Bila Ufunguo Huwezi Kufungua Mlango

Pata picha kwamba unaamka asubuhi mtu wako wa karibu anakupa zawadi ya gari, anakukabidhi gari lakini hakupi ufunguo wa gari, je utaweza kuliendesha? Ni ngumu hutoweza kuliendesha. Kwa mfano, mfalme Solomoni alikuwa na ufunguo wa hekima ambao ulimwezesha kufanya makubwa kwenye maisha yake. Na hata wewe ukitaka kufanya makubwa, hakikisha unakuwa na ufunguo wa eneo …

Shida Nyingi Huwa Zinaanzia Hapa

Zinaanzia pale tunapolazimisha mambo yaende kama tunavyotaka sisi. Acha mambo yatokee kama vile yalivyopangwa kutokea. Usitake kuwa kiranja wa dunia wa kutaka kulazimisha mambo yaende kama vile unavyotaka wewe. Iachie asili iamue na kila jambo linalotokea huwa lina kusudi lake. Kwenye kila jambo linalotokea kwako huwa lina fundisho ndani yake. Hata kama ni baya kuna …

Usikubali Kulipa Gharama Hizi Za Kujitakia

Watu wengi wako radhi kulipa gharama kubwa mwishoni baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo kuliko kulipa gharama mwanzoni. Kulipa gharama za akili. Elimu yetu haina mwisho, kila siku ukiamka salama ni siku ya kujifunza tena kwako. Lakini watu wengi wako radhi wasiwekeze kwenye eneo la akili lakini waje walipe riba kubwa baadaye kwa kutafuta maarifa …

Tamaa Mbili Zinazomsukuma Mteja Kununua Kwako

Lengo kuu la biashara ni kutengeneza wateja. Lakini watu wengi wanakuwa wanasema lengo kuu la biashara ni kutengeneza faida. Ndiyo maana biashara nyingi hazifanyi vizuri sana kwa sababu mtu yuko pale kwa sababu ya kutaka kutengeneza faida. Ukiwa ni mtu wa kutaka kutengeneza faida tu, biashara yako itakufa haraka sana. Lakini, ukiwa ni mtu wa …

Kitu Unachopaswa Kulinda Sana Kwenye Maisha Yako

Usikubali mwili ukulazimishe utende matendo ambayo yatavunja heshima yako. Usiuridhishe mwili kwenye kila kitu kwa sababu utaishia kuvunja heshima. Shabaha yangu kubwa kwako leo ni wewe kulinda heshima yako. Linda sifa yako, linda heshima yako. Jiwekee misingi ambayo utaishi na kuisimamia maisha yako yote. Usipokuwa na misingi kwenye maisha yako, utakuwa unakaribisha matatizo. Ila ukiwa …

Hii Ndiyo Hisia Ya Hovyo Kabisa

Ni chuki. Ni bora hisia nyingine zinaweza kukupa raha lakini chuki inakupa raha gani wewe? Zaidi ya kujiumiza wewe mwenyewe? Chuki na malalamiko hayakufanyi upige hatua hata siku moja. Hii ni kama kujikaanga na mafuta yako mwenyewe. Shabaha yangu kwako leo, usiwe na chuki na watu. Usitengeneze maadui kabisa kwenye maisha yako. Wapende watu, hata …

Jinsi Ya Kushika Hatamu Ya Maisha Yako

Wakati wengine wakilalamika, kulaumu na kusubiri wengine wawasaidie kutoka pale walipokwama, lakini mabilionea wameshika hatamu ya maisha yao. Huwezi kumsikia mtu aliyefanikiwa akilalamika kwa kitu ambacho kipo nje ya uwezo wake, kulalamika juu ya jua kuongezeka, joto, umeme, maji ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako. Unachotakiwa ni kununua uhuru wako mapema, upambane, utoke …

Design a site like this with WordPress.com
Get started