Ijue Biashara Yako Kwa Kina

Rafiki yangu nikupendaye, Dunia inaenda kwa kasi, watu wanaofanya kile unachofanya wewe ni wengi. Utafanyaje ili uweze kujitofautisha na wengine? Ili uweze kujitofautisha na wengine unapaswa kuijua biashara kwa kina. Jua kile unachofanya vizuri sana kuliko mtu mwingine yeyote yule. Kuwa na uwezo wa kuilezea biashara yako kwa sekunde 30 na mtu akaelewa unafanya nini. …

Njia Nzuri Ya Kujitofautisha Na Wengine

Rafiki yangu nikupendaye, Ili upige hatua kwenye maisha yako, unapaswa kufanya kitu kimoja ambacho wengine hawakifanyi. Kitu ambacho ukikifanya, utapata matokeo mazuri. Utapata matokeo mazuri kwenye kila eneo la maisha yako. Ni kitu ambacho watu wengi hawako tayari kukifanya licha ya kuwa wanajua kile wanachofanya. Miaka nenda rudi, kama umekuwa huendi mbele, basi unarudi nyuma. …

Adui Mkubwa Anayekuzuia Usifanikiwe

Rafiki yangu nikupendaye, Ili tuweze kufanya, lazima tutake kweli kufanya, lazima tuwe tayari kuweka kila kinachopaswa kuwekwa kwenye mchakato wa kile tunachotaka ndiyo uweze kupata matokeo makubwa na ya tofauti. Adui mkubwa ambaye atakuzuia usiweze kufanya kama ambavyo unapaswa kufanya ni uvivu na kuridhika na matokeo madogo ambayo mtu anakuwa amepata. Ili uweze kupata zaidi …

Kitu Muhimu Kwenye Kila Uwekezaji

Vitu viwili vya kuwekeza vizuri ili kufanikiwa kwenye biashara, ambavyo ni fedha na muda. Lakini pia kuna kitu cha tatu muhimu sana kinachohitajika ili uwekezaji wa vitu hivyo viwili uwe na tija. Kitu hicho ni UVUMILIVU. Uwekezaji ni sawa na kupanda, huwezi kupanda mbegu leo na kesho ukaanza kuvuna. Unahitaji muda wa kupalilia mbegu hizo …

Jinsi Ya Kudbibiti Hisia Zako

Moja ya changamoto kubwa zinazowapelekea wengi kushindwa kwenye maisha ni kuendeshwa na hisia badala ya wao kuendesha hisia zao. Wote tunajua kwamba pale tunaporuhusu hisia zitutawale, tunakuwa tumeondoa kabisa uwezo wetu wa kufikiri. Kwa sababu hisia kali na fikra haviwezi kukaa pamoja. Kupitia falsafa ya ustoa, tunajifunza kwamba hisia ni kitu ambacho tunakitengeneza sisi wenyewe …

Achana Naye Kama Anafanya Maisha Yako Kuwa Magumu

Rafiki yangu nikupendaye, Hakuna kazi ngumu hapa duniani kama kushughulika na watu.Kwa sababu kila mtu huwa ana tabia zake binafsi. Tumekulia makuzi tofauti, kiasi kwamba mpaka upate mtu wa kufanya naye kazi vile unavyotaka wewe ni kazi. Siyo kwamba wazuri hawapo, wazuri wapo. Na habari njema ni kwamba duniani tuko zaidi ya watu bilioni 7, …

Zijue Sababu Kuu Mbili Zinazowafanya Watu Kufanya Kitu

Rafiki yangu nikupendaye, Watu huwa wanapotaka kufanya kitu, huwa wanafanya bila shida. Watu wanapokuwa hawataki kufanya kitu, huwa hawafanyi au utaona tu sababu wanazokupa. Sababu ambazo watu huwa wanakupa pale wanapokuwa hawataki kufanya kitu ni kama vile nikiwa tayari nitakutafuta, siko vizuri kwa sasa. Watu huwa wana sababu nzuri sana pale wanapokuwa hawataki kufanya kitu. …

Faida Za Kuuliza Maswali

Rafiki yangu nikupendaye, Maisha ni mauzo. Kila dakika ya maisha yako, unauza. Hivyo, kwenye mauzo, yule anayeongea sana ndiyo anaishia kushindwa. Ukitaka kutawala mazungumzo na mtu yeyote yule, awe mteja au la tawala mazungumzo kwa njia ya kuuliza maswali. Maswali yana nguvu ya kukusaidia wewe kupata kile unachotaka.Na unapouliza maswali, uliza maswali ya kimkakati. Kuuliza …

Fanikiwa Kwenye Kile Unachotaka Kufanikiwa

Rafiki yangu nikupendaye, Fanikiwa kwenye kile unachotaka kufanikiwa. Inawezekana kabisa, ni wewe tu ndiyo unajizuia kupata kile unachotaka. Ukiamua unafanikiwa. Kama umeshajua kile unachotaka kwenye maisha yako, weka juhudi zaidi ili ukipate. Kinachowasumbua watu ni kwamba hawajajua wanataka nini, kama wewe umeshajua kile unachofanya, basi weka juhudi kukipata. Mwenye nia ya kutaka kitu, huwa hashindwi. …

Kama Bado Hujajipata

Rafiki yangu nikupendaye, Kama bado hujajipata, sema ndiyo kwa kila kitu. Unasema ndiyo kwa sababu unahitaji fursa ya koneksheni mbalimbali ili ujipate. Unasema ndiyo kwa mambo ambayo ni sahihi na yanayokupa mchongo fulani. Kama hujajipata kanuni ni moja tu mtumikie kafiri, upate unachotaka. Lakini kama umeshajipata sema hapana kwa kila kitu. Sema hapa kwa mambo …

Design a site like this with WordPress.com
Get started