Habari za leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na huku ukimalizia mwisho wa juma vizuri. Hongera sana kwa zawadi ya siku hii ya leo uliyoweza kuipata natumaini utakua umeitumia vema.

Leo mwisho wa juma hili pangilia mambo yako ambayo utakwenda kuyatekeleza kuanzia juma jipya linaloanza kesho. Pia leo jaribu kujipa muda wewe mwenyewe kwani unawapa watu wengine muda wako lakini unajisahu wewe mwenyewe. Leo ongea na wewe tafuta sehemu tulivu isiyokuwa na bugdha unakuwa wewe kama wewe hata simu yako weka pembeni ili upate utulivu wa akili na anza kuongea na wewe na msikilize wewe anakuambiaje.
Mpendwa rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ambapo leo tutakwenda kujifunza wimbo wa hamasa utakao kuhamasisha kufanya kazi unayoifanya. Hivyo basi, nakusihi sana uweze kuambatana na mimi hadi mwisho wa somo letu ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Je uko tayari kuufahamu wimbo huo? Basi karibu rafiki ili uweze kuufahamu wimbo huo.
SOMA; Ufahamu Wimbo Bora Unaopendwa Na Watu Wengi Duniani
Rafiki, katika maisha yetu tunapitia changamoto za kila aina na ili tuendelee kufanya yale tunayoyafanya tunahitaji hamasa kila siku ya kutuwezesha kwenda mbele zaidi bila kukata tamaa. Ndio maana leo napenda kukushirikisha wimbo wa hamasa utakaokuwa unakuhamasisha kufanya kile unachokifanya hata kama umepigwa na mawimbi kiasi gani.
Mpendwa msomaji, wimbo wa hamasa utakao kuhamasisha katika kazi unayoifanya licha ya kupitia changamoto ni kufanya kazi unayoipenda au kufanya kitu unachokipenda. Kwa mfano, mimi Deogratius Kessy nimejichangulia falsafa ya kuandika kila siku katika maisha yangu kwa sababu ninapenda ndio maana sioni kazi yoyote. Naandika bila sababu na hii imenijenga mfumo mzuri katika maisha yangu.
Kwahiyo, mpendwa msomaji, nikikupa kazi ya kuandika kila siku kwako utaona ni mzigo mkubwa lakini kwangu naona siyo mzigo kwa sababu naipenda. Hivyo basi, hata wewe nakusihi sana ufanye kitu unachokipenda kwani ndio mwimbo wa hamasa utakaokuhamasisha kufanya kile unachokifanya kwa ushindi kila siku.
Mwanafalsafa confuncius anatualikwa mimi na wewe kuweza kufanya au kuchagua kazi tunazozipenda na hatutoona mzigo katika kazi tunazofanya. Kufanya kazi usiyopenda hakika ni mzigo mkubwa unaopaswa kuutua sasa.
SOMA; Moto Wa Hamasa Utakaokuwezesha Kupata Nafasi Ya Kazi Sehemu Yoyote Duniani
Hatua ya kuchukua leo, kufanya kazi usiyoipenda ni mzigo hivyo basi, chagua kufanya kazi unayoipenda kwani ndio wimbo wako utakuwa unakuhamasisha kufanya kazi kukuletea matokeo makubwa hatimaye kuishi maisha ya furaha na mfanikio.
Kwa kuhitimisha, ili tuweze kufanikiwa na kuwa na maisha ya furaha basi ni muhimu kusikiliza sauti zetu za ndani zinataka nini. Sikiliza sauti yako ya ndani na itakujulisha kazi unayoipenda kutoka moyoni. Kufanya kazi usiyoipenda itakufanya kuwa mlalamikaji na hatimaye utakuwa unazalisha haba.
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com