Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukiwa Na Utulivu Wa Akili

Utaweza kufanya makubwa na kutatua changamoto nyingi zinazojitokeza kwako. Hata ukiletewa changamoto ambayo wengine wanaona ngumu wewe unaitatua vizuri sana kwa sababu tu umekuwa na utulivu wa akili. Unapokuwa na utulivu wa akili maana yake uwezo wako wa kufikiri unakuwa juu. Hivyo hata maamuzi unayofanya yanakuwa sahihi kwa sababu hayaongozwi na hisia. Mtu mwenye hisia …

Hizi Hapa Sababu Tatu Kwa Nini Tunathamini Zaidi Tunachomiliki

Ukisoma kitabu cha Predictably Irrational, nguvu zilizojificha ambazo zinatengeneza maamuzi yetu. Mwandishi ametushirikisha sababu tatu kwanini Tunathamini zaidi kile tunachomiliki. Kwanza  tunakuwa  tunakipenda,  ukikaa  na  kitu  kwa  muda  unakuwa  unakipenda  na hivyo  kukipa  thamani zaidi. Pili, tunaangalia  kile  tunachopoteza  kuliko  tunachopata,  hivyo  mtu  anapouza  kitu, anaona  kama  anapoteza  kile  anachomiliki  na  kupenda  na  siyo  kupata  …

Sifa Moja Ya Mtu Aliyestarabika

Huwa hanisumbui na kabisa ba vitu visivyokuwa na maana kwao. Huwa hawahangaiki na sifa za kijinga. Wakifanya kitu kidogo hawataki kujitangaza wala kujulikana kwa kila kwamba wao ndiyo wamefanya. Lakini mtu ambaye hajastarabika anakazana kujitangaza ili kuonekana kwamba amefanya kitu fulani. Watu waliostarabika hawajisifii kwa wengine kwa mali, utajiri au kwa vile ambavyo wao wanavyo …

Sababu Moja Inayosababisha Kutokupata Kile Unachotaka

Watu wengi wana ndoto, wanatamani sana wapate kile wanachotaka lakini kuna kitu kimoja kinawakwamisha. Na kitu hicho ni hawajaamua kupata kile wanachotaka. Sikufichi rafiki yangu, kama hujaamua kupata kile unachotaka, huwezi kupata. Hatua ya kwanza ya kufanikiwa ni kuamua kupata kile unachotaka. Amua kufanikiwa, kama hujaamua kufanikiwa huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako. Watu ambao wameamua …

Ujumbe Mzito Kutoka Kwa Mwanafalsafa Seneca

"I do not know where I shall make progress; but I should prefer to lack success rather than to lack faith" SenecaIkiwa na maana kwamba, sijui kama nitafanikiwa ,lakini ni bora nikose mafanikio kuliko nikose imani. Hii sentensi unapaswa kujiambia kila wakati, kwa sababu itakusukuma kutekeleza wajibu wako na kutokukatishwa tamaa na chochote. Watu wengi …

Hakuna Kitu Kinachowarudisha Watu Nyuma Kama Hiki

Kitu kinachowarudisha watu nyuma ni kuishi maisha ya kuiga. Kama unataka kutoka kwenye changamoto za kifedha ambazo tunazo, tuache kuiga maisha ya wengine. Chagua kuishi maisha yako mwenyewe, kuwa tayari kuchekwa na kuonekana mshamba au wa chini lakini unajua wapi unaenda. Kama utakua tayari kuishi tofauti na wengine wanavyoishi sasa , baadaye utaweza kuishi tofauti …

Tafsiri Ya Mtu Mwenye Roho Nzuri Na Mbaya

Kifupi, hakuna mtu mwenye roho nzuri au mbaya. Mwenye roho nzuri au mbaya anakuja kutokana na tafsiri ambayo wewe unayo juu ya yule mtu. Kwa mfano, kama ukimuomba mtu kitu na akakusaidia utasema ana roho nzuri na akitokea mtu mwingine akienda kumuomba na kumwambia hapana utasema ana roho mbaya. Kumbe basi, roho nzuri au mbaya …

Hii Ndiyo Njia Rahisi Ya Kupokelewa Kokote Unakokwenda

Kama unataka kupokelewa kokote unakokwenda, kila mtu unayekutana naye mpe tabasamu, tabasamu la kweli kabisa kutoka ndani yako. Kuwa na sura ya kisirani inasababisha kujikosesha bahati kwenye kila eneo la maisha yako. Kama una fanya biashara na huna tabasamu funga hiyo biashara yako kwa sababu tabasamu ndiyo linawavuta watu kuja kwako. Ukiona huuzi jaribu kujichunguza …

Sababu Kubwa Kwa Nini Wauzaji Wanashindwa Kuuza

Kutoka kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling, mwandishi Frank Bettger anatushirikisha kwamba sababu kubwa inayopelekea wauzaji wengi kushindwa kuuza ni kuongea sana. Tabia ya kuongea kupitiliza ni chanzo cha wengi kushindwa kuwashawishi wengine kukubaliana nao. Na ubaya wa tabia ya kuongea sana hakuna mtu atakayekuambia kwamba unaongea sana. …

Dunia Huwa Inampisha Mtu Huyu

Dunia inampisha yule ambaye anajua wapi anapokwenda. Kama hujui wapi unapokwenda dunia haiwezi kukupa njia. Ni kawaida katika maisha, pale mtu anapopanga kufanikiwa na kupiga hatua zaidi kwenye yake, ndipo vikwazo vya kila aina vinaibuka. Hii ni njia ya dunia kukupima kama kweli umejitoa kufanikiwa zaidi. Na yule ambaye anaonesha nia, dunia huwa inampisha yule …