Jinsi Ya Kujifunza Unyenyekevu

Asili huwa ina kawaida ya kuwanyang'anya wale wote ambao wana majivuno kwenye kile wanachofanya. Majivuno yanatuharibia vitu vingi sana kwenye maisha yetu ya kila siku.Tunapoteza vile tulivyokuwa navyo kwa sababu ya kukosa unyenyekevu. Tunajiona kuwa sisi ndiyo kila kitu kwa kila kitu na wengine hawana maana kwetu. Ili tuweze kuwa na maisha ya unyenyekevu ambayo …

Usitumie Tu Fedha Kwa Sababu Una Fedha

Wengi wanajikuta wanatumia fedha kwa sababu wana fedha. Hawa ni wale ambao hawawezi kujizuia au kusema hapana pale wanapokutana na kitu halafu wana hela ya kununua. Kama hakuna ulazima sana wa kitu unachotaka kufanya siyo lazima kutumia fedha linda fedha yako. Usiwe wakala wa fedha zako mwenyewe yaani wewe unakua ni mpokeaji tu baada ya …

Fanya Kinachowezekana Halafu Kisichowezekana Mwachie Huyu

Fanya mambo ya kawaida yaani yale ambayo yako ndani ya uwezo wako halafu mambo makubwa ambayo yako nje ya uwezo wako mwachie Mungu atafanya. Huwa tunajisumbua kupambana na kila kitu, ndiyo maana tunajikuta tuna kazi sana. Kwa mfano, tukimchukulia Musa kwenye kitabu cha Biblia yeye alikuwa na fimbo tu ya kawaida iliyokuwa mkononi mwake alifanya …

Kama Unaishi Kwenye Karne Ya 21 Usiache Kujifunza Kitu Hiki Hapa

Kuna kitu ambacho watu wengi wanapuuzia bila kujua ni kitu muhimu kwa kila mtu. Kama uko hai na unaishi kwenye karne 21 basi unapaswa kujifunza kitu hiki kimoja ambacho tunakwenda kujifunza leo. Unatakiwa ujifunze kuuza. Jifunze namna ya kuuza kwenye kile unachofanya kwa mfano, kama wewe ni mwalimu jifunze kuuza ualimu wako, kama wewe daktari …

Haziwezi Kukusaidia Kamwe

Ni rahisi kuwadanganya watu kwa maneno lakini matokeo na matendo yanakuumbua. Tumekuwa ni watu tunaofanya kazi kwa mdomo na kujielezea sana kile tunachofanya badala ya kuweka kazi na kazi zetu zitutangaze. Nikuambie ukweli rafiki yangu, sababu hazitoweza kukusaidia hata siku moja. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa kwenye eneo lolote lile la maisha kwa njia ya sababu. …

Hili Ndiyo Eneo Gumu Kwako Kufanikiwa

Watu wanaofanya vizuri kwenye vile wanavyofanya ni wale wanaopenda vile wanavyovifanya. Ni rahisi kufanikiwa kwenye mchezo uliochagua kucheza kama unaupenda mchezo huo. Angalia wanaofanya vizuri kwenye michezo mingi ni wale wanaoupenda huo mchezo na muda wao mwingi wanautumia kujifunza huo mchezo wanaoupenda. Eneo gumu kwako kufanikiwa ni lile eneo unalolichukia. Huwezi kufanikiwa kwenye kile unachokichukia. …

Hii Ndiyo Habari Ya Kuifuatilia Leo

Kila siku umekuwa unasikiliza, unaangalia habari mbalimbali lakini leo nakusihi uende ukafuatilie habari unayokwenda kuijua leo na kuacha na habari nyingine. Hivi tokea uanze kufuatilia habari imekusaidia kuingiza kipato? Kama unaingiza kipato kupitia habari endelea maana ni kazi yako lakini kama huna unachopata zaidi ya kupoteza wakati, nguvu na fedha zako ni bora uzitumie leo …

Nguvu Za Ajabu Zinapatikana Kwa Njia Hii

Binadamu tunayo nguvu ya kufanya vitu vya kushangaza sana lakini hii nguvu tuliyonayo ndani yetu huwa hata hatuitumii vile ipasavyo. Ili uweze kutumia nguvu za ajabu zilipo ndani yako unapaswa kuwa na kitu hiki kimoja ambacho ukiwa nacho utafanya yasiyowezekana hata kama watu wanaona hayawezekani. Tunaweza kuwa na nguvu ya ajabu ndani yetu kama tukiwa …

Jinsi Ya Kutokichosha Kichwa Chako Kufanya Kazi

Vichwa vyetu vina mambo mengi kwani karibu kila kitu huwa tuanza na kufikiri kwanza kwa kichwa.Hebu fikiria tokea umezaliwa mpaka leo huoni kama kichwa chako kinabeba mambo mengi sana?Vipi kama leo ukiamua kukisaida baadhi ya mambo? Nafikiri kitapumua kama siyo kupumzika. Kisaidie kichwa chako kutokuchoka kufanya kazi maana kichwa chako kina mambo mengi hivyo kisaidie. …

Huyu Ndiye Mtu Ambaye Hawezi Kufukuzwa Kazi

Kwa kutumia akili ya kawaida wewe unafikiri mtu ambaye hawezi kufukuzwa kazi ni mtu wa namna gani? Mtu ambaye hawezi kufukuzwa kazi ni yule mtu ambaye ana thamani. Kama mtu anazalisha na kukupa faida huwezi kumfukuza kazi lakini kama hana thamani anayozalisha lazima utamuondoa. Unalipwa kadiri ya thamani unayoitoa sokoni. Kwa mfano, mchezaji mpira mwenye …

Design a site like this with WordPress.com
Get started