Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tafuta Mali Lakini Usisahau Kufanya Kitu Hiki

Tafuta mali lakini pia,Hakikisha unayaishi maisha yako kwa ukamilifu. Usiishi kama  nyuki,  ambaye  anatumia  maisha  yake  yote kutengeneza  asali halafu  hali  yeye  asali  hiyo,  ila  inaliwa  na  wengine. Watu  wamekuwa  wanatoa maisha  yao  yote kutafuta  mali,  ambazo  hawapati hata  muda  wa  kuzitumia  na kuzifurahia,  katika  harakati  hizo  wanakufa  na  kuwaacha  wengine wakitumia hovyo  mali ambazo  …

Usisubiri Mpaka Uwe Tayari

Ukisubiri mpaka kila kitu kiwe vizuri ndiyo uanze, kuna vitu unaweza kupata lakini ni vile vilivyoachwa na wale walioanza kabla ya hata ya kuwa tayari. Kama umeiona fursa ya biashara lakini hujaanza kwa sababu hujawa tayari, utakapokuwa tayari kuanza utapata wateja lakini ni wale ambao waliachwa na wale ambao waliweza kuanza kabla hata hawajawa tayari. …

Jinsi Ya Kuwapenda Watu

Njia bora ya kuwapenda watu na kujenga mahusiano bora ni kuwakubali watu kama walivyo. Bila ya kutaka wabadilike au wawe kama unavyotaka wewe. Lakini, ukishaanza kusema unawapenda watu kwa sababu wako kwa aina fulani na ukishaanza kutaka watu wabadilike na kuwa kama unavyotaka wewe ndiyo uwapende, jua hapo hujawapenda watu. Kamwe haitatokea kila mtu kwenye …

Kama Unataka Matokeo Tofauti

Basi panda juhudi tofauti. Msingi mkuu unaopaswa kuujua kwenye maisha yako ni sheria ya usababishi au sheria ya kupanda na kuvuna. Kila kinachotokea kwenye maisha yako, umekisababisha wewe mwenyewe. Yaani unachoona sasa ni mavuno ya ulichopanda huko nyuma. Kiasili, dunia haina upendeleo. Mafanikio na furaha yako kwenye maisha inategemea misingi ya asili ya dunia. Ukiijua …

Kuishi Kwake Sisi Tumepona

Kuishi kwake Yesu, wakristu wamepona.Kuishi kwake Mtume Mohammed waislamu wamepona. Tunaweza kuwa na orodha ndefu ya watu ambao waliishi na kupitia wao na sisi tumepona. Je, kuishi kwako wewe, watu wanapona? Unatakiwa maisha yako yawe msaada kwa wengine, kupitia maisha yako na yale unayofanya yanakuwa yanawaponya watu. Kufungua kwako biashara, wengine watapona. Kuendelea kukaa na …

Kitu Ambacho Wanandoa Wengi Hawana

Wengi wanaishi kwenye ndoa lakini afya yao ya ndoa siyo nzuri. Hivi nikiuliza vipi afya yako ya ndoa ndani ya miaka 10 au mitano iliyopita utasemaje? Ndoa ni biashara kama zilivyo biashara nyingine kwa sababu kwenye biashara, ikiwa biashara haina mzunguko mzuri yaani afya yake haiko vizuri ni rahisi kuanguka. Kuna vitu vidogo vidogo tu …

Hawa Ndiyo Watu Ambao Hawafanyi Kazi

Watu wanaopenda wanachofanya, huwa hawafanyi kazi. Huwezi kufanikiwa kwenye maisha kama unafanya kazi kwani kazi inachosha, kazi ni mzigo na kila mtu anapenda kukimbia kazi. Kwenye maisha yako, utafanikiwa kama unafanya kile unachopenda kufanya. Unapofanya kile unachopenda kufanya inakuwa siyo kazi tena bali inakuwa maisha yako inakuwa ni burudani. Huwezi kuchoka kufanya kwa sababu ndiyo …

Kwenye Biashara Kama Huna Hiki Huo Ni Umbea

Pata picha wewe ni meneja wa mauzo na unaambiwa onesha namba ya mauzo ya biashara yako halafu unaanza kutoa maelezo ambayo hayana ushahidi huo unakuwa ni umbea. Kama wewe ni meneja wa mauzo, au unafanya biashara au kitu chochote kile tuoneshe ushahidi unafanya. Kama huna ushahidi huo unakuwa ni umbea tu. Ukitaka watu wakuamini kwenye …

Vikwazo  Viwili  Vinavyokuzuia  Kupata Kile Unachotaka

Kwa  haya  yote unayojifunza,  kwamba  unaweza  kupata  chochote unachotaka,  mawazo yako  yanavuta  chochote  unachofikiria,  unaweza  kuhisi ni uongo  kwa  sababu  labda wewe umejaribu  lakini hujapata  ulichokuwa  unataka. Kwa sababu kuna wengine wanapenda kuona matokeo ya haraka, hivyo wakijaribu na kuona hakuna kitu wanaacha kabisa na kukimbilia fursa nyingine. Kama  hivi ndivyo  unavyofikiria, basi  kuna  vitu  …

Kupata Fedha Zaidi, Unahitaji Hivi

Kupata fedha zaidi unahitaji kuwa mkubwa zaidi na siyo bora zaidi. Mtu ambaye kipato chake ni milioni moja kwa mwezi na mtu ambaye kipato chake ni milioni kumi kwa mwezi, unafikiri nani mwenye matatizo zaidi? Kwa haraka au akili ya kawaida utasema ni mwenye kipato cha milioni moja, kwa sababu ni kidogo ukilinganisha na milioni …