Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Sala Bora Duniani Inayopaswa Kusaliwa Na Kila Mtu

Mpendwa rafiki yangu,

Sisi binadamu tumekuwa ni viumbe ambao tumependelewa kuliko viumbe vyote duniani. Ni viumbe ambao wana akili ya kufanya mambo makubwa duniani. Wanaofanya hii dunia iendelee kupendeza ni watu na wanaofanya dunia isipige hatua ni watu. Ukifananisha miaka mia moja ya nyuma dunia ilivyokuwa huwezi ukaifananisha na sasa, hata wale wa zamani wakifufuka na kuona dunia jinsi ilivyo wanaweza wakashangaa na kuhisi labda wamepotea njia.

Tangu enzi na enzi binadamu amekuwa ni mtu wa malalamiko na manung’uniko, hata umfanyie nini binadamu hawezi kukosa cha kuongea hiyo ndiyo asili yetu sisi binadamu. Tumekuwa ni watu wa kuangalia tumekosa nini na siyo kuhesababu baraka zetu.

Sala bora ambayo kila mtu anaalikwa kuisali ni sala ya shukrani. Watu wengi huwa hawashukuru katika maiaha yao, bali wanaishi kulalamika na kuangalia wamekosa nini.

Kukosa kushukuru ni kukosa fadhila. Sala ya kushuru kwa yote ambayo Mungu amekuwezesha kuwa nayo ni jambo la kushukuru sana, kuendelea tu kuwa hai ni jambo la kushukuriu sana.

Sala ya kushukuru ina maajabu makubwa sana katika maisha yetu. Ni sala yenye nguvu sana , unapoanza kuwa mtu wa shukrani ni kama vile unafungua milango ya baraka kwenye maisha yako, utaziona fursa nyingi sana kwenye maisha yako.

Kila mtu ana imani yake, lakini licha ya kuwa na imani hebu wewe kila siku kuwa mtu wa shukrani halafu utaniambia ni namna gani maisha yako yatakavyobadilika. Watu wanatumia muda mwingi kunung’unika na kulalamika kuwa dunia haina usawa, kwamba jinsi walivyo wao ni kwa sababu ya watu fulani ndiyo wamesababisha wao kuwa hivyo wanashikilia mambo ya kale ambayo yanawarudisha nyuma badala ya kuwapeleka mbele.

SOMA; Jambo Muhimu La Kufanya Katika Safari Ya Mafanikio Ili Ujisikie Raha

Kuanzia sasa kuwa mtu shukrani, orodhesha vitu vyote unavyopaswa kushukuru halafu uwe unavisoma kila siku, kwa namna hiyo utakuwa kama sumaku kuvuta vitu vingi kwenye maisha yako. Najua wengi wataishi kusoma tu lakini hawatachukua hatua ya kufanya zoezi hili, unapoandika chini ni kama vile unadownload kitu fulani.

Kuandika kuna nguvu sana, acha kufanya kila kitu kichwani, weka mambo yako kimaandishi na unapoandika ni kama vile unasaini mkataba au unakula kiapo.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa mtu wa shukrani kwenye maisha yako. kuwa mtu wa sala ya kushuru kwa kila jambo, ukiwa ni mtu kushukuru utaona ukuu wa Mungu ndani yako lakini ukikosa kuwa na shukrani utakuwa umejichagulia kukata tamaa na kuona kila kitu kina kasoro kwako.

Kwahiyo, kukosa kushukuru ni kuamua kupoteza yote, unaposhukuru inaamsha hata hamasa ya kuendelea kufanya mambo yako kwa furaha. Lakini unapokaribisha hali ya kutokuwa na shukrani kwenye maisha yako ni kama vile unafungulia bomba la matatizo kwenye maisha yako.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

www.mtaalamu.net/kessydeo

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: