Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unataka Matokeo, Fanya Kitu Hiki

Rafiki yangu nikupendaye, Kinachokukwamisha na kushindwa kupata matokeo unayotaka ni kwa sababu moja tu nayo ni sababu unazojipa. Kuna sababu nzuri unazojipa ambazo zinakufanya usichukue hatua. Pale unapokutana na changamoto mbalimbali unajipa sababu ambazo ambazo unaona ni za kweli na zinakufariji. Nikuambie kitu, sababu unazojipa hazitokusaidia kulipa bili wala kubadilisha maisha yako. Na kitakachokusaidia kupata …

Fanya Kilicho Sahihi, Lakini Usitegemee Hiki

Moja ya sababu zinazopelekea wengi kukosa furaha ni kufanya vitu ambavyo wanajua siyo sahihi. Kitu kingine ni watu kufanya kitu huku wakitegemea matokeo fulani yatokee.Kwa mfano, unachukua hatua, ukitegemea matokeo fulani ili uwe na furaha. Hii ni njia ya kujitengenezea kushindwa na kujinyima furaha. Cicero anasema furaha siyo kitu unachokipata kutokana na kupata vitu fulani …

Uko Bize Siku Nzima, Umekamilisha Nini?

Kama huna kitu ambacho unajipima nacho kamwe huwezi kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma. Unaweza ukajikuta bize siku nzima au maisha yako yote lakini ukija kuangalia matokeo hakuna kitu. Changamoto kubwa ya watu kuwa bize ni kwa sababu hawana orodha ya mambo ya kufanya. Unachotakiwa kufanya, kila siku unapoamka kabla hujaanza siku yako weka …

Hatua Ya Kwanza Ya Mafanikio

Ni kuwa mkweli kwanza kwako mwenyewe. Kitu kikubwa kinachokuzuia usifanikiwe ni kujidanganya. Wewe mwenyewe unajua wazi kabisa unapaswa kufanya nini lakini unajidanganya kwa sababu nzuri. Katika maisha watu huwa wana sababu nzuri za kufanya kitu na sababu za kweli. Sababu nzuri ni zile za kujifariji kwa mfano, mtu anasema sijafanya kitu fulani kwa sababu nilikuwa …

Hiyo Hela Tuma Kwenye Namba Hii

Matapeli ni watu wazuri sana kwenye mauzo. Wanapotuma meseji kila siku kwa watu elfu moja wanajua wazi kabisa hawawezi kukosa wateja ambao wanaenda kutuma hela na wakafanikiwa kuwapata. Ndiyo maana watu wakipata ujumbe wa matapeli kwenye simu zao wengine huwa waingia laini, wananaswa. Kwa sababu gani? Wanajua ni kanuni ya asili kwamba, katika watu wengi …

Njia Za Kuongeza Thamani Ya Maisha Ya Wateja Wako

Wateja wako wanapokaa na wewe kwa muda mrefu ndivyo unavyonufaika zaidi. Ili ukae na mteja muda mrefu unatakiwa uendelee kumfuatilia mpaka pale atakapokufa. Na hata pale atakapokufa bado unaweza kuwafuatilia wale watu wake wa karibu na kuwafanya kuwa wateja wako. Unahitaji kuweka juhudi kuhakikisha wateja wanabaki na wewe muda mrefu. Yafuatayo ni mambo muhimu ya …

Acha Ujuaji

Watu wengi wanajikuta wao ni wajuaji lakini bado wanafanya ujinga. Ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti. Watu wanajikuta wao ni wajuaji kwenye biashara, mahusiano, kazi na kadhalika. Wanajikuta wajuaji lakini bado hawana matokeo mazuri. Ujuaji una wamaliza watu wengi kwa kutokujisumbua kujifunza. Watu tayari wanajiona wanajua …

Kama Unataka Bahati Amini Kwenye Hili

Kama unataka bahati kwenye maisha yako, amini kwenye mchakato sahihi. Utapata matokeo pale utakapokaa kwenye mchakato. Unaweza kujiona una nuksi lakini ukweli ni kwamba wewe huna nuksi, tatizo lako ni kwamba hutaki kukaa kwenye mchakato sahihi ili ukutane na bahati yako. Bahati zipo, ila bahati inataka ikukute ukiwa unafanya kitu yaani ukiwa umekaa kwenye mchakato. …

Watu Wengi Huwa Hawafanyi Hivi

Watu wengi wanapopitia changamoto au kufikia katika hali fulani ya mkwamo huwa wanafanya kosa moja ambalo ni kushindwa kukaa chini na kujitafakari. Huwezi kujua kujua kama wapi umekosea au wapi umepatia kama hutengi muda wa kujitafakari. Kama unapitia hali yoyote ambayo siyo ya kawaida kwako, hakikisha unapata muda wa kujisikiliza wewe mwenyewe. Katika hali hiyo …

Lazima Upitie Maumivu Kati Ya Haya Mawili

Maisha ni maumivu, huwezi kukwepa hata siku moja. Kila mmoja anapitia maumivu yake. Jim anatuambia; “We must all suffer one of two things: the pain of discipline or the pain of regret.”Akimaanisha kila mmoja wetu lazima ataumia na kimoja kati ya hivi viwili;maumivu ya nidhamu au maumivu ya majuto. Iko hivi, ili kupata chochote kwenye …