Chagua Moja Kati Ya Hivi

Dunia huwa haina huruma, inamwadhibu mtu kadiri ya uzembe wake na inamlipa mtu kadiri ya thamani yake. Watu wengi wamekuwa wakitumia fedha ambazo hawana kununua vitu ili kuwafurahisha watu wasiojali. Leo ninakuomba kitu kimoja, uchague kuwafurahisha watu uendelee kuwa masikini au ujinyime na kuwa tajiri. Huwezi kutoka katika umasikini bila kuishi tabia za kitajiri. Chagua …

Huyu Ndiye Rafiki Wa Kweli

Kila mtu ana rafiki yake wa karibu lakini licha ya kuwa na rafiki wa karibu bado huyo rafiki anaweza kukuangusha pia. Yuko rafiki wa kweli, ambaye hajui kuangusha watu pale unapokuwa na shida na rafiki huyo siyo mwingine bali ni kazi. Kazi ni rafiki wa kweli kwa sababu anakupa kile unachotaka. Ukifanya kazi, utapata fedha …

Kamwe Usiogope Kuwa Mtu Huyu

Ni wangapi tokea wazaliwe hawajawahi kuishi maisha yao?Je maisha unayoishi sasa ndiyo maisha yako halisi? Kile unachofanyia kazi sasa ndiyo ndoto unayoishi? Wengi wamepotea kwa kutokuishi ndoto na hata maisha yao halisi.Maisha ya watu wengi ni maigizo matupu. Tuko radhi dunia ituone sisi ni watu wanaoenda na fasheni, tukope fedha ambayo hatuna kununua vitu ambavyo …

Epuka Kutumia Lugha Hii Ya Ufundishaji Katika Malezi Ya Watoto

Wanasema watoto ni malezi, je malezi unayowapa watoto wako yanawawezesha kusimama kwa miguu yao wenyewe hapo baadaye? Unawapa misingi au unawalea ili mradi tu?Zawadi nzuri ya kumpatia mtoto ni kumpa malezi bora ambayo hatoweza kuyapata sehemu nyingine yoyote ile. Hata kama mzazi umekosa vitu vyote bado unayo nafasi ya kutoa upendo kwa watoto wako. Na …

Ni Bora Kufa Kwa Kitu Kuliko Kuishi Bure

Ni bora upambane kwa kitu kuliko kutokupambana.Ni bora uwe na kitu cha kusimamia kuliko kuishi bila kuwa na kitu cha kusimamia. Kuwa na misingi michache ambayo itakuongoza kwenye kila eneo la maisha yako. Usiwe kama bendera fuata upepo. Huwezi kuwa na ushawishi kama huna kanuni na msingi. Watu huwa wanavutiwa na watu ambao wanaushawishi tayari …

Kama Unataka Kujinyanyua Juu…

Binadamu hatufanikiwi kwa miujiza, Bali sheria ya asili inafanya kazi yake. Kama alivyowahi kusema Jim Rohn, ukitaka kufanikiwa wasaidie au wawezeshe wengine kwanza kupata kile wanachotaka na wewe utafanikiwa. Ni hivyo tu ,wala hakuna njia ya mkato rafiki yangu. Ukitaka Kujinyanyua Juu wewe mwenyewe, basi anza kuwanyanyua juu watu wengine. Unapowanyanyua wengine nawe unanyanyuka. Unapomsaidia …

Hii Ndiyo Faida Ya Jawabu La Upole Kwa Mtu Ambaye Ana Hasira

Mpendwa rafiki yangu, Sisi binadamu tunayo mamlaka ya kudhibiti hisia zetu lakini hatuwezi kuzuia tusiwe na hisia. Unaweza kudhibiti hasira lakini huwezi kuzuia usiwe na hasira. Kwa mfano, kitu chochote cha hasira kikitokea unaweza kujidhibiti kutochukua hatua pale unapokuwa na hasira ambayo inaweza kuleta madhara. Leo tunakwenda kujifunza jawabu la upole linavyoleta mafanikio katika maisha …

Hiki Ndiyo Kitu Pekee Ambacho Teknolojia Hakizalishi

Tunashukuru kwa uwepo wa Teknolojia duniani. Ni msaada mkubwa sana miongoni mwetu, hili halihitaji sababu nyingi kuthibitisha hilo. Teknolojia inawasaidia watu wengi kuwa matajiri katika zama hizi. Watu wanatengeneza koneksheni mbalimbali kupitia teknolojia ambayo tunaitumia leo hii katika maisha yetu. Dalai Lama aliwahi kunukuliwa akisema, ninafikiri kweli teknolojia imeongeza uwezo wa binadamu. Lakini, teknolojia haiwezi …

Mafanikio Yoyote Yale Kamwe Hayaji Kwa Njia Hii

Kwa asili tu hakuna kitu kinachotokea kwa njia rahisi, asili huwa haifanyi kazi kwa njia za miujiza ya haraka hata siku moja. Kwa mfano, ulishawahi kuona mwembe umepandwa leo na leo uzae? Vipi sisi binadamu tunafanya kazi leo na tunataka mafanikio ya haraka? Asili ndiyo inaleta mafanikio ya kweli na ya uhakika. Hakuna mafanikio yanayokuja …

Usiweke Mayai Yote Kwenye Kapu Moja

Ni usemi maarufu sana katika uwekezaji.Ukiwa na maana kwamba usiwekeze katika eneo moja. Unatakiwa kutawanya uwekezaji wako katika maeneo tofauti tofauti. Inapotokea hatari ya uwekezaji, labda umewekeza kwenye eneo moja utapata hasara sana lakini kama utakua umewekeza maeneo tofauti haiwezi kukuletea shida, haiwezekani maeneo au sekta zote ulizowekeza zikaanguka zote kwa mara moja. Kama uwekezaji …

Design a site like this with WordPress.com
Get started