Design a site like this with WordPress.com
Get started

Nyumba Usiyolala Hujui Hila Yake

Ukiwa nyumbani kwako ukiziangalia nyasi za jirani yako kwa mbali unaona za kijani kweli, unavutiwa nazo na kuziona za kwako siyo za kijani kama za jirani yako, ila ukizisogelea karibu unaona siyo za kijani kama ulivyoziona na ukiziangalia za kwako wakati uko kwa jirani unaona tena nyasi zako ni nzuri. Hapa tunapata somo gani? Tunapata …

Funga Hiyo Biashara

Kama una biashara na una msaidizi au wasaidizi ambao wanakusumbua lakini  unashindwa kuwafukuza, funga hiyo biashara. Ukiona mtoto au msaidizi wako anakupanda kichwani hataki kutii mamlaka basi hapo jua huna mtoto wala msaidizi. Kama mmiliki wa biashara unatakiwa kua na maamuzi magumu dhidi ya biashara yako. Umeajiri ndugu au watu wako wa karibu halafu wanafanya …

Bila Maumivu Mteja Hawezi Kununua

Siyo tu bila maumivu mteja hawezi kununua bali pia bila maumivu huwezi kuuza. Maumivu aliyonayo mtu ndiyo yanamsukuma kuchukua hatua katika mauzo. Kama mtu hana maumivu hakuna chochote kitakachomshawishi kuchukua hatua kwa mfano, wewe unauza dawa ya kufunga kuharisha na mteja anakuja kwako akiwa anaumwa sana, na wewe umeshajua maumivu ya mteja ni kupata dawa …

Kuwa Polisi Wa Muda Wako

Akitokea mtu anakunyang'anya laki moja yako hutakubali kirahisi, utapambana mpaka dakika ya mwisho. Lakini ikitokea mtu anatumia muda wako vile anavyotaka wala huna wasiwasi utamchekea tu. Watu wanasahau sana thamani ya muda wao kwamba muda ndiyo unawaletea fedha. Kwa mfano, kama thamani ya muda wako kwa saa ni laki moja hivyo kila dakika moja utakua …

Una Maoni Kila Mahali Lakini Huna Maoni Juu Yako

Unatoa maoni kwenye michezo mbalimbali inayoendelea duniani. Unatoa maoni kwenye maisha ya watu wanavyoishi. Unatoa maoni kwenye siasa na nchi kwa ujumla inavyoenda. Kifupi unatoa maoni kila mahali lakini hutoi maoni kwenye maisha yako binafsi. Ukiacha kutoa maoni kwenye kila kitu na kutunza muda huo kwenye kufanya kazi, na kujitathimini binafsi, kwa nini uko hivyo …

Kama Huna Shauku Unakuwa Umekosa Hiki

Shauku ndiyo sifa inayolipa duniani kuliko sifa zote. Kwa chochote kile unachokwenda kukifanya leo, nenda kakifanye kwa shauku na utajenga ushawishi lakini pia kukubalika na kufanikiwa kwenye kile utakachofanya. Mtu ambaye hana shauku anakuwa amekosa ladha. Anakuwa kama chakula kilichokosa chumvi kinakosa ladha. Pata picha unajisikiaje ukila chakula ambacho hakina ladha? Kinakuwaje? Unapokuwa unafanya chochote …

Ila Wanapuuza Tu

Watu wanajua kile wanachopaswa kufanya ila wanapuuza tu ukweli na kujifanya kama vile hawajui. Ni nani asiyejua kuishi maisha yasiyokuwa na maadili ni kitu ambacho siyo sahihi kwa jamii? Watu wanajua wanapaswa kufanya kazi lakini ni wachache wanaofanya kazi na kupata mafanikio. Watu wanajua wanapaswa kuweka akiba kile wanachopata na kukiwekeza lakini ni wangapi wanafanya …

Njia Rahisi Sana Ya Kutokupoteza Muda Wako

Ni kujua thamani ya muda wako. Pata picha kama unajua thamani ya muda wako kwa saa moja ni million moja utalipoteza kwenye mambo ya kijinga? Unatakiwa kukokotoa thamani ya muda wako na kuona muda wako ni fedha na pale unapotumia kwenye mambo ambayo siyo sahihi jisikie vibaya kutumia fedha zako kwa mambo yasiyokuwa muhimu kwako. …

Usijali Wengine Wanakuchukuliaje

Huwa tunajali sana wengine wanatuchukuliaje, ndiyo maana mambo mengi sana tunayofanya ni kuwaridhisha watu na kujionesha kwa wengine. Ikiwa utaweza kuishi maisha yako na kutokujali wengine wanakuchululiaje basi utaweza kuishi maisha bora na uhuru wa kufanya kile unachotaka. Wewe ndiyo mkurugenzi wa maisha yako, unaelewa unatoka wapi, ulipo na kule unakotaka kufika. Hivyo basi, usiogope …

Ukifanya Kazi Matokeo Yaonekane

Kama unafanya kazi, basi matokeo yataonekana kama kweli unafanya kazi wala hayawezi kudanganya. Na kama hufanyi kazi matokeo yataonekana. Kama unafanya kazi halafu matokeo hayaonekani basi jua kuna mahali unakosea. Unatakiwa ukae chini ujitafakari ni wapi unakosea ili basi matokeo yaonekane. Unapofanya kazi, lazima maisha yako yabadilike. Kazi ni rafiki mzuri kwako. Kama huoni matokeo …