Kitu Chochote Unachotegemea Kutoka Kwa Wengine Hakikisha Unakuwa Hiki

Huwa tunaweza kupanga sisi wenyewe lakini tunapangua sisi wenyewe. Tunakuwa tunaweka mipango yetu huku tukiamini kuwa mambo yataenda kama vile tunavyotaka sisi. Tunapoweka malengo yoyote, au kitu chochote ambacho tunahitaji kukikamilisha lakini kinafanywa na wengine jiwekee nafasi ya mambo kutokwenda kama vile unavyotaka wewe. Jiwekee nafasi ya kuangushwa, usijiwekee uhakika kabisa kwamba kile nilichopanga kitaenda …

Huyu Ndiye Mtu Masikini Duniani

Huwa tunafikiria kuwa mtu masikini ni yule ambaye hana fedha mfukoni. Kwanza , umasikini hauanzii mfukoni wa mtu, bali unaanzia kwenye akili. Akili huwa ikilala basi na mwili unalala. Unapotumia akili yako vizuri itakusaidia vizuri. Mtu masikini kuliko wote duniani ni yule ambaye hana maono makubwa. Dunia iko hivi ilivyo leo kwa sababu ya watu …

Haya Ndiyo madhara Ya Kujikata Wewe Mwenyewe

Watu wa nje hawawezi kukukataa isipokuwa wewe mwenyewe ukijikataa kwa ndani. Ukishajikatalia kwa ndani hata nje watu watakuchukulia hivyo hivyo. Mafanikio yoyote yanaanzia ndani yetu, usipokuwa ndani vizuri basi hata nje utakua vibaya. Unakuwa vile unavyoonekana ndani kadiri ya wewe unavyojichukulia. Unaweza kujiona huna maana, kama wewe mwenyewe umejiwekea mtazamo huo. Unaweza kujiona wewe kuwa …

Usishindande Bali Fokasi Katika Mtu Huyu

Kushindana katika mafanikio ni njia rahisi ya kusahau malengo yako na kujiandaa kushindwa. Unaweza ukashindana na mtu ambaye wala hashindani wewe na pia malengo yake na yako hayafanani hata kidogo. Badala ya kushindana na watu, wewe shindana na wewe mwenyewe. Pambana na malengo uliyojiwekea. Angalia vipau mbele vyako na pambana navyo. Katika ushindani wa kibiashara …

Waambie Wengine Changamoto Zako

Hakuna changamoto mpya hapa duniani, kila changamoto unayokutana nayo basi kuna mtu tayari alishaipitia na ana suluhisho nayo. Rai yangu ni kwamba, ukiwa na changamoto usiwe kama bubu kwa kukaa kimya bali jaribu kuongea na wenzako.Unaweza kukiona kitu ni kigumu sana kwako lakini kwa mwenzako ni rahisi sana. Ndiyo maana leo nakusihi sana usikae na …

Hiki ndiyo kitu pekee cha kufanya au kujali pale tu unapopata Mshahara au Fedha

Heri ya mwezi Februari rafiki yangu, Wote tunajua kuwa fedha ni muhimu sana katika maisha yetu, na hilo halina ubishi. Huwa tunafanya kazi kwa shida lakini cha ajabu tunakuja kutumia fedha tuliyoipata kizembe. Cha ajabu ni kwamba, pale tunapopata mshahara, fedha au kipato chochote kile huwa tunafikiria kuwalipa watu wengine na kujisahau sisi wenyewe. Sasa …

Huyu Ndiye Mtu Anayejali Mambo Yako

Iko hivi rafiki yangu,Kama wewe hujali mambo yako basi jua kabisa hata wale wanaokuzunguka hawatajali sana mambo yako. Huwa watu wa nje wanapata picha kutoka ndani yetu kwanza, wakituona sisi ni watu wa namna fulani basi wanatuchukulia kwa namna ambavyo sisi tupo. Watu wakishakusoma watakuchukulia vile unavyotaka wewe.Wakiona wewe ni mtu unayejali mambo yako, kazi …

Kama Wengine Wanakosea Hata Wewe Unakosea

Ni kawaida yetu sisi binadamu kujiona kuwa sisi ndiyo tuna stahili zaidi kuliko wengine. Tunapenda kujiona kuwa sisi hatuna makosa bali watu wengine ndiyo wenye makosa.Pale tunapokosea huwa tunamtafuta mtu wa kumlaumu kwanza. Huwa hatupendi kukubali kuonekana sisi ndiyo tunakosea bali wengine ndiyo wanakosea. Kama wengine wanakosea basi na wewe unakosea pia. Tunatakiwa kukubali makosa …

Kinachowafanya watu Wengi Kutoingia Kwenye Biashara Ni Hiki Hapa

Hapo mwanzoni kulikuwa hakuna ajira bali biashara ndiyo ilikuwepo na itaendelea kuwepo kwa sababu asili ya binadamu ni biashara. Ili tuweze kuwa na kipato cha uhakika na kufikia uhuru wa kifedha tunapaswa kila mmoja wetu kuwa na biashara. Biashara ni njia ya kupata kipato bila kikomo. Hata kama umeajiriwa hakikisha unakuwa na biashara ya pembeni …

Design a site like this with WordPress.com
Get started