Design a site like this with WordPress.com
Get started

Acha Kufanya Mambo Yasiyokuwa Sahihi

Ili uweze kwenda mbele, lazima kwanza uache kufanya mambo yasiyokuwa sahihi. Ukiwa ni mtu wa kufanya kazi na kufanyia kazi yale mambo sahihi tu lazima utafanikiwa. Hufanikiwi, kwa sababu unafanya mambo yasiyokuwa sahihi mengi. Ukifanya mambo sahihi, lazima utapata majibu sahihi. Mambo sahihi yanafanya kazi kama ukiyafanyia kazi. Ukiamua tu kufanya mambo sahihi lazima utapata …

Usiwe Na Wasiwasi Na Mtu Huyu

Usiwe na wasiwasi na nafsi yako mwenyewe. Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni kuwa na wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe. Na ukishakuwa na wasiwasi huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako. Kwa sababu adui mkubwa wa imani ni mashaka. Watu wana wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe kwa sababu walijaribu na kushindwa huko nyuma. Hivyo wanahofia kujaribu tena …

Anza Na Soko

Wafanyabiashara wengi wanakosea kitu kimoja, wanaanza na bidhaa badala ya kuanza na soko. Kabla hujazalisha tafuta kwanza soko la kwenda kuwauzia kile unachozalisha. Unapaswa kutafuta kundi ambalo tayari lina njaa, kisha unaliuzia kundi hilo chakula. Kwa kuwa watu wengi wanakosea kwa kuanza na bidhaa kisha kutafuta soko,wewe anza na soko kisha bidhaa. Ukishakuwa na watu …

Uliwezaje Kuanza Kama Unashindwa Kuacha

Sisi binadamu tunaongozwa na hisia kweli kuliko mantiki. Yaani tunafanya mambo kwa hisia halafu tunakuja kuhalalisha kwa mantiki. Watu huwa wanatoa sababu za kijinga kweli pale wanapokuwa hawataki kufanya jambo fulani. Sababu hazina mashiko kabisa lakini anataka kuhalalisha kile anachotaka kuwa ukweli hata kama si kweli. Watu wanajiingiza kwenye uraibu kama vile wa ulevi, uvutaji …

Usiuze Sifa, Uza Manufaa

Kwenye mauzo, usihangaike sana kutaja sifa za bidhaa zako, jitahidi sana kuuza manufaa ambayo mteja atapata baada ya kununua bidhaa yako. Huwa tunafanya makosa sana kwenye mauzo, unamwambia mteja sifa za bidhaa zako ambazo kiuhalisia sifa hazimsaidii mteja kwa changamoto alizonazo. Mteja atafarijika pale bidhaa yako itakapokwenda kumtatulia changamoto zake. Pale bidhaa itakapokuwa suluhisho la …

Wakati Mwingine Unashindwa Kuuza Kwa Sababu Hii Hapa

Kuna wakati utajiona kama vile una kisirani, huna bahati kwa sababu kila unavyopambana kuuza huuzi. Kuna kosa moja ambalo unafanya na kosa hilo ni kukosa shauku. Shauku ndiyo sifa namba moja inayolipa duniani. Yeyote anayeongea kwa shauku au kufanya kitu chochote kwa shauku anakuwa anauza kile anachofanya. Shauku ni ile hali ya uungu ndani yako, …

Kwenye Maisha Hakuna Kitu Hiki

Kwenye maisha hakuna kitu kinachoitwa ndugu mtazamaji. Bali kwenye maisha tuna ndugu mchezaji. Kama uko hai basi wewe ni ndugu mchezaji. Uko uwanjani na unatakiwa ucheze namba yako na siyo kutazama wenzako wanavyocheza. Pia, una uamuzi wa kuwa bize na maisha yako au kuwa bize na dunia ikuendeshe vile inavyotaka. Ili upate ushindi unapaswa kucheza …

Sina Uhakika Kama Itakufaa Lakini Kama Ungetumia Muda Wako Kufanya Hivi Ungekuwa Mbali Sana Kibiashara

Binadamu wote tuna asili ya uvivu na uzembe. Ili maisha yako yaende vizuri lazima kwanza uzikatae dhambi hizi mbili ambazo ni uzembe na uvivu. Unakuta mtu analalamika hana fedha, mauzo ni madogo kwenye biashara, mshahara ni mdogo lakini hachukui hatua yoyote itakayomwezesha kuwa bora. Kwa wale ambao ni wauzaji, najua hata wewe ni muuzaji kwa …

Njia Inayosababisha Watu Wengi Kutokuchukua Hatua

Iko hivi rafiki yangu nikupendaye, Kadiri unavyotumia  muda  mwingi kufikiria  na  kutafakari jambo,  ndivyo inavyokuwa  vigumu  kwako  kuchukua  hatua. Wewe angalia hata kwako mwenyewe, mambo mengi uliyochukua hatua haraka ndiyo yameleta matokeo lakini yale ambayo unafikiria hujafikia hata kuchukua hatua. Hivyo basi,  jifunze kufikia  maamuzi haraka,  kisha  ukishaamua,  chukua  hatua,  usianze tena  kufikiria  na  kutafakari. …

Hiki Ndiyo Kinasababisha Ukomo Wa Kipato Chako

Kanuni ya mafanikio makubwa inasema hivi, kipato chako ni matokeo ya idadi ya watu unaowahudumia na kwa ubora kiasi gani unawahudumia. Kwa  maneno mengine,  kipato  chako  kinalingana  na  idadi ya  maisha  unayoyagusa. Hii ni kanuni nyingine muhimu  sana  kwenye  mafanikio  yako,  kanuni ambayo  inaondoa ukomo  kwenye  kipato  chako  na  hata  mafanikio  yako.  Unafikiri ni kwa …