Hii Ndiyo Maana Ya Mafanikio

Watu wengi hawana uelewa juu ya mafanikio. Hata wale ambao tunawaona wamefanikiwa kwa nje ni wachache sana ambao wamefanikiwa. Wengi wanapima mafanikio kwa vitu ambavyo mtu anavyo kama vile gari au nyumba. Kifupi tu, kuwa na nyumba au gari siyo mafanikio bali kitu cha kawaida kwa binadamu kuwa nacho. Kwa mfano, wewe unakula kila siku, …

Tabia Inayowashinda Watu Wengi

Ni uaminifu. Watu wameshindwa kuwa waaminifu kwao wenyewe na kwa wengine. Uaminifu ndiyo mtaji unaolipa kwenye kila eneo la maisha yetu. Kuanzia kazi, mahusiano, biashara na nk. Kama kila mmoja angekuwa mwaminifu tu kwenye mambo madogo ambayo anajiwekea kufanya na angeyafanya basi dunia ingekuwa sehemu salama sana. Usiishi kwa kufuata mkumbo wa watu, kama watu …

Hiki Ndicho Unachopaswa Kukilinda Kuliko Vitu Vingine Vyote

Mpaka hapo ulipo tayari kuna sifa ambazo umeshajijengea na unajivunia kuwa nazo kwako wewe mwenyewe na kwa watu wengine. Umetumia muda mrefu kujenga sifa na jina lako. Hivyo basi, unapaswa kulinda sifa ulizojijengea pia ili juhudi zako zisipotee bure. Usikubali kufanya jambo ambalo litakuja kuharibu sifa yako hata siku moja. Shabaha yangu kubwa leo ni …

Ikiwezekana Kaa Mbali Kabisa Na Watu Hawa

Kuna watu ambao kila ukienda kwao na wazo la kufanya kitu cha tofauti, hata kabla hawajakusikiliza unapanga utafanyaje, tayari wanakuwa na jibu kwamba haiwezekani. Kaa mbali na watu ambao wanakuambia haiwezekani. Watu wa haiwezekani hawana maana kwenye hii dunia zaidi ya kuwaaminisha wengine kwamba mambo hayawezekani kumbe yanawezekana. Watu wa haiwezekani, ni watu ambao unapaswa …

Haya Ndiyo Yawe Malengo Yako Ya Kwanza Ya Fedha

Chochote ambacho kinatokea sasa kwenye eneo lako la fedha, ni matokeo ya tabia ambazo umejijengea. Hakuna kinachotokea kama ajali, huwezi kupanda mahindi ukavuna mbaazi. Kila kinachotokea umekisababisha kutokea. Ni kawaida ya watu, wakishakuwa na fedha zinakuwa zinawawasha wanahakikisha kwanza wazitumie ndiyo wajisikie. Ndiyo maana watu wakiwa na hela ni rahisi kutapeliwa au kutumia hovyo kwa …

Changamoto Ya Kukosa Hela Inaanzia Hapa

Ukiona huingizi hela kwenye maisha yako basi changamoto yako ni moja huna unachouza au unauza kidogo. Fedha inapatikana kwa kutoa thamani kubwa kwa wengine na katika kutoa thamani ndiyo tunapata fedha. Kifupi fedha ni mbadilishano wa thamani. Unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako kama utaweza kuuza zaidi. Ukiweza kuuza zaidi utaweza kutatua changamoto …

Usiweke Nukta Weka Koma

Kibinadamu inafikia mahali unachoka na kupelekea hata kukata tamaa ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Inafikia mahali unaweka nukta, unasema sasa basi hapa ndiyo umefikia mwisho. Njia za Mungu siyo zetu, kwenye maisha hakuna kukata tamaa, kikubwa ni kuendelea kukaa kwenye mchakato sahihi. Unaweza ukapoteza kila kitu, ukajiona uko njia panda na ukaweka nukta …

Hakuna Mfanyabiashara Anayeweza Kufanikiwa Kwenye Biashara Yake Bila Kujua Kitu Hiki Hapa

Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa kama haijui vizuri biashara yake kwa undani. Na changamoto ya watu wengi ya kutozijua biashara zao ni kwa sababu ya kushindwa kujifunza kwa vitendo na uzoefu. Hata kama umewaajiri watu wakusaidie kwenye kile unachofanya, hakikisha unakijua wewe mwenyewe vizuri sana na kwa undani. Unakuta hata waajiri wengi wanadanganywa na wafanyakazi wao …

Nawasaidia Lakini Hawana Shukrani

Ukiwa ni mtu wa kutaka kurudishiwa shukrani pale unaposaidia basi utaumia sana kisaikolojia. Waswahili wanasema shukrani ya punda ni mateke. Kazi yako kubwa iwe ni kufanya kazi yako na siyo kusubiri shukrani. Wewe toa bila kuwa na matarajio ya kupokea. Pata picha kuku anavyotimiza wajibu wake wa kutaga na kutoa mayai, ulishawahi kumuona akilalamika hata …

Tahadhari; Usikosee Wito Wako

Kukosea wito wako, ni sawa na mtu anayefanya kazi sana halafu haoni matokeo anayozalisha. Na hakuna kitu kigumu kama kujua wito wako, ukikosea wito ni kama vile umepotea njia. Kitu muhimu ambacho ningependa uondoke nacho hapa leo ni kwamba utafanikiwa zaidi iwapo utafanya kazi au biashara inayoendana na wito uliopo ndani yako. Achana na kufanya …

Create your website with WordPress.com
Get started