Ni wakati wa kujitathimini wewe mwenyewe. Je, familia yako inanufaikaje na wewe? Unatumika katika familia kama chombo cha kuleta amani au mafarakano? Kama familia yako haifurahii uwepo wako tafadhali, tafakari mwenendo wako na jibadilishe. Tumika kuleta mafanikio katika familia yako na familia yako itakuwa takatifu na inayompendeza Mungu. Tumia uwezo wako ulio nao kuifanya familia …
Bure Ina Gharama, Lipia Bili Zako
Kila unapoambiwa bure jua kuna gharama ambayo huioni kwa macho. Mpaka mtu anakuambia ni bure jua kuna manufaa ambayo yeye anayapata. Pendelea kuwa mtu wa kulipia gharama kwa sababu hakuna kitu cha bure duniani. Kila mtu anatumia rasilimali zake kufanya kitu fulani. Bure pia inatuzia kupata kile tunachotaka. Ukiamua kununua kitu unachopenda nenda kanunue usiyumbishwe …
Hakikisha Unakuwa Na Kitu Hiki Kama Unataka Kupiga Hatua
Aliyekuwa baba wa falsafa, mwanafalsafa Socrates aliwahi kunukuliwa akisema, maisha ambayo hayatathiminiwi ni maisha ambayo hayana maana kuishi. Kumbe basi, kama wewe unaishi halafu hujitathimini huwezi kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma. Kwenye kila kitu unachofanya lazima uwe na kitu cha kujipima. Kama kile ulichopanga kufanya unapata matokeo unayotaka au la. Kama unataka kupiga …
Continue reading "Hakikisha Unakuwa Na Kitu Hiki Kama Unataka Kupiga Hatua"
Utakimbilia Kwa Nani Ukipatwa Na Kitu Hiki?
Pale unapopatwa na changamoto fulani huwa unamkimbilia nani? Mwingine akipata changamoto ya ndoa labda mke au mume anamsumbua, anachofanya anaungana na wanawake au wanaume wengine ambao nao wanachangamoto kama yake. Watu wanafikiri wakipata shida wanatakiwa kuungana na watu wenye shida kama wao hilo ni kosa. Huwezi kutoka kwenye changamoto kwa kutafuta faraja na huruma au …
Continue reading "Utakimbilia Kwa Nani Ukipatwa Na Kitu Hiki?"
Fanya Mambo Haya Muhimu Kama Unataka Kuaminiwa
Kila mmoja wetu ni rasilimali muhimu katika kufanikisha malengo yake na ya mwingine. Kifupi, kila mmoja anamtegemea mwenzake hivyo basi kujitegemea siyo kujitosheleza. Watu huwa wanatujua sisi vizuri kwa sababu ya tabia zetu. Tabia zetu ndiyo zinatupa sisi nafasi ya kuaminiwa katika kitengo fulani. Ukweli ni kwamba, ukitaka kuaminiwa kubeba chakula, onesha sura iliyoshiba; kwa …
Continue reading "Fanya Mambo Haya Muhimu Kama Unataka Kuaminiwa"
Jinsi Ya Kumiliki Machaguo Yako
Watu wengi wanapenda kumiliki mawazo yao, kumiliki kile wanachotaka yaani kifupi watu wanapenda kuongea lugha zao wenyewe. Ndiyo maana nilisukumwa kuandika kitabu cha Ongea Lugha Yako, Sauti yako ya Ndani ndiyo mafanikio yako. Watu wanashindwa kuwa vile wanavyotaka kuwa kwa sababu ya kushindwa kusikiliza sauti zao za ndani na kuongea lugha zao wenyewe. Unakuta mtu …
Jinsi Ya Kulinda Muda Wako
Muda ndiyo mteja namba moja kwa chochote kile unachotaka kufanya kwenye maisha yako. Unapokuwa na muda utaweza kufanikiwa kufanya vitu vingi sana. Zama tunazoishi ni zama za mitandao ya kijamii. Kama usipokuwa makini utajikuta muda wako wote unatumika kuzurura kwenye mitandao ya kijamii kujua nini kinaendelea. Wako wengine wanasema hawataki kupitwa na habari yoyote ile …
Huu Ndiyo Utumwa Wa Kazi
Utaona kazi ni mbaya pale utakapokuwa siyo mtu wa kutimiza majukumu yako kwa wakati. Siyo tu kwa wakati, bali kwa kukumbushwa kila kitu. Waswahili wanasema, hiyari ya shinda utumwa. Ukiwa mtu wa kutimiza majukumu yako bila kuambiwa hutamwona mtu mbaya lakini ukisubiri kukumbushwa majukumu yako utajihisi kama unaonewa. Cheza namba yako. Ukikabidhiwa jezi nenda kacheze …
Siku Huwa Hazifanani
Kila siku huwa inakuja na mambo yake. Matokeo uliyopata jana huenda leo usiyapate. Hakuna anayeweza kutabiri kesho itakuwaje bali wote huwa tunaishi kwa matumaini tu. Mbinu uliyotumia jana huenda leo isikupe matokeo kama yale ya jana. Hivyo usiishi kwa mazoea. Kwa sababu siku hazigandi zinasogea kila siku. Kila siku unayoipata kwako iwe ni siku ya …
Kitu Cha Kuepuka Kufanya Pale Unapokutana Na Changamoto
Kila mmoja wetu ni rahisi kutoa ushauri kwa wengine pale wanapokutana na changamoto. Lakini ushauri huo huo anaotoa kwa wengine anashindwa kuutumia yeye mwenyewe akiwa na changamoto. Kitu cha kuepuka pale unapokutana na changamoto ni kwamba, usitaharuki. Unapotaharuki unakuwa unajivuruga wewe mwenyewe. Ukitaharuki siyo kwamba utajivuruga wewe mwenyewe, bali pia utawavuruga na wengine pia. Ukikutana …
Continue reading "Kitu Cha Kuepuka Kufanya Pale Unapokutana Na Changamoto"