Mpendwa rafiki yangu, Ukurasa wa sita wa kitabu hiki ambacho utakwenda kukisoma utakutana na kiapo cha siku yako yaani positive declaration Hiki ni kiapo ambacho kitakusaidia kuinza siku yako kwa ushindi mkubwa. Maana kuna nguvu kubwa sana ya kuapa wewe hushangai kwanini watu huwa wanaapa wakati wa kuweka nadhiri, ndoa, kazi n.k? Unapoapa unakuwa unajiunganisha …
Haya Ndiyo Mapambano Ambayo Hutakiwi Kupigania
Rafiki, Siyo kila mapambano yana faida kwako. Siyo kila mapambano yanakuja kwako unatakiwa kuyapigania. Kabla hujaingia kwenye pambano lolote lile, jiulize je haya mapambano yana faida kwangu? Kwa mfano, unaingia kwenye pambano na kupigana eti kwa sababu kuna mtu hajakusalimia, au umemsalimia hajaitikia. Unaanza kujiambia kuwa fulani anajisikia ndiyo maana hajaitikia salamu yangu au ndiyo …
Continue reading "Haya Ndiyo Mapambano Ambayo Hutakiwi Kupigania"
Je Unajua Ushindi Huwa Unaanza Na Kuanza? (Utaratibu Wa Kupata Kitabu Cha Kwa Nini Umezaliwa Kushinda)
Huwezi kupata ushindi wowote katika maisha yako kama hujaanza kufanya kile unachotaka. Unapochukua hatua ya kwanza kwenye kitu chochote kile ni kama kuondoa laana. Kumekuwa na laana ya watu wengi kwenye eneo la kuanza. Ukitaka kupata kile unachotaka, anza kwanza kukifanyia kazi. Unapoanza usiangalie matokeo gani utapata, wewe chukua hatua ambacho ndiyo kitu kilichopo ndani …
Huu Ndiyo Wasifu Mzuri Unaopaswa Kuuacha Duniani (CV)
Kitu pekee ambacho unatakiwa kufanya hapa duniani kabla hujafa ni kurefusha CV au wasifu wako. Kuna wasifu mwingine ni wa kibinafsi sana hauwezi kusomwa mbele ya watu. Wasifu wa kibinafsi huwa unagusa maisha yako tu na familia yako. Hebu jiulize miaka 50 ijayo utaitwa mzee nani? Dunia itajivunia nini kutoka kwako? Nyumba nzuri uliyojenga, au …
Continue reading "Huu Ndiyo Wasifu Mzuri Unaopaswa Kuuacha Duniani (CV)"
Ukitaka Kuwaelewa Wengine Fanya Hivi
Jaribu kuvaa viatu vyao na kutembea kwenye viatu hivyo. Unaweza ukawa unamlaumu mtu au unamhukumu mtu lakini ukivaa viatu vyake na kutembea kwenye viatu hivyo ndiyo utajua kile anachosema ni nini. Kifupi, jiweke kwenye nafasi ya wengine na fikiri na kufanya kwa namna wanavyofanya wao utawaelewa vizuri kwa nini wanafanya kile wanachofanya. Kuna wengine kile …
Kabla Hujaanza Mambo Makubwa Hakikisha Unafanya Mambo Haya Muhimu
Mtu akifunga kula iwe ni kwaresma, mwezi wa ramadhani au siku yoyote ile ambayo amejipangia kufunga kwa sababu zake za kiroho pale anapofungua mfungo wake huwa haanzi kwa kula ugali mgumu. Ila ataanza kunywa vitu vya moto kama vile uji au chai kwa ajili ya kufungua tumbo. Kwanini sasa mtu amekaa na njaa muda wote …
Continue reading "Kabla Hujaanza Mambo Makubwa Hakikisha Unafanya Mambo Haya Muhimu"
Usiingie Kwenye Mtego Huu
"Chukua tu halafu utanilipa mwisho wa mwezi"Ni mtego mbaya ambao watu wengi huwa wanaingia. Usitumie fedha ambayo hujaipata kununulia vitu. Maana unatengeneza shida kubwa. Usikubali mtu akuambie chukua halafu utalipa mwisho wa mwezi. Unatengeneza deni kubwa ambalo linakuja kukutesa hapo baadaye katika ulipaji. Kutumia fedha ambayo hujaipata kwa lugha rahisi ni kukopa. Ushauri mzuri wa …
Tawala Kile Ulichonacho
Ukishindwa kutawala kile ulichonacho utashindwa maeneo mengi ya maisha yako. Itawale nafasi nzuri uliyonayo wewe kama baba, mama au mtoto katika familia yako. Kushindwa kutawala nafasi yako ni dalili ya kushindwa kutimiza wajibu wako. Tawala mawazo yako. Una mawazo mengi mazuri unayopata kila siku lakini unashindwa kuyatawala na kuyaweka kwenye vitendo. Tawala akili yako kwa …
Ukishindwa Kwenye Kitu Hiki Wewe ni Mzembe
Kuna maeneo ambayo ukishindwa dunia haitakulaumu lakini kuna maeneo ambayo ukishindwa kufanya kile unachopaswa kufanya dunia lazima itakulaumu. Dunia itakulaumu pale wewe utakaposhindwa kwenye kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako. Kwa mfano, kitu chochote ambacho kipo ndani ya uwezo wako ukikishindwa utaonekana ni mzembe. Kuwa na uzito uliopitiliza ni uzembe wa mtu mwenyewe kwa …
Continue reading "Ukishindwa Kwenye Kitu Hiki Wewe ni Mzembe"
Jiwekee Ukomo Kwenye Vitu Hivi
Kwenye vitu ambavyo utajihusisha navyo. Kufanikiwa siyo kufanya kila kitu kama wengi wanavyodhani. Huhitaji kufanya kila kitu ndiyo ufanikiwe, bali unahitaji kufanya machache kwa ubora. Jua ni maeneo gani uko vizuri na weka nguvu zako zote huko ambako uko vizuri na siyo kufanya kila kitu. Mengine achana nayo, wewe weka kazi kwenye yale ambayo yana …