilika anza kujijengea tabia ya kujifunza kila siku kwenye maisha yako. Huwezi kufanikiwa bila kujifunza na ukitaka usipige hatua yoyote katika maisha yako endelea kukumbatia na kung’ang’ania ujinga.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.comA

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: