Pampu Mpaka Maji Yatoke
Ukiwa kwenye kisima cha kupampu, ukipampu mara moja maji hayawezi kuja juu, ila ukipampu mara nyingi maji yatakuja juu. Na ukipampu na kuishia njiani bila kuona maji kama yale maji yalikuwa karibu kutoka yote yatarudi chini. Ukija kuanza tena utaanza upya. Katika maisha unapaswa kuwa na msimamo. Uwe na nguvu ya ung'ang'anizi. Kuwa na ung'ang'anizi …
Ukitaka Kuwaelewa Watu Jinsi Walivyo
Sababu Kuu Moja Kwa Nini Umchukulie Kila Mtu Kwa Heshima
Sisi ni binadamu na maisha yetu kwa asilimia kubwa yanawategemea wengine. Kile ambayo tunahangaika kukitafuta tayari kipo kwa wengine. Mafanikio yote tunayotaka tunapata kwa watu wengine. Hivyo basi watu ni rasilimali muhimu sana.Mchukulie kila mtu unayekutana naye kwa adabu na heshima kwa sababu huwezi kujua ni wakati gani utamwitaji sana kwenye maisha yako. Kila mtu …
Continue reading "Sababu Kuu Moja Kwa Nini Umchukulie Kila Mtu Kwa Heshima"
Uza Matumaini kuliko Laana
Huu Ndiyo Msingi Mkuu Wa Kupata Fedha Duniani
Unaweza kumuona mwenzako anapiga hela eneo fulani na wewe ukaiga ukaenda kufanya huenda hata usipate kama anavyopata yeye. Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini katika timu ya mpira au hata makazini watu wanalipwa tofauti?Wote mnafanya kitu kimoja lakini kila mtu analipwa fedha tofauti? Fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu hilo halina kabisa ubishi. Ni jawabu …
Continue reading "Huu Ndiyo Msingi Mkuu Wa Kupata Fedha Duniani"
Kushindwa Kitu Ambacho Kipo Ndani Ya Uwezo Wako
Huo ni uzembe mkubwa. Usikubali kushindwa kwa kitu ambacho tayari unao uwezo wa kila namna kukishinda.. Unapopata nafasi yoyote ile, itumie vizuri kwa sababu usipoitumia nafasi ambayo iko ndani ya uwezo wako baadae itakuja kukutesa sana kisaikolojia. Utaanza kujilaumu laiti ningelijua, usikubali upitie maumivu ya laiti ningelijua kwa ni fedheha kubwa kwako. Kama unaweza kushinda, …
Continue reading "Kushindwa Kitu Ambacho Kipo Ndani Ya Uwezo Wako"
Amini Hata Kama Huoni
Utajiri Muhimu Utakaobaki Na Wewe Mpaka Mwisho
Ni utajiri wa familia na marafiki. Pale mwili na roho yako inapotaka kujitenganisha hutatamani kupata muda wa kufanya kazi zaidi kwenye kile unachofanya au biashara unayofanya. Lakini, utatamani sana kama ungepata muda zaidi wa kuwa na wale watu wako wa karibu unaowapenda. Kwa sababu kila mmoja wetu ametokea katika familia na ataondokea katika familia. Ni …
Continue reading "Utajiri Muhimu Utakaobaki Na Wewe Mpaka Mwisho"
Mambo Matatu Ya Kufanya Dhidi Ya Mshindani Wako Kibiashara
Katika ushindani wa kibiashara, usipokuwa makini utajikuta na wewe unakimbia mbio za panya na hata ukishinda utabaki kuwa panya. Kwenye ushindani wa kibiashara fanya kile ambacho mshindani wako hafanyi. Hii ndiyo njia bora kabisa ya kushindana kwa sababu haitokuumiza, badala ya kuwa kama yeye, wewe unakomaa kuwa kama wewe. Unakuwa bora sana kwenye kile unachofanya …
Continue reading "Mambo Matatu Ya Kufanya Dhidi Ya Mshindani Wako Kibiashara"